Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Ukijamba mkiwa wa 3 wakati wa kula usiku mezani lazma utafutwe ata kwa kunuswa!!! Ukijuwa utagundulila bora utoke nduki ukalale kwa mjomba kuepuka kipigo kisicho kuwa na kipimo!!
Maana ukichapwa ukaendela kulia zoezi Lina anza upya! Ukichapwa ukajamba tena zoezi linaanza tena Automatic!!
 
Aisee
 
Ukifeli mitihani utachapwa:
Jirani alimkuta dogo amekaa barazani akilia. Alipoulizwa sababu ya kulia akasema nilikuwa nimekaa tu sebuleni ghafla baba akaja na kunichapa. Jirani kaona hapa dogo ameonewa na alipokutana na mzazi alimwuliza nini sababu ya kumchapa dogo wakati hajafanya kitu? Baba akamjibu: "Ni hivi, kesho atapata matokeo yake ya mitihani, na kawaida yake anafeli na ninamchapa! Lakini kesho mimi nitakuwa safarini, kwa hiyo nimeitanguliza kichapo!"
 
hapo kwny kuimba kawimbo baada ya kuchapwa ni mimi kabisa huyo.

Na kula taratibu,ilibidi niwe naanza kukaa mezani kbl ya wengine lkn bado watakuja kula na wataniacha.Fimbo zake sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…