Watoto wangu wote hufariki baada ya kuzaliwa au mimba kuharibika

Jitibie bro

Hiyo ya miguu sio poa,nilipatwa na gonjwa aisee lililoambatana na miguu yaani nilirudi utotoni
Ndio nipo najishughulikia mkuu, mwanzo nilikua napuuzia maana sikuwa nikiamini ila sasa nimesurrender baada ya kuona natibu tatizo hili linaibuka jingine, yaani ni bandika bandua[emoji1430]
 
1:mimi kinyama changu hakiumi mkuu kipo kawaida kama kinefifia

2:Mahusiano yangu hayayumbi wala hatugombani kama kuachana tunaachana kwa amani kabisa

3:Biashara zangu zinaenda fresh hazina misukosuko
Basi tuna vyanzo tofauti za tatizo. Lako naona ni la hospitali zaidi, fuata ushauri wa hao walozungumzia Rh factor unaweza pata mwanga.
 
Ndio nipo najishughulikia mkuu, mwanzo nilikua napuuzia maana sikuwa nikiamini ila sasa nimesurrender baada ya kuona natibu tatizo hili linaibuka jingine, yaani ni bandika bandua[emoji1430]
Fanya hivyo aisee,,,Afya ndio mtaji,
 
Acha ujinga wewe, nani ambaye hajawahi kupitia misuko suko?
mbona unatok povu mkuu,,jamaa alihisi labda kuna maagano yalifanyika ndio nikamjibu hilo linawezekana maana huko nyuma nilipitia misukosuko mingi sana hasa upande wa baba kidogo walimwengu waniondoe duniani lakini ndio vile Mungu alinipigania sana pamoja na wazazi kuhangaika zaidi ya miaka m3 ndio nikakaa sawa..Ni stori ndefu ipo siku nitaiweka hapa
 
Basi tuna vyanzo tofauti za tatizo. Lako naona ni la hospitali zaidi, fuata ushauri wa hao walozungumzia Rh factor unaweza pata mwanga.
lakini wote si tuna vinyama!
 
Kabisa, Siku moja nitaleta mrejesho wa kupona tatizo na nikiwa nalea mtoto[emoji4]
Hata mimi mkuu ipo siku nitaleta mrejesho wa huu uzi,,tena ikimpendeza Mungu mwakani[emoji120]
 
Nimesoma maelezo yako lakini naona kama mimba zote zilikuwa na sababu ambazo hazihusiani na wewe kuharibika. Nadhani umepata tu bahati mbaya ya kukutana na wanawake ambao sababu za mimba zao kuharibika ziko wazi.
Wa kwanza umesema alitoa mwenyewe kwa sababu ya mimba kumsumbua. Sioni wewe ulihusika vipi na mimba yake kusumbua.
Wa pili aliharibikiwa mimba kwa sababu umeshasema alikuwa na tatizo hata kabla hamjakutana.
Wa tatu alijifungua mapacha wanne na wote wakafa. Hili nalo halina ajabu yoyote kwani mapacha wanne uwezekano wa kufariki ni mkubwa.
Wa nne naye alijifungua vizuri lakini akamsumbua sana kwa homa na akafariki. Hapa inawezekana alikutana na matatizo mengine tu na sababu siyo wewe.
Wa tano aliharibikiwa mimba ya mapacha. Hapa napo sioni kitu special sana kwani mimba ya mapacha kuharibika siyo ajabu sana.
 
mkuu kukatwa sehemu ya mwili tena kwenye haja sio jambo dogo[emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]usiogope,wenzio wanaenda kuoga makaburini usiku was manane kutafuta Tiba[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…