Watoto wangu wote hufariki baada ya kuzaliwa au mimba kuharibika

Watoto wangu wote hufariki baada ya kuzaliwa au mimba kuharibika

Kama watoto wanaozaliwa wanakua na homa za mara kwa mara na joto kali,kuna tatizo linataka kufanana na bawasiri ila sio bawasiri na sijui linaitwaje kitaalam ni kinyama sehemu ya haja kubwa mwanaume ukiwa na hilo tatizo ndio hutokea hayo matokea watoto wako kufariki wakiwa wachanga au mimba kuharibika halipo sana sababu nilipata maelezo kwa mzee fulani muda kidogo

Solution nn ukiwa ivo
 
Yawezekana wewe sio mleaji Mungu nae anaepusha viumbe hivyo visije kupata tabu duniani,kingine watoto ni Rizki kama Rizki nyingine kama Muumba kakupangia usiipate basi hata ufanyaje hautapata muhimu shikamana na imani yako Oa muombe Mungu akupe hitajio lako la Watoto acha uzinifu.
 
Ngoja nikwambie ukweli, maana hata mimi nilishawahi kukumbana na kitu kinachofanana na chako. Shida ni wao kukosa uhakika wa kuolewa au kutunzwa na wewe. Mimi ilikuwa hivi

Wa kwanza: Ikiwa imefika miezi mitano, Alikuja kuniambia imeharibika , ila nikaja kigundua alitoa.

Wa pili na watatu: walishika ujauzito kwa pamoja na kwa mpigo, sikutaka wajuane, ila siku mmoja wao akapekua simu akamjua mwenzake, na huyu mwingine nae akapekua simu yamgu akamjua mwenzake, kila mmoja akakaairika wakaamua watoe, mmoja alifanikiwa kwa mateso makali sana, huyu mwingi ilikuwa kidogo afe ila haikutoka, ndio akazaliwa wa kwanza.

Nikaendelea naye huyo aliyezaa, akapata ujauzito tena ndani ya miezi minne tu toka ajifungue,, hakuaniambia, ila akatoa, nikaja kujua tu baadae. Tukaendela akashika ya tatu, akaniambia, akazaa wa pili.

Nikaendelea nae, akashika ya tatu, ilipofika miezi miwili akatoa bila kuniambia, miezi kuenda tumbo halionekani, nikambana ndio akasema ametoa, haya..

Nikaendelea nae, akashika ya nne.., ilipofika miezi 6 ikaharibika, aliumwa sana ila akapona...haya..

Tumeendelea....
😀 😀 😀daah na wew na huyo mwanamke hamjielewii wote... yani mtu ana mtoto wa miezi 4 unamwagia ndani tu na maskini ndo tuna huu upuuzi una vitoto vingi kuvibebanisha tu
 
Naona tuna tatizo linalofanana, tofaut Ni kwamba mm sijawah bahatika kuzaliwa mtoto. Yaani mtoto anafia tumboni,zimeshafika 5 (tuseme 4 maana moja ilitolewa kwa makusudi) mpaka sasa kati ya wasichana watatu nilowahi kua nao toka mwaka 2018. Vingine tunavyofanana ni kwamba mi pia nakaribia 30's na wiki ilopita nimekumbwa na hilo tatizo la kinyama kwenye njia ya haja kubwa, linaambatana na maumivu kila baada ya siku 2. Nimekua nikitumia dawa za asili hasa hasa Aloe vela na inanisaidia kiukweli kutuliza maumivu na kuelekea kwenye kupona.

Nirudi kwenye ishu la ujauzito kuharibika, huyu wa mwisho mimba ya nne kwangu ambayo ya kwanza kwake iliharibika ilipokua na miezi 4. Tukakaa miezi 7 akabeba nyingine ilipofika miezi 8 ikaharibika (ilianza kumsumbua toka ina miezi 2). Tulijitahidi kwenda hospital tatizo halikuonekana kwenda kwa mtaalamu ikaonekana anachezewa. Mtaalamu akaifunga ila bahati mbaya ikaja kuharibika ilipofika miezi 8 (Kosa letu nadhani hatukurudi tena kucheck Kama bado wanamchezea hadi ikaharibika tuliona amepona kabisa tatizo).

