Ngoja nikwambie ukweli, maana hata mimi nilishawahi kukumbana na kitu kinachofanana na chako. Shida ni wao kukosa uhakika wa kuolewa au kutunzwa na wewe. Mimi ilikuwa hivi
Wa kwanza: Ikiwa imefika miezi mitano, Alikuja kuniambia imeharibika , ila nikaja kigundua alitoa.
Wa pili na watatu: walishika ujauzito kwa pamoja na kwa mpigo, sikutaka wajuane, ila siku mmoja wao akapekua simu akamjua mwenzake, na huyu mwingine nae akapekua simu yamgu akamjua mwenzake, kila mmoja akakaairika wakaamua watoe, mmoja alifanikiwa kwa mateso makali sana, huyu mwingi ilikuwa kidogo afe ila haikutoka, ndio akazaliwa wa kwanza.
Nikaendelea naye huyo aliyezaa, akapata ujauzito tena ndani ya miezi minne tu toka ajifungue,, hakuaniambia, ila akatoa, nikaja kujua tu baadae. Tukaendela akashika ya tatu, akaniambia, akazaa wa pili.
Nikaendelea nae, akashika ya tatu, ilipofika miezi miwili akatoa bila kuniambia, miezi kuenda tumbo halionekani, nikambana ndio akasema ametoa, haya..
Nikaendelea nae, akashika ya nne.., ilipofika miezi 6 ikaharibika, aliumwa sana ila akapona...haya..
Tumeendelea....