Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Ukijamba mkiwa wa 3 wakati wa kula usiku mezani lazma utafutwe ata kwa kunuswa!!! Ukijuwa utagundulila bora utoke nduki ukalale kwa mjomba kuepuka kipigo kisicho kuwa na kipimo!!
Maana ukichapwa ukaendela kulia zoezi Lina anza upya! Ukichapwa ukajamba tena zoezi linaanza tena Automatic!!
Hahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiweka kiwembe kwenye kaptula ya Shule mama wakati anafua akakikuta aisee kichapo chake balaa...[emoji23][emoji23]

Ukila kwa jirani kichapo...

Usiposalimia asubuhi kichapoo...

Ukipigwa ukasusa chakula eti usilee ukaenda kulala aisee mboko zitakufata huko kitandani hutaamini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukivaa nguo za kike nawewe ni wakiume lazima Nichape

Ukichelewa kuoga,Usiku unaogeshwa maji ya baridi (kwa tuliokulia sehemu za baridi)
 
Kwa wale wenzangu wa chandimu, umetoka shule badala ya kwenda nyumbani, mkaweka mawe barabarani mkaanza kucheza mpira. Hiyo hata atokee jirani tu anayekufahamu, utakula kipigo halafu anakushika shati hadi nyumbani huko ndo utaenda kukutana na holy brutal
 
Halafu ukifanya kosa mtaani mfano mkikutwa mnapigana,anaweza atokee mzee yeyote ambaye hata hawafahamu akawachapa na ukienda kusema nyumbani utachapwa tena

Sent from my TECNO F1 using Tapatalk
 
Furaha ilikua pale mzazi anataka akuchape mara paap anatokea mgeni, halafu anasena mwache mtoto

Sent from my TECNO F1 using Tapatalk
 
Ukifeli mitihani utachapwa:
Jirani alimkuta dogo amekaa barazani akilia. Alipoulizwa sababu ya kulia akasema nilikuwa nimekaa tu sebuleni ghafla baba akaja na kunichapa. Jirani kaona hapa dogo ameonewa na alipokutana na mzazi alimwuliza nini sababu ya kumchapa dogo wakati hajafanya kitu? Baba akamjibu: "Ni hivi, kesho atapata matokeo yake ya mitihani, na kawaida yake anafeli na ninamchapa! Lakini kesho mimi nitakuwa safarini, kwa hiyo nimeitanguliza kichapo!"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom