Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Ukikojoa kitandani
Utachapwa.
Usipoenda shule
Kesi
Usipoosha vyombo kisa mwanamme
Kesi
Ukiwachungulia wanawake chupi
Utachapwa
 
Sio uongo kabisa wazee wamekunywa maji ya bendera kuna mdogo wangu anaipenda chadema ila akiwa na mzee mdogo wang akisema ubaya wa ccm yan mzee ananuna mpaka ana sahau kama huyo ni mwanae
hahahah...huyo mzee ni mkoloniii[emoji38][emoji38][emoji38]
 
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena

2. Umechapwa hukulia utachapwa tena

3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa

4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa

5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa

6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .


7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa

8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa

9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.

10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.

11. Usiposalimia wageni, utachapwa

12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.

13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.

14. Ukikataa kula, utachapwa..

15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa

16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.

17. Kujitia kisirani, utachapwa.

18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.

19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.

20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.

21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.

22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.

23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.

24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.

25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.

26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.

27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.

28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.

29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.

30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila ya wakubwa,utachapwa

31.Ukinawa bila ya wakubwa,Utachapwa

32.Ukimaliza kula ukanyanyuka bila ya wakubwa,Utachapwa

33.Umechelewa kutoka dukani,Utachapwa
34.U..........

KAMA UMEPITIA MALEZI HAYA NA UKAKOSA HESHIMA BASI WEWE NI KONKODIII

-kijiji cha ujamaa
-wadudu wana maajabu
-Nondo mla watu
-sadiki na sikiri
1: Nani atamfunga paka kengele?
2: Sikulamba sukari
3: Mua uliozamisha meli
4: Hawafu mwenye nguvu
5: Sizitaki mbichi hizi
6: Sadiki na Chitemo
7: Juma na Uledi
8: Chopeko na mnofu
9: Kibanga ampiga mkoloni
10: Siku ya gulio Katerero

[HASHTAG]#OldSkulz[/HASHTAG]

Wengine hatujapitia ila ni maisha flani hivi amazing[emoji1531][emoji1531]
 
Ng'ombe wakizamia mashambani
Utachapwa

Usipooga utachapwa

Ukioga usitakate utachapwa

Ukiachwa nyumbani usipofagia uwanja utachapwa

Ukifagia na using'oe vijani utachapwa

Usipoandika darasani utachapwa

Ukiandika ila mwandiko mbaya utachapwa
Usipokariri tebo utachapwa
Ukikariri tebo ukasahau kidogo utachapwa
Usipolima utachapwa
Ukilima ungoe mmea utachapwa

Dah yaani umenikumbusha mbali mjinga wewe
 
Kuchapa mtoto ni ujinga mwingine mwafrika anauendeleza.
 
Back
Top Bottom