Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

😂😂😂uwii mkuu mbavu zangu
Ukijamba mkiwa wa 3 wakati wa kula usiku mezani lazma utafutwe ata kwa kunuswa!!! Ukijuwa utagundulila bora utoke nduki ukalale kwa mjomba kuepuka kipigo kisicho kuwa na kipimo!!
Maana ukichapwa ukaendela kulia zoezi Lina anza upya! Ukichapwa ukajamba tena zoezi linaanza tena Automatic!!
 
Umeenda kuoga mara sabuni ikadondoka chini ikawa na mchanga .utachapwa tu.
 
Kukalia kiti anachotumia mzee.. Utachapwa.
Kutumia sahani na vikombe vya dingilai yani hapo ni kama umeisiga na kuikanyaga katiba.. Mahakama ya baba mkazi lazima ikuhusu. Ni viboko mbele ya watoto wengine halafu unakiri kosa, na adhabu ndogo ndogo kufagia banda la kuku wiki nzima...
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Dah usipofanya homework hauchapwi....[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Ukimwambia mtu kuwa yeye kwamba ni.

Underdog - utachapwa

Ukimdhihaki mtu kuwa ni yeye ni mtu wa,

Hovyohovyo - utachwapwa

Ila Kama ni Swahiba wa Mtukufu huchapwi.
Wala huruhusiwi kumwomba radhi mtu yoyote hata kama umemkosea.
Kwakuwa Unakuwa ni Kipenzi Pekee cha cha Mtukufu.

Chifu wa Kabila Lenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifumwa unatoka direction ya jikoni na tuchembe chembe twa sukari pembeni ya mdomo, halafu unaulizwa nini hiyo mdomoni, "Mara unajibu oooh sijui iiiiih" hutoi Maelezo yaliyonyooka, Kumbe umetoka kulamba sukari jikoni.
Lazima uchapwe tu.
 
Ukisumbua kanisani ukirudi nyumbani utachapwa
Ukipewa sadaka ukala pipi utachapwa

Ukichelewa sunday school unachapwa



God first
 
Ukijamba mkiwa wa 3 wakati wa kula usiku mezani lazma utafutwe ata kwa kunuswa!!! Ukijuwa utagundulila bora utoke nduki ukalale kwa mjomba kuepuka kipigo kisicho kuwa na kipimo!!
Maana ukichapwa ukaendela kulia zoezi Lina anza upya! Ukichapwa ukajamba tena zoezi linaanza tena Automatic!!
Ha ha ha ha ha Aisee nimecheka kinoma
 
1.Ukiagizwa dukani na mama ukaonyesha kukasirika utachapwa.
2. Ukikutwa unaangalia miziki ya kizungu wamevaa vibaya utachapwa.
3. Mtoto wa jirani akikupita shuleni utachapwa.
4. Ukivunja sahani au kikombe cha udongo viboko.
5. Ukidondosha chenji utakula mboko.
6. Ukicheza mvua inanyesha utachapwa [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from Nokia 7 Plus
 
Ukianza kumega kitoweo kabla ya chakula.. Utakatwa jicho hilo mpaka unashika adabu yako.

Tulikuzwa na mihogo ya kuchemsha, viazi, uji wa dona, mahindi ya kuchemsha. Maandazi mpaka mfuko wa mzee baba utune.Halafu walitufundisha kushukuru.

Hakuna kususa susa.. Sio vitoto vya sasa usipolipia king'amuzi tu.. Wanakununia wao na mama yao. Enzi zetu ukicheka cheka ovyo tu unachapwa.. Ukikasirika unachapwa..
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. ukimuomba mgeni hela utachapwa
2. Ukimtizama mkubwa jinsi anavyokula utachwapa
3. Ukigoma kuoga utachapwa
4. Ukichafuka baada ya kuoga utachapwa
5. Ukipata 98% kwenye mtihani utachapwa kwann hukupata mia
 
Back
Top Bottom