Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Ukijamba mkiwa wa 3 wakati wa kula usiku mezani lazma utafutwe ata kwa kunuswa!!! Ukijuwa utagundulila bora utoke nduki ukalale kwa mjomba kuepuka kipigo kisicho kuwa na kipimo!!
Maana ukichapwa ukaendela kulia zoezi Lina anza upya! Ukichapwa ukajamba tena zoezi linaanza tena Automatic!!
 
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaangua kicheko, utachapwa.
27. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
28. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
29. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
30. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
,,N.K
*Kama umepitia malezi haya na bado ukakosa heshima basi wewe ni KONKODI. Kinga ni bora kuliko tiba.

Jr[emoji769]
Aisee
 
Ukipata ZIRO utachapwa tu hamna namna!
[emoji23][emoji23]
IMG-20190401-WA0056.jpeg


Jr[emoji769]
 
Ukifeli mitihani utachapwa:
Jirani alimkuta dogo amekaa barazani akilia. Alipoulizwa sababu ya kulia akasema nilikuwa nimekaa tu sebuleni ghafla baba akaja na kunichapa. Jirani kaona hapa dogo ameonewa na alipokutana na mzazi alimwuliza nini sababu ya kumchapa dogo wakati hajafanya kitu? Baba akamjibu: "Ni hivi, kesho atapata matokeo yake ya mitihani, na kawaida yake anafeli na ninamchapa! Lakini kesho mimi nitakuwa safarini, kwa hiyo nimeitanguliza kichapo!"
 
hapo kwny kuimba kawimbo baada ya kuchapwa ni mimi kabisa huyo.

Na kula taratibu,ilibidi niwe naanza kukaa mezani kbl ya wengine lkn bado watakuja kula na wataniacha.Fimbo zake sasa
 
Back
Top Bottom