Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Poleeee
 
Zamani hata mahali alipoketi mtu mzima akainuka ,nawe ukakimbilia kuketi utachapwa tu ,hata kama kiti kiko wazi kaa mbali nacho
 

Mlikuwa vilaza sana no wonder Baba bashite anafanya aliyofanya anadhani tuko enzi zenu.
 
Zamani sikukuu zote ndugu wanatembeleana majumbani na Kula pamoja lakini siku hizi beach, club, disko, live band ndo mpango mzima
 
Mkuu samahani miaka hiyo na karne hii upo na unapost jf shikamoo mkuuu
Marhaba kijana wangu... mbona humu wakongwe tupo wengi tuu

Enzi hizo tunaenda shule peku 14KM, njiani kuna simba na chui..

Ngoja nilale bibi yenu ameniita..... nikipata time ntarudi kesho
 
Marhaba kijana wangu... mbona humu wakongwe tupo wengi tuu

Enzi hizo tunaenda shule peku 14KM, njiani kuna simba na chui..

Ngoja nilale bibi yenu ameniita..... nikipata time ntarudi kesho
Haya babu usiku mwema
 
*WATOTO WA SIKU HIZI HAWAJUI KABISA ENZI ZETU UNAWEZA KUCHAPWA KWA SABABU ZIFUATAZO:*
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
,,N.K
*Kama umepitia malezi haya na bado ukakosa heshima basi wewe ni KONKODI*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…