Turudi nyuma kidogo, kipindi mtaalamu amemaliza kumtibu bibie wakati ujauzito una miezi 2 nilimuomba anicheck na baada ya kunicheck niligundulika pia nimefungwa na nina jini ambalo ndio linaloniharibia mimba zangu na kuniambia nisipojitibia sitokuja pata mtoto na wala sitofanikiwa kimaisha. Sijafanikiwa kujitibia mpaka sasa ILA NDIO NIPO KWENYE MCHAKATO baada ya kuona hii kitu ipo serious sasa maana nimeanza kuugua magonjwa ya kishenz sana ambayo kwa umri wng ni nadra kuugua mfano miguu kuwa na ganzi mwezi sasa.

OP nina maswali kidogo hili tupate kuoanisha kama ni kweli 100% tuna tatizo moja.

1. Hiko kinyama kinauma wakati wa kujisaidia haja kubwa mpaka kufikia mda mwingine kushindwa kutembea?

2. Mimba zinapoharibika au mtoto kufariki huwa mahusiano yenu yanayumba na kuambatana na mafarakano mpaka kufikia kuachana?

3. Hisia za kimapenzi/kufanya ngono zinakupungua?

4. Mambo yako ya kutafuta hela yanayumba?

Majibu ya maswali hayo yatakupa mwanga tatizo limeelemea upande gani.

NB: TATIZO LANGU NI LA KIIMANI ZAIDI SIO HOSPITAL.
😃😃😃🙌msalimie mtaalam
 
Wakuu poleni na majukumu ya kujenga nchi..

Nimekuja kwenu kama mwana Jamii Forums nikiwa na uzoefu wa takriban miaka 10 na huu mtandao wetu pendwa unatusaidia kwenye mambo mbalimbali kwenye maisha. Nipo mkoani Dodoma kwa sasa ambapo nafanya biashara zangu na kupata riziki.

Nikiwa kama kijana na approach 30's nimekumbwa na matukio mfululizo ya kufiwa ama kuondokewa na watoto wangu punde tu wanapozaliwa wengine kabla ya kuzaliwa au hata muda mrefu baada ya kuzaliwa

Miaka ya hivi karibuni nilipita kwenye mahusiano na wasichana kadhaa, kati ya hao watano niliwapa ujauzito na mchanganuo wake ulikuwa kama ifuatavyo..

Wa kwanza alitoa mimba ikiwa na miezi minne ilimsumbua sana nusu na yeye aondoke na hakunipa taarifa juu ya hilo hadi nilipobaini na nikamuacha papo hapo.

Wapili aliharibikiwa mimba ikiwa na mwezi mmoja(huyu alikuwa na matatizo ya tumbo kabla ya kukutana na mimi alikuwa hashiki ujauzito hivyo alikuwa anajaribu kama amepona bila mimi kujua badala yake mimba ikaharibika).

Watatu alijifungua mapacha wanne kwa vipindi viwili tofauti na wote walifariki ndani ya wiki moja baada ya kujifungua.Yeye ni mwenyeji wa Tanga na ana uzao mzuri wa watoto mapacha.

Wanne alijifungua mtoto wa kiume mwaka mmoja uliopita na amekaa naye huku akimsumbua sana kwa homa za hapa na pale na wiki moja iliyopita nilipewa taarifa kuwa amefariki baada ya kuugua mfululizo.

Watano alishika ujauzito wa mapacha uliodumu kwa miezi sita na mimba ikaharibika pasi na kutegemea. Alichanganyikiwa sana maana alikuwa na matarajio mengi juu ya hao watoto pindi watakapozaliwa..

