adrenaline
JF-Expert Member
- Jun 17, 2015
- 3,152
- 4,843
Lazima utafutiwe sababu..tena kina mama.hahaha.....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lazima utafutiwe sababu..tena kina mama.hahaha.....
Usipoenda madrasa
Ha ha ha ha haUkivaa chupi mpya wakati za zamani zipo utachapwa..[emoji12][emoji12][emoji12]
Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha, mazingaombwe ya akina Profesa Eyeso; Nilikuwa nasononeka sana ku miss mazingaombwe ya huyu Prof! Uncle akigoma kunipa 'mpunga' wa kuona mazingaombwe na nikaonyesha uso wa huzuni nachapwa. Solution ni kuvaa uso wa furaha.Aseee vyote nimepitia ......nilichelewa kurudi home kisa nilikua naangalia mazingaombwe ...nikafukuzwa home na maza na kipigo juu ....nikisusa kula kipigo na kufukuzwa juu yaani ni balaa juu ya balaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahahaah yaani maza alikua ananipa pesa yeye mwenyewe niende ila nikirudi saa moja usiku nafukuzwa na kipigo cha mbwa koko dah......Ha ha ha, mazingaombwe ya akina Profesa Eyeso; Nilikuwa nasononeka sana ku miss mazingaombwe ya huyu Prof! Uncle akigoma kunipa 'mpunga' wa kuona mazingaombwe na nikaonyesha uso wa huzuni nachapwa. Solution ni kuvaa uso wa furaha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwa sisi tuliokulia vijijini naomba usitukumbushe zahma hizo, ni balaa.1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaangua kicheko, utachapwa.
27. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
28. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
29. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
30. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
,,N.K
*Kama umepitia malezi haya na bado ukakosa heshima basi wewe ni KONKODI. Kinga ni bora kuliko tiba.
Jr[emoji769]
Duuh!Hahahahahahaah yaani maza alikua ananipa pesa yeye mwenyewe niende ila nikirudi saa moja usiku nafukuzwa na kipigo cha mbwa koko dah......
Sent using Jamii Forums mobile app
Sure!Ukianza kumega kitoweo kabla ya chakula.. Utakatwa jicho hilo mpaka unashika adabu yako.
Tulikuzwa na mihogo ya kuchemsha, viazi, uji wa dona, mahindi ya kuchemsha. Maandazi mpaka mfuko wa mzee baba utune.Halafu walitufundisha kushukuru.
Hakuna kususa susa.. Sio vitoto vya sasa usipolipia king'amuzi tu.. Wanakununia wao na mama yao. Enzi zetu ukicheka cheka ovyo tu unachapwa.. Ukikasirika unachapwa..
Madrasa [emoji23][emoji23] kucheza mpira kumenifanya nitege sana madrasa na ilkua lazima baba ajue. Kilichofata ni kulala mapemaUsipoenda madrasa
Usipoenda Sunday school
Jr[emoji769]