1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa..
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila ya wakubwa,utachapwa
31.Ukinawa bila ya wakubwa,Utachapwa
32.Ukimaliza kula ukanyanyuka bila ya wakubwa,Utachapwa
33.Umechelewa kutoka dukani,Utachapwa
34.U..........
KAMA UMEPITIA MALEZI HAYA NA UKAKOSA HESHIMA BASI WEWE NI KONKODIII
-kijiji cha ujamaa
-wadudu wana maajabu
-Nondo mla watu
-sadiki na sikiri
1: Nani atamfunga paka kengele?
2: Sikulamba sukari
3: Mua uliozamisha meli
4: Hawafu mwenye nguvu
5: Sizitaki mbichi hizi
6: Sadiki na Chitemo
7: Juma na Uledi
8: Chopeko na mnofu
9: Kibanga ampiga mkoloni
10: Siku ya gulio Katerero
[HASHTAG]#OldSkulz[/HASHTAG]