Watoto ni gharama si baraka. Kabla hujafikiria kuzaa watoto tambua hili mapema

Watoto ni gharama si baraka. Kabla hujafikiria kuzaa watoto tambua hili mapema

We na huyo mwanamke mtakao kaa kujadili wote wapuuzi

Hivi mtu unaweza kupanga jinsi ya mkumlea mtoto maana mtoto kwa mzazi hakui sasa we unajua maisha yako kesho yatakuaje au unaweza kupanga plan ya sio chini ya 35 yrs
 
Wewe ndio Mwanaume sasa. Ila unaweza usiombe mtu chakula lakink ukazaa unawalisha mihogo kila siku na wengine wanaishia kujiuza kwa maisha magumu.
Mtoto wa obama {mkubwa} ushawahi futatilia status zake?

Kujiuza sio sababu ya kuwa na maisha magumu. nitabia ya mtu tu sawa na kutumia madawa ya kulevya na kuwa shoga nk. jiulize wewe ukiwa na maisha magumu unaweza kujiuza?

mbona akina gigy money wanajiuza licha ya kuwa na maisha mazuri nk? hamna point zingine mkuu?

zipo family nyingi tu za kimasikini lakini watoto wao sijawahi waona wakijiuza nk.
 
Unataka msaada gani?
Wa kifedha au mawazo?
WA MAWAZO NA HATA PESA KAMA UNAYO .

wawili wapo private mkuu mwingine hajaanza nimeshajipangia nitazaa watoto 5-7 kama nitakuwa na afya njema pamoja na wife. nikishindwa kusomesha private wanarudi kayumba. ninachoomba ni afya tu
 
Nianze kwa kusema Watoto si Baraka, Watoto ni Gharama.
Kabla hujafikiria kuleta kiumbe kwenye hii dunia tambua hili mapema.

Kabla ya kufikiria kuzaa watoto hapa duniani, Kaa chini wewe na mwenza wako mpange kabisa namna mtakavyo lea na kuhudumia watoto wenu hadi watakapo fika umri wa kujitegemea.

Kuna maelfu ya watoto maskini wanateseka sana hapa duniani kutokana na ujinga, uzembe na upumbavu wa wazazi wanao zaa hovyo hovyo kama mapanya bila malengo wala uwezo wa kutoa huduma na malezi.

Na hili ni janga kubwa sana kwa nchi maskini hasa barani Afrika.

Mtu maskini akizaa mtoto anaongeza maskini mwingine duniani na anaipa serikali mzigo mzito wa kugharamia ujinga wake na umaskini wa kizazi chake.

Wazazi maskini huzaa watoto kwa dhana uchwara kwamba
"watoto ni baraka" Lakini ndio haohao wa kwanza kutelekeza familia zao, kukwepa majukumu na uwajibikaji na wengine hufikia hatua hadi ya kuua au kujiua wao na familia zao kwa kigezo kwamba maisha ni magumu.

Kabla mtu hujafikiria kuzaa watoto kwenye hili dunia, Tambua kwamba, Maisha hayajawahi kuwa marahisi, Maisha si rahisi na Maisha hayatakuja kuwa marahisi kwa watu wazembe, wajinga na maskini.

Ewe kijana kabla hujafungua hiyo zipu yako kuleta watoto, Tambua kwamba Dunia haina huruma na haitakuja kukuonea huruma wewe na kizazi chako. Jipange na hakikisha uko vizuri kiuchumi.

Ewe binti kabla hujapanua hayo mapaja, tambua kwamba dunia haina huruma na haitakuja kukuonea huruma wewe na kizazi chako.

Kabla mtu hujafikiria kuzaa watoto kwenye hii dunia, tambua kwamba una wajibu wa kuhudumia na kulea hicho kiumbe wewe mwenyewe, Sio kulia lia kuanza kusumbua watu, ndugu, jamaa na marafiki wakusadie malezi, pesa au mahitaji kwa wanao uliozaa wewe mwenyewe.

Mwanaume kama unajua huna uwezo wa kuhudumia funga hiyo zipu. Mwanamke kama unajua huna uwezo wa kuhudumia usivue chupi.

Hakuna mtu anakusaidia kuzaa watoto kwenye hii dunia.Vivyo hivyo Usitegemee uje usaidiwe kulelewa watoto wako.

Watoto si baraka, Na Hakuna Mungu wa kuja kukusaidia kulea wanao. Kama una hii dhana futa huko kichwani. Ukishaleta mtoto kwenye hii dunia tambua kwamba wewe mwenyewe ndiye utawajibika kuhudumia.

This world 🌍 is not for the weak, ignorant, lazy and poor people.
You either go hard, go home or you die.

In the jungle of life salvation is largely on your hands.

Hakuna Mtu au Mungu wa kukuhurumia wewe na kizazi chako.

I'm out.
Loud and clear
 
Gigy ana maisha gani mazuri? Unafata mkumba wa maigizo ya media🤣🤣🤣
Haijarishi huyo nimeweka tu kama mfano mbona wapo wengi lukuki?

Narudia kujiuza,madawa ya kulevya, ulevi,ushoga nk ni tabia ya mtu tu haiingiliani na umasikini.

nina mfano..... ndg yangu mtoto wake alishindwa kusoma seminari akafukuzwa akiwa form3 dogo akagoma kusoma mazima na kuzama dar jitihada kadhaa za kumrudisha home pamoja na kumtafutia kazi lkn wapi akawa mtoto wa mitaani tu hana makao. baada ya naisha kumnyoosha akarudi saivi ana duka la simu mtaji kapewa na wazazi wake
 
Compare and contrast
 
What if, wazazi wako wasingekuleta duniani kwa kumfikiria dhana hiyo na ikizingatiwa wewe si mtoto wa kwanza, usiogope majukumu we fyatua tu maana Mungu na shetani wanatupia jicho hapo hapo.
Haya maelezo mepesi sana mkuu,,ikumbukwe wewe kuzaliwa ni either walipanga watu wawili wewe ukiwa haupo au hawakupanga wewe ukatokea kama bahati mbaya kwa hivyo hata wasingekuleta duniani siyo issue kwa maana ndiyo hivyo hawajakuleta,,lakini kumleta duniani mtu halafu aje ataabike huo ni uzwazwa mleta mada yupo sahihi 100%
 
Hahahaa
 
Nina watoto kumi na tatu, watoto 13 na ninawapenda . Ninawapenda wote. Na ninafikiri nimekuwa baba-bora kwa kila mtoto kwa watoto wangu wote 13.
 
Back
Top Bottom