Watoto wa viongozi wakuu wa nchi walipwe ili kuwatia moyo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
WATOTO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIPWE ILI KUWATIA MOYO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.

Lakini ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa na watoto wa viongozi wa taifa letu tukufu.

Watoto wa Marais Walipwe.
Watoto wa Makamu wa rais Walipwe.
Watoto wa Spika wa bunge walipwe
Watoto wa Waziri Mkuu walipwe!
Watoto wa Jaji Mkuu walipwe.
Watoto wa Ma-IGP walipwe.
Watoto wa Wakurugenzi wakuu wa TISS walipwe.

Wapewe Mishahara hata milioni moja au mbili au tatu hivi kwa mwezi. Hayo ndio maendeleo. Wazazi wao wanatumikia nchi hilo nani atabisha?

Wazazi wao wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kuhangaikia nchi, nani anabisha? Wazazi wao wanatukanwa na wananchi wakati mwingine bila kosa nani anabisha?

Walipwe! Walipwe! Tuwalipe! Kodi ni zetu na wao ni viongozi wetu. Tunafurahi wakilipwa. Sisi tutawatumikia kama wao wanavyotutumikia ili kuiendeleza nchi.

Watoto wa viongozi jiandaeni. Tutawalipa kila mwezi. Ni bora tuwalipe tuu kuliko mjilipe wenyewe kwa kificho. Hata tusipowalipa tunajua mtajilipa kivyovyote tuu.

Muswada upelekwe bungeni, kisha upitishwe. Watoto nao walipwe.
Ambao hawataki wahame nchi.

Tusiishie kuwalipa Wenza wao(waume na wake zao) twendeni mbele zaidi. Tuwe na jicho la mbali kama tai.

Mimi nimemaliza, hayo ni mawazo yangu. Kama hutaki hayo ni mawazo yako na kwangu sio shida.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Naunga mkono hoja, ila malipo hayo sio kwa ajili ya kuwatia moyo bali ni compensation of loss of parental love and parental quality time with their children and kupunguza mateso ya ridicule kwa wazazi wao, wao ndio waathirika.

P
 
Walala hoi walipwe ili kuwatoa umaskinini🤔
 
Naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…