Kiukweli kuna Watu mnapenda kujipa kazi sana,
Hivi hata mambo ya mitandaoni mnaumizwa nayo kiasi hiki jamani!?
Kama wakerwa sana na kitu jiepushe nacho, hupendi kuwaona hao humu JF basi jitoe wewe ili ubaki na Amani,
Dhambi ya Ubaguzi ni mbaya na hua haina kikomo,
Kuna single moms humu hutukanwa kila leo, kuna wale wa Dini hutukanana kila leo, huko kwenye Siasa ndio balaa, sasa wewe kuliko kuamrisha wenye Forum wawafungie watu usiowataka ni aidha wewe ujitoe au usishiriki kabisa kwenye mada za namna hiyo,
Ila ajabu kila Mada za Ushoga nawe umo, sijui wataka tukueleweje.