Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Kwa Sasa maisha yanaenda Kwa mfumo kuzaa zaa tu ili watoto waje wajitafutie bila kuwatengeneza ili wafiti kwenye mfumo ni kumleta Ili aje ateseke,
Nakubaliana na kwa 100%
 
Reactions: G4N
Ardhi tele uzazi wa mpango sio sahihi kwa Africa still mapori tele ukitoka tu Kibaha mapori kibao walimaji na wafugaji hakuna.
We zaa tu,
 
Wenye watoto tumekuelewa vizuri tu una hoja, ila si rahisi kueleweka kwa akili za kawaida.

Nimeuza asset zangu nyingi sana kila inapotokea school fees inasumbuwa ili mradi wasome shule bora.

Wakati unahakikisha wanapata elimu bora na wewe ndio unazidi kuteketea usipokuwa makini unaweza kukata mwaka hujajikumbuka hata kufanya shopping ya kupiga pamba mpya.
 
😀 😀 😀
 
Dah nakumbukaga mchango wa hasimu wangu mwamba Accumen Mo kwenye uzi flani bonge la mchango mwamba anakuambia watoto wanaleta furaha na faraja wanakupelekea upambane na upigane zaidi kwenye maisha. Napenda sana watoto hasa wa kike.
 
Binafsi naamini hakuna mtu anataka awe na mtoto mmoja au wawili
Exactly hakuna mtu huyo, lakini hali halisi hutaki kutesa kiumbe innocent.

Mimi classmate wangu alikuwa mwana sana school yeye ana watoto 10 sasa hivi na nadhani na wawili kwa mchepuko, yeye hajali mambo ya quality school, shule za kata zipo.
 
anayebisha ameamua kubisha.
 
Watoto wanaleta furaha kama account inapumuwa, kama mambo siyo ukiwaangalia unaweza kulia kwa kujiona una hatia kubwa mbele yao.
 
Mkuu masahihisho. Bushi ana mabinti wawili.

Halafu mwijaku ana mmoja tu.
 
Kwanini unadhani/amini hao walipenda kuwa na watoto wachache?
 
wanaopinga wengi mtakua wasukuma. kuna mmoja msukuma kipindi nabeba tofali tulikua tunabeba naye tofali. amemzalisha mkewe watoto 8 wote wa kike. akawa kuna mkruya anambembeleza amchukue yule wa 2 awe dada wa kazi ili akipata hela amsaidie kulea wenzake. unaona akili hiyo? mtu kama huyu ni wa kumtia sindano ya ugumba. jamaa akamchukua binti akawa anaishia kupigwa na kunyanyaswa na bosi wake.
 
1. Kuna jama moja alidhani akiacha pombe ndo atatajirika, sasa ni takribani miaka nitatu tangu aache pombe, ila umasikini wake unaendelea kua mbaya zaidi.

2. Kuna jama ni jirani ana watoto wa wiwili ila wote wanasoma shule za st kayumba na bado anaendelea kuishi kwenye nyumba ya kupanga wakati mualimu mwenzie ana wake wawili na watoto 8 ila wote amewajengea na baadhi ya watoto wanasoma shule za private.

3. Kuna ndugu yangu ana watoto wawili tu, ila anaenda kwa ndugu zake wampe watoto wa kuka nae kwasbb wa kwake wote wawili wa ligoma kuenda shule na mama yao alisha fariki.

Hakuna uhusiano kati ya idadi ya watoto na maisha mazuri ni issue ya kichwa cha muhusika tu.........jamii ya waarabu inazaliana sanaa hapa Tanzania ila wana maisha mazuri na wa meajiri watu wenye watoto wawili kwanini?
 
So duniani ulizaliwa ufanye nini kama hutakuwa na watoto? Maisha ni mazuri sana ukiwa na familia. Yani hata unavyoenda kupambana kuna spirit inakuongoza na kukupa ujasiri pindi unapoifikiria familia yako. Kupata na kukosa ni matokeo lakini familia kwanza. Kindly mtoa mada angalia wosia wa marehemu usijekuwa mfupi, marehemu alizaliwa, marehemu amefariki, jina la bwana lihimidiwe .......... Pambana uache chata zako Duniani the rest is history!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…