Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Hahahahahaahahhaahah nimecheka sana ile staili kiboko......unafumuliwa vizuri tena ukute mboga kidogo halafu wewe unakula ulaji wa hovyo uuuwi

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aisee tume teswa sana.
Sasaivi watoto wana towea mchuzi mbele ya babazao, wana chukua nyama bila kuambiwa kama wazee daah.

Mitoto ya sikuhizi inaweza kumwambia mzazi "mshenzi we" na mzazi akakenua meno tu......

Mimi mama yangu ni mkali vibaya mnooo hata Leo nikimtibua karibu yake Kofi linanihusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hapo! Ndo kumesababisha enzi hizi kuwa na kichwa. Siku hizi hakuna viboko basi balaaa.
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaangua kicheko, utachapwa.
27. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
28. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
29. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
30. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
,,N.K
*Kama umepitia malezi haya na bado ukakosa heshima basi wewe ni KONKODI. Kinga ni bora kuliko tiba.

Jr[emoji769]

Ukipata ZIRO utachapwa tu hamna namna!
 
Hahahahhahahahahaha nielekeze huu mfuko wa kijaruba upoje mkuu
Miaka ya themanini kuna watu waliibuka kutengeneza mifuko kwa kutumia Ukili (Ukindu) na baadhi ya wazazi wa Uswahilini hasa ndiyo ilikuwa mifuko ya kubebea madaftari kwa watoto wao. Baadae hata magunia ya juche yalitumika pia.

Ukifunua Kawa lililofunikia chakula cha baba mwenye nyumba, utachapwa!!
 
Back
Top Bottom