Kiujumla nimepoteza watoto 9 ndani ya miaka mitatu kwa sababu mbalimbali, hii kitu imekuwa ikinitesa sana na nashindwa kuelewa tatizo hasa ni nini na nini suluhisho lake maana napoteza viumbe wasio na hatia inaniumiza sana[emoji22]

Naombeni ushauri wenu juu ya hili tatizo linalonikumba nifanyeje niweze kuepukana nalo na kama ni mpango wa Mungu kwanini kila siku mimi ukizingatia umri nao unakwenda wazazi wanataka wajukuu.

Naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri juu ya suala hili

Pole kwa unayopitia. Ni vyema kufika hospitali na kufanya ufatiliaji kwa mambo haya:

1: Grupu la magonjwa yanaitwa TORCH.
TORCH ni kifupi cha magonjwa ya: Toxoplasma gondii, Others/wadudu wengine wahusikao( Syphilis, Pavovirus, Listeria na H. Zoster), Rubella, Cytomegalovirus (CMV), na Herpes simplex virus (HSV).

Magonjwa haya huambukizwa kwa mtoto wakati wa ujauzito kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na wakati mwingine baada ya kuzaliwa. Kama una mojawapo ya haya, unaweza kuwa chanzo cha maambukizi kwa wenzio.

Madhira ya magonjwa haya ni:
1: Ujauzito/mtoto kutokukua vizuri
2: Mimba kuharibika
3: Kuzaa watoto waliofariki
4: Kuzaa watoto ambao hufariki baadaye.

2: Rhesus factor/incompatibility
Hii pia inaweza kuhusika, kwani ina madhira kama TORCH. Litabaki hapo kwa sababu hatujui aina ya magrupu ya damu na rhesus factor zao zote. Ni vyema pia ukilifanyia kazi kabla ya maamuzi yako ya mwisho kwenye kupata mwenza wa maisha.

3: Coincidence:
Suala la mapacha, linaweza likawa ni sababu ya uchanga/prematurity na huduma waliyopata baada ya kuzaliwa kulingana na changamoto zinazowakuta.

20220624_083302.png
20220624_083108.png
 
Pole na poleni nyote wenye kadhia kama hii, kwa namna tofauti.

CHUNGUZA ILI KUJUA CHANZO.
Chukua hatua mbili.
1. Kisayansi. Nenda hospitali kamuone daktari.
2. Kiiman.
Uchunguze ukoo wenu kwa kuwaangalia ndugu upande wa baba na upande wa mama, ikibidi washirikishe maana wazazi hua ni ngumu kuwaeleza watoto wao mambo kama haya mpaka yatokee. Chunguza unaweza kuta ni tatizo la ukoo.
Je, umewahi kumkatili binti wa watu kihisia? Chunguza.
Je, umewahi changia binti kutoa mimba yako? Chunguza.
Hutakosa pakutokea. Binafsi hapo kwenye imani wekeza nguvu zaidi.
Kila kheri MUNGU akusaidie.
 
Wakuu poleni na majukumu ya kujenga nchi..

Nimekuja kwenu kama mwana Jamii Forums nikiwa na uzoefu wa takriban miaka 10 na huu mtandao wetu pendwa unatusaidia kwenye mambo mbalimbali kwenye maisha. Nipo mkoani Dodoma kwa sasa ambapo nafanya biashara zangu na kupata riziki.

Nikiwa kama kijana na approach 30's nimekumbwa na matukio mfululizo ya kufiwa ama kuondokewa na watoto wangu punde tu wanapozaliwa wengine kabla ya kuzaliwa au hata muda mrefu baada ya kuzaliwa

Miaka ya hivi karibuni nilipita kwenye mahusiano na wasichana kadhaa, kati ya hao watano niliwapa ujauzito na mchanganuo wake ulikuwa kama ifuatavyo..

Wa kwanza alitoa mimba ikiwa na miezi minne ilimsumbua sana nusu na yeye aondoke na hakunipa taarifa juu ya hilo hadi nilipobaini na nikamuacha papo hapo.

Wapili aliharibikiwa mimba ikiwa na mwezi mmoja(huyu alikuwa na matatizo ya tumbo kabla ya kukutana na mimi alikuwa hashiki ujauzito hivyo alikuwa anajaribu kama amepona bila mimi kujua badala yake mimba ikaharibika).

Watatu alijifungua mapacha wanne kwa vipindi viwili tofauti na wote walifariki ndani ya wiki moja baada ya kujifungua.Yeye ni mwenyeji wa Tanga na ana uzao mzuri wa watoto mapacha.

Wanne alijifungua mtoto wa kiume mwaka mmoja uliopita na amekaa naye huku akimsumbua sana kwa homa za hapa na pale na wiki moja iliyopita nilipewa taarifa kuwa amefariki baada ya kuugua mfululizo.

Watano alishika ujauzito wa mapacha uliodumu kwa miezi sita na mimba ikaharibika pasi na kutegemea. Alichanganyikiwa sana maana alikuwa na matarajio mengi juu ya hao watoto pindi watakapozaliwa..

Kiujumla nimepoteza watoto 9 ndani ya miaka mitatu kwa sababu mbalimbali, hii kitu imekuwa ikinitesa sana na nashindwa kuelewa tatizo hasa ni nini na nini suluhisho lake maana napoteza viumbe wasio na hatia inaniumiza sana[emoji22]

Naombeni ushauri wenu juu ya hili tatizo linalonikumba nifanyeje niweze kuepukana nalo na kama ni mpango wa Mungu kwanini kila siku mimi ukizingatia umri nao unakwenda wazazi wanataka wajukuu.

Naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri juu ya suala hili
Pole sana ndugu mungu atakujalia siku moja …… ushauri wangu nenda kapimwe mimi nazani kuna possibility kubwa huko na ugonjwa unaita sickle cell anemia. Again pole sana
 
[emoji117]Mwaka juzi Kuna binti alikua hampendi, alikuja kumpa mimba bahat mbaya, kamwambia binti aitoe Hana mpango nae. vinginevyo akizaa wasijuane, binti akakataa kata kata.
Mimba imebebwa mpk miez 9, hospitali binti kafariki pamoja na mtoto wkt wa kujifungua.[emoji26]

Hii kitu iskie TU kwa mwenzako,
Dogo Sahv Kila mwanamke akikutana nae anamwagia ndani TU liwalo na liwe kujaribu bahati yake
Huyo Rafki yako Ana Laana!! Amempa mimba Mschana asiempenda akamforce atoe mimba ila Dada WA watu alikataa akaishia kufariki siku ya Kujifungua! Hajajifunza wala Hajakoma eti sshv anaendelea Kumwagia Ndani kila anaekutana nae eti liwalo na Liwe, huyo atakuja kuishia kupata UKIMWI. Mwambie akaombe Msamaha kwenye Kaburi LA huyo Binti na Kichanga chake😏
 
mkuu hii kitu inaumiza sana ni vile inawakuta watu wchache hawawezi kuelewa,ila namini yote ni mipango ya Mungu wakati sahihi ukifika nitapata watoto wengi zaidi hata ya niliowapoteza
Imani ndio Cha muhimu, jipe Moyo mkuu
 
Katika maelezo yako yote hamna sehemu uliyosema umeoa, Mimi naona utafute mwenza sahihi uoe Kwa pamoja mtashinda Hilo unalopitia.
Si ajabu Kuna agano lilifanywa na mababu zako kuwa usizae Nje ya ndoa.
Mambo ni mengi other things are more spiritual than we can imagine.
 
Kwani lazima mzae,ulimwengu ushakuwa mgumu huu.
 
Ingia kwenye Maombi kaka lia