Watoto waliozaliwa tumbo moja kuwa na uadui

Watoto waliozaliwa tumbo moja wakiwa wadogo huwa wana mshikamano na wanakuwa na upendo ila sasa wakikua na kila mmoja akawa na mji wake ndipo changamoto zinapoanzia.

Ule upendo wa utotoni upotea na kuanza kuwa maadui. Hii huwa ni kwanini?

Nimejaribu kupitia vitabu mbalimbali ikiwamo na biblia ili niweze kupata jibu sahihi lakini bado kufanikisha. Tatizo huwa ni nini wakuu?

Kawaida kabisa kwasababu kila mtu anaakili timamu. Ndio maana utaona kurwa ni mlevi ja doto ni mchungaji
 
Watoto waliozaliwa tumbo moja wakiwa wadogo huwa wana mshikamano na wanakuwa na upendo ila sasa wakikua na kila mmoja akawa na mji wake ndipo changamoto zinapoanzia.

Ule upendo wa utotoni upotea na kuanza kuwa maadui. Hii huwa ni kwanini?

Nimejaribu kupitia vitabu mbalimbali ikiwamo na biblia ili niweze kupata jibu sahihi lakini bado kufanikisha. Tatizo huwa ni nini wakuu?
Mkuu matatizo haya yapo sana, sema nachoamini kwenye Self development, hayaepukiki. Kingine tatifuta kitu kiwe kinakupa furaha
 
Vipi kuhusu malezi kwa wazazi,yanaweza kuchangia?
Malezi ya wazazi yanachangia sana,ukiwalea watoto,ukawa baadhi unawapendelea,na kuwaona Bora kuliko wengine,hii inamadhara makubwa,Yule uliyekuwa una muona bwege,au kilaza kuriko wenzie,siku akizipata huko ukubwani,hutaweza kuona msaada wake,mzazi usioneshe upendo zaidi kwa mtoto mmoja zaidi ya mwingine,
Kitu kingine nafikiri human is human,hata Kama mmezaliwa tumbo moja,
Kuna ndugu zangu,nikiwaangalia,isingekuwa kuzaliwa tumbo moja,Wala wasingekuwa watu ninao endana nao,maana tupo tofauti sana,
 
Watoto waliozaliwa tumbo moja wakiwa wadogo huwa wana mshikamano na wanakuwa na upendo ila sasa wakikua na kila mmoja akawa na mji wake ndipo changamoto zinapoanzia.

Ule upendo wa utotoni upotea na kuanza kuwa maadui. Hii huwa ni kwanini?

Nimejaribu kupitia vitabu mbalimbali ikiwamo na biblia ili niweze kupata jibu sahihi lakini bado kufanikisha. Tatizo huwa ni nini wakuu?
Tatizo ni Pesa tu mkuu! Bila hii mambo mbona life lingekuwa yechu tu aisee!!!

Mwenye hela anataka asujudiwe, ukiwaza tumechezea tope wote, tumekula sinia moja, tumeshea nguo zetu pamoja. Leo hii we utaniambia nini eroo?!

Ubaya zaidi ni endapo kidume ana familia yake tayari inamaana utaratibu wa maisha unabadilika automatically. Lazma mke apandikize sheria zake hapo mbaya sasa awe mbinafsi kila ndugu anaekuja kwa mumewe ataona analeta njaa zake anataka kuwamalizia hela zao!😂😂😂😂😆

Huu mpasuko unachangiwa na influence ya wake, malezi mabovi halikadhakika hali ya uchumi endapo ndugu wengine watakuwa tegemezi basi hapo lazima shida iwe kubwa zaidi endapo kaka akishindwa ku neutralize na ndugu zake bila mke kujua. Hapo ndugu walio chini wataunda alliance yao wakitusua inakuwa ni kumkomesha aliyewatangulia tu.
 
Hio ya malezi nakubali kabisa, lazma tuwa mould watoto kuwa independent ila pia kuwa connect katika mazingira ya kimaisha hasa kipindi cha ukuaji.

Kuwaonesha respomsibility zao kwa kila mmoja. Wakubwa wawaangalie wadogo zao tokea utotoni. Hii inasaidia sana kutengeneza bond baina yao.

Japo kila mtoto ana fate yake ila endapo watakuwa katika roho ya kupendana na kutokuwa wabinafsi basi it will be a success. Kuna ambao watazingua ila kuna ambao watawainua wenzao.

Malezi ya wazazi yanachangia sana,ukiwalea watoto,ukawa baadhi unawapendelea,na kuwaona Bora kuliko wengine,hii inamadhara makubwa,Yule uliyekuwa una muona bwege,au kilaza kuriko wenzie,siku akizipata huko ukubwani,hutaweza kuona msaada wake,mzazi usioneshe upendo zaidi kwa mtoto mmoja zaidi ya mwingine,
Kitu kingine nafikiri human is human,hata Kama mmezaliwa tumbo moja,
Kuna ndugu zangu,nikiwaangalia,isingekuwa kuzaliwa tumbo moja,Wala wasingekuwa watu ninao endana nao,maana tupo tofauti sana,
 
Inategemea tu na familia au Koo, kwetu tumekuwa na bado tunapendana na kujaliana Kama ndugu na hata kusaidiana. Kwa kweli namshukuru Mungu kwa familia yetu iliyo na upendo na ushirikiano
Una bahati sana na ningependa nipate mke kwenye familia ya aina hio. People are so selfish these days kiasi kwamba unatakiwa uwe makini na mahali ambapo hata unaenda kuoa.
 
Mimi kwa nilivyoona kwa familia yetu mara nyingi hii shida iko kwa watoto wa kiume na si wa kike. Hawa watoto wa kiume kabla hawajaoa huwa wanapendana sana ila wakishaoa tu basi balaa ndio linaanza. Yaani unakuta hata mkipanga vikao vya familia wengine hawaji matokeo yake sisi watoto wa kike ndio inabidi tuongoze familia au kuishikilia familia iwe moja ila makaka looh!
Tatizo kubwa ni wake, ukishamwambia changamoto za familia anakujaza bichwa. Esp. kama una hela utaskia usiende! Kwani hiko kikao hakitafanyika bila wewe?

Kama hela tutawapa tu...Mbona mdogo wake yeye alikufanyia vile kikao chetu hakuja, nawewe usiende. Hizi ndio akili za wake zetu..Ukiwa bendera unagombana na ndugu yako kabisa bila sababu ya kueleweka.
 
Umeongea ukweli wake wanaweza sambaratisha familia yote. Unakuta watoto wa kaka zenu hata hamuwajui yaani mke anaona sijui hao watoto mtawaloga kwa kweli heri ukosee kujenga nyumba lakini sio kuoa. Mwanaume ndio inabidi awe na msimamo kuhusu familia yake ila ubaya saa nyingine hao wake wanatumia sana ndumba unakuta mwanaume mpk anaita mama ake mzazi mchawi.
 
Hii hali imemkuta dingi yangu mkubwa...Ana mke mbinafsi sana kiasi kwamba ndugu wamemtenga mshua ila mzee ni roho safi sana yani hana noma na mtu.

Ila mke ndio anaweka vigingi yani hadi sio poa. Ubaya sasa kabila langu na ukoo mzima huwa hatupendagi dharau. Maskini jeuri, watu wa kufa na tai shingoni...Hamna mtu atakulilia shida hata kama zinamuua wacha afe tu 😂😂😂😂😂😂
 
Una bahati sana na ningependa nipate mke kwenye familia ya aina hio. People are so selfish these days kiasi kwamba unatakiwa uwe makini na mahali ambapo hata unaenda kuoa.
Mungu atakujalia utapata mke kwenye familia yenye upendo na utu. Sikuhizi watu wengi wabinafsi Sana hata mtu ukiolewa au kuoa ndugu ndo wanaleta maneno yakugombanisha, ili our family hata Jambo likitokea huitana, huelekezeana hata kusaidiana ili Mambo yaende na kila mtu awe na amani, mengine hushirikiana hata kiukoo. Kila mtu Yuko happy na mji wake aisee. Mungu alinde tu ukoo wangu na familia yangu
 
Tatizo kubwa ni wake, ukishamwambia changamoto za familia anakujaza bichwa. Esp. kama una hela utaskia usiende! Kwani hiko kikao hakitafanyika bila wewe?

Kama hela tutawapa tu...Mbona mdogo wake yeye alikufanyia vile kikao chetu hakuja, nawewe usiende. Hizi ndio akili za wake zetu..Ukiwa bendera unagombana na ndugu yako kabisa bila sababu ya kueleweka.
Mume makini na nyie kuoa jamani, mwanamke asiye na upendo na ushirikiano na alikoolewa naye mchawi tu aisee, ushirikiano ni muhimu pia ndugu washirikiane maana hao ndo wakubebana nilikitokea tatizo, Sasa na mwanaume ukikosa SAUTi ndio majanga.
 
Hahahah mke anatakiwa awe na ushirikiano na ndugu wa mume na wa kwake at 50% kila upande. Ila unakuta mke 80% ya upendo ni kwa ndugu zake 20% kwa ndugu za mume wakati yeye ndio kaenda kujiunga undugu na family ya mume.

Ni ujinga ujinga tu na kukosa kujitambua.
 
Back
Top Bottom