Watoto na wajuku zako watanunua viwanja vya kujenga wapi?

Watoto na wajuku zako watanunua viwanja vya kujenga wapi?

Hii nchi bado mapori ni mengi mno. Wewe kama unaharaka na ardhi kazi kwako ila tuliotembea hii nchi vizuri lamda tuje tuwe na raia pacha ndio nchii hii itajaa.
Nchi bado ni tupu. Watu wa Dar mje muwekeze huku. Labda Hizi industrial parks zinazoota huku Pwani zitasaidia kiuchumi. Ila bado nchi iko tupu. Masuala ya kubanana Dar inabidi yapungue
 
Ivi mnajua kuwa hii nchi ina ardhi kubwa sana we wakat una safir angalia nje ndo utajua mda mwingine unawaza hivi kweli kutakuja kujengwa huku kote, Pia mbuga za wanyama nazo si ardh pia [emoji849][emoji849][emoji849]
 
Ukiwa una papara Dar unaweza kuiona imejaa, lakini hadi kesho kuna viwanja vingi tu vya bei nafuu... Tatizo lenu mkipata hela kidogo mna wehuka mnapata kiherehere na ushamba wa pesa, kiwanja cha million 5-10 unaambiwa million 20. Kama hadi leo hii Tabata, Kinyerezi, Kimara, Tegeta, Boko, Mbezi n.k kuna viwanja vingi tu vizuri mnasemaje kumejaa???
Ukiwa una papara ya kununua kiwanja hata Katavi au Tabora kumejaa hakuna viwanja...
Wewe ni dalali sivyo?
 
Waruhusu watu binafsi wamiliki ardhi Ili izalishe haina faida ikikaa tu
Wawape wananchi fidia kisha wapewe wenye hela zao wawekeze kwa haki bila dhuruma. Sio kukaa nayo tu nyasi zinaota tu. Hii itachochea uwekezaji na fdi nyingi na kutengeneza ajira. Hii ya watu kubanana kwenye miji bila kazi ndio inaleta uhalifu.
 
🤣🤣
Nchi iko tupu sana.
Hivi naweza kwenda serikalini, halmashauri au kwa mkurugenzi kuomba sehemu open space kwa ajili ya kufanya labda kilimo?.. maana sehemu Nyingi ipo wazi au hata hizo sehemu tunazoziona ziko wazi zimeshamilikiwa na watu?
 
Dogo usikariri kuishi si lazima uwe katikati ya mji, maisha ya familia inapendeza zaidi yakiwa nje ya mji sehem ambayo hakuna kelele za magari wala pikipiki au bar, sehem zenye changanyikeni ni nzuri kibiashara tu na siyo kuishi
 
Serikali ya kijiji unaeza ukaomba eneo. Au ukakodi kwa wazawa au kununua kwa wazawa. Ila ufatilie eneo lisiwe na migogoro ya wakulima na wafugaji. Au wanyama wa porini kama tembo, ndege au ngedere kama wanapita hapo. Au historia ya mafuriko au ukame.
 
Nimekuelewa kaka, Lakini nafikiria umbali kutoka sehemu ulipojenga mpaka eneo lako la kazi, Yuko rafiki yangu anauza vitunguu Hapo stereo temeke, Lakini kanunua kiwanja kibaha na kaanza kuweka mawe, kama unavyojua biashara za sokoni ni asubuhi saa 11 mpaka saa 4 Mwisho, atawezaje kufika kwa wakati?
 
Serikali ya kijiji unaeza ukaomba eneo. Au ukakodi kwa wazawa au kununua kwa wazawa. Ila ufatilie eneo lisiwe na migogoro ya wakulima na wafugaji. Au wanyama wa porini kama tembo, ndege au ngedere kama wanapita hapo. Au historia ya mafuriko au ukame.
Sawasawa
 
Pia kila halmashauri huwa wana idara ya ardhi. Huwa wanauza maeneo kwa ajili ya biashara, makazi, viwanda, uwekezaji n.k. Bei ni kwa square meter. Huwa ina range 1500 kwa sqm mpaka 20000 inategemea na matumizi na halmashauri husika.

Serikali ingeanzisha viwanja portal ili viwanja vyoote vinavyouzwa na halmashauri matangazo yawe centralized ili kila mtu apate taarifa
 
Back
Top Bottom