Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Kwahiyo kwa mujibu wa Bibilia “maneno matakatifu ya Mungu” yanaelekeza masikini wasio na uwezo wa kuachia urithi hadi wajukuu basi wasizae watoto?

Mkuu watu wamekua soft sana siku hizi kwa kudhani ujinga na uzembe wao wa kupambania maisha yao ni jukumu la wazazi wao....... haujazaliwa na wazazi wako ili uje kurithi mali zao, umezaliwa ili uje KUISHI swala la utaishi namnagani ni juhudi zako

Uvivu unawafanya watu wanatengeneza maisha ya kufikirika ambayo hayapo kwamba wazazi wote wanapaswa kuwa matajiri na wakifa waache urithi kwa watoto wao....... hipo dunia ya namni hii
 
Mi nitakuuliza: Unataka watoto wawili kwani wewe ni OBAMA?
 
Hiyo tafsiri ni mbovu kumbuka hata iweje hatuwezi kuepuka uwepo wa vibaka mjini hata vijijini, kwan binadamu hatupo sawa ,lakin hii pia imekuja kutupatia maana halisi ya kutegemeana,je kungekua hakuna vibaka polisi wangekua na kazi gani?
Hapo siyo kuacha kuzaa lakin tunatakiwa kuona namna gani mzuri ya kuwafanya hao watoto wapite kwenye njia sahihi ambazo watoto wa miaka 1980 walikua wanapita.

Wanapambaji wengi ambao wanatamba kwa sasa ni watoto wa masikini mfano hansrafael,hamornize,diamond na wengine wengi.
 
Kabisakabisa
 
Mafundisho yadanganyayo Kwa sisi tunaosoma bible tu akuona kabisa kama unatekeleza agenda ya mpinga kristo kuwa watu wasioe hivyo wawakiane tamaa maana matokeo ya kuoa ni kuzaa hivyo unapingana na agizo la mungu kuwa zaeni muongezeke na kuijaza nchi.

Hivyo tamko lako Lina laani uumbaji wako mwenyewe na kukosoa hadi wazazi wako na kuvunja heshima ya wazazi wako( waeshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na bwana mungu wako)
Hivyo kijana umekwisha kuyatimba autaiona sasa laana inayoanza kukuandama ila nakusihi tubu na ulejee miguuni pa muumba wako na makosa yako yatasamehewa ( ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu kama damu utasafishwa uwe kama theruji) akuna dhambi mbaya kama kukufuru.
 
Ukiwa na akili timamu huwezi shadadia kuzaa watoto wengi usioweza kuwamudu.
Zaidi zaidi ni kujiongezea na kuwaongezea shida hao watoto.
Watanzania wengi wanazaa bila mpangolio. Ndio maana kumejaa wahuni kila kona . Mtu ana watoto 6, kapanga chumba kimoja, kipato kwa siku elfu 10 , unategemea nini kwa mtu kama huyo. Unawapa shida watoto wako tu.
 
Watanzania wengi wanazaa bila mpangolio. Ndio maana kumejaa wahuni kila kona . Mtu ana watoto 6, kapanga chumba kimoja, kipato kwa siku elfu 10 , unategemea nini kwa mtu kama huyo. Unawapa shida watoto wako tu.
Shida ipo kwenye mgao wa keki ya taifa hatuna viongozi tuna watawala
 
Yaani nisizae kisa? Kwani huyo Obama ndio mimi? au sijui Clinnton hata nikijifanya nazaa mtoto mmoja nitawafikia kiuchumi? tuzae tu jamani tuzae mapori bado yapo mengi ya kutosha nchi kubwa hii
 
Labda huelewi kuwa nchi zilizokuwa zinazaliana kidogo sasa hivi wanahaha watu wazae.

Unaonesha kwenu ilikuwa mnazaliana mpata watumwa.

AlhamduliLlah, Waislam tunafahamu kuwa watoto ni moja katika furaha za duniani.
 
Kwahiyo kwa mujibu wa Bibilia “maneno matakatifu ya Mungu” yanaelekeza masikini wasio na uwezo wa kuachia urithi hadi wajukuu basi wasizae watoto?
Je katika vifungu vya neno nilivyoviweka hapo juu Kuna maneno yoyote kati ya hayo uliyoweka? Kuna sehemu biblia imeandika masikini wasizae au ni utashi wako tu?

Kasome upya biblia mkuu, hata Mungu hakumuumba Adamu ndio akaanza kuumba vitu. Alianza kuumba vitu, biblia inasema aliumba mbingu na nchi, akaumba bahari. Maana yake hadi anamuumba Adamu na kumuweka bustani ya Eden ikiwa na kila kitu. Adamu alikula bata bustani ya Eden, aliishi soft life, hakutafuta kuni za kupikia wala kubeba mizigo kila kitu Mungu alikuwa amemuwekea kasoro mwanamke.

Turudi kwako wewe, ikiwa Mungu alifanya yote haya kwa Adam, wewe masikini huna kitu where do you get moral authority ya kuzaa zaa hovyo bila kuwaandalia watoto mazingira mazuri mwishowe wanakuwa chokoraa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…