Watoto wa viongozi wakuu wa nchi walipwe ili kuwatia moyo

Watoto wa viongozi wakuu wa nchi walipwe ili kuwatia moyo

WATOTO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIPWE ILI KUWATIA MOYO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.

Lakini ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa na watoto wa viongozi wa taifa letu tukufu.

Watoto wa Marais Walipwe.
Watoto wa Makamu wa rais Walipwe.
Watoto wa Spika wa bunge walipwe
Watoto wa Waziri Mkuu walipwe!
Watoto wa Jaji Mkuu walipwe.
Watoto wa Ma-IGP walipwe.
Watoto wa Wakurugenzi wakuu wa TISS walipwe.

Wapewe Mishahara hata milioni moja au mbili au tatu hivi kwa mwezi. Hayo ndio maendeleo.
Wazazi wao wanatumikia nchi hilo nani atabisha? Wazazi wao wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kuhangaikia nchi, nani anabisha? Wazazi wao wanatukanwa na wananchi wakati mwingine bila kosa nani anabisha?

Walipwe! Walipwe! Tuwalipe! Kodi ni zetu na wao ni viongozi wetu. Tunafurahi wakilipwa. Sisi tutawatumikia kama wao wanavyotutumikia ili kuiendeleza nchi.

Watoto wa viongozi jiandaeni. Tutawalipa kila mwezi.
Ni bora tuwalipe tuu kuliko mjilipe wenyewe kwa kificho. Hata tusipowalipa tunajua mtajilipa kivyovyote tuu.

Muswada upelekwe bungeni, kisha upitishwe. Watoto nao walipwe.
Ambao hawataki wahame nchi.

Tusiishie kuwalipa Wenza wao(waume na wake zao) twendeni mbele zaidi. Tuwe na jicho la mbali kama tai.

Mimi nimemaliza, hayo ni mawazo yangu. Kama hutaki hayo ni mawazo yako na kwangu sio shida.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Hii nchi tunapoelekea sijui maana wanasiasa wanazidi kuleta machukizo makubwa ndani ya jamii
 
Nimejaribu kuisoma hii habari kwa umakini ili nione kama upo serious or not. Hadi sasa sijajua kama umedhamiria kabisa iwe hivi au umeleta utani. Kama upo serious kabisa na unatamani iwe hivi, nimekutukana matusi yote yale makubwa makubwa siandiki hapa maana nitapigwa ban.

Nitukane mkuu. Nitawaomba Mods Kwa uamuzi wangu na hiyari yangu mimi mtukanwaji ambaye ndiye mlengwa na ninayetakiwa kulalamika, wasikupige Ban wala wasikupe adhabu yoyote.

Tukiachana na hasira zako, nini ambacho kimechochea hasira zako kutokana na maoni yangu?
 
Tusiishie hapo tu hata wakwe zao yaani ukioa au kuolewa kwenye familia ya kiongozi pia ulipwe, ndugu wajomba mashangazi mabinamu na wajukuu wote walipwe.

Mpaka wafanyakazi wa ndani na wafungua mageti na madereva pia walipwe na serikali tena.

Maoni yangu naomba yaheshimiwe.👆✌️
 
Machawa watalipwa na Maboss zao.
Ila sisi wananchi tumeamua kulipa watoto wa viongozi wetu.
Ninyi wenye wivu hamna nafasi. Gombeeni muwe viongozi ili nanyi tuwalipe. Kwani shida nini
Tena waambie kabisa wagombee hadi wahakikishe wanashinda. Wakishindwa wagombee tena. Nchi tamu sana hii[emoji3]
 
Nimejaribu kuisoma hii habari kwa umakini ili nione kama upo serious or not. Hadi sasa sijajua kama umedhamiria kabisa iwe hivi au umeleta utani. Kama upo serious kabisa na unatamani iwe hivi, nimekutukana matusi yote yale makubwa makubwa siandiki hapa maana nitapigwa ban.
kuna elimu ya utani,unafiki na uzandiki ilikua inatolewa CUBA nafikiri wewe hukubatika kuchaguliwa kusomea hii kozi?
 
Watoto wa kamishna wa magereza walipwe.
Watoto wa kamishna wa zimamoto na uokoaji walipwe.
Watoto wa kamishna wa tra walipwe
Kamishna wa madawa ya kulevya
Watoto wa watumishi wote wa umma walipwe maana sisi watumishi tunafanya kazi kwa uzalendo
 
Machawa watalipwa na Maboss zao.
Ila sisi wananchi tumeamua kulipa watoto wa viongozi wetu.
Ninyi wenye wivu hamna nafasi. Gombeeni muwe viongozi ili nanyi tuwalipe. Kwani shida nini
mkuu watoto wao wanunuliwe crown au subaru forester halafu ziwe na plate number maalumu ili wasisumbuliwe barabarani
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Kuna hawa wanoitwa "chawa" me nadhani na wenyewe waingizwe pay rol mana na wenyewe wana sifa kama za "wake za Viongozi" au hili unalionaje ndugu mwandishi?
Jomba unataka kusemaje?. Kwamba Viongozi nchi hii ni wanaume tu?[emoji3]
 
Back
Top Bottom