Watoto waliozaliwa tumbo moja kuwa na uadui

Aisee mm nimeshuhudia jirani zangu kabisa wale watoto ni mama mmoja na baba mmoja lakini hawapendani hata kidogo mpaka huwa nauliza wanamatatizo gani? Maana ilifikia kipindi wanachomeana nguo wanashikiana visu sijajua tatizo huwa ni nini
Mmh hao ni too much

Wanaishi eneo moja?
 
Kabisa ilifikia kipindi maza akamfuta mama yao akamwambia waite watoto wako wote waje uongee nao kama kuna mwenye shida na mwenzake waombane msamaha yaishe ungali hai akadharau now hali ndio imezidi kuwa mbaya coz hata mama yao akiwatafuta kuwajulia tu hali wanamblock yaani hadi sometimes namuoneaga huruma
Ndio hivyo, kwenye familia zetu hizi kuna mambo mengi sana
 
Hii ndio mbaya, yaani,hapa majuzi,Kuna mtu alifariki akaacha eneo,watoto wakagawana sehemu ya Hilo eneo,la pili,wakashindana kwa sababu mmoja alitaka mgawo mkubwa kuliko wengine,(wako watatu) mmoja inasemekana wakaamua kumuua ili wabaki wawili wagawane pasu,wakashindana,mmoja akachukua eneo lote na kumuacha huyu mwingine.yaani Mali ya urithi ni mbaya Sana!
9. MIRATHI
 
Kwann alikaidi mawazo ya maza ako?

Na naamini huyo mama ndo chanzo
 
Hee wamemuua?
 
Inategemea tu na familia au Koo, kwetu tumekuwa na bado tunapendana na kujaliana Kama ndugu na hata kusaidiana. Kwa kweli namshukuru Mungu kwa familia yetu iliyo na upendo na ushirikiano
 
Ila shida nyingine huwa ni roho mbaya za kiasili anazo zaliwa nazo mtu hata umulee vipi yeye Yuko hivo hivo tu it's like generational curses, Kuna baadhi ya Koo au ndugu huwa hawapatani na hawana upendo kabisa kuanzia mababu, so I think inakuwa ka asili flani hivi
 
Yaan ndo kiini cha kila kitu

Unakuta mzazi anampambania mtoto fulani anayempenda ili atoboe, ( mpaka anatumia rasilimali zake kumtoa) watoto wengine anatupa kule

Unahisi kutatokea nini zaidi ya chuki

Maza anataka auze nyumba ya familia ampe mtaji kipenzi chake. Nawaza sisi wengine hatutaki kuendelea au. Wazazi kaeni mkijua upendeleo unavunja undugu
 
1 & 3 ni majibu sahihi sana kupita mengine, hasa 3. Ukute mtu hana kipato na mwingine ana kipato, asiye na kipato akiugua tu anaenda kwa mganga na mganga anamjaza ujinga. Hapo tayari.
 

Mimi kwa nilivyoona kwa familia yetu mara nyingi hii shida iko kwa watoto wa kiume na si wa kike. Hawa watoto wa kiume kabla hawajaoa huwa wanapendana sana ila wakishaoa tu basi balaa ndio linaanza. Yaani unakuta hata mkipanga vikao vya familia wengine hawaji matokeo yake sisi watoto wa kike ndio inabidi tuongoze familia au kuishikilia familia iwe moja ila makaka looh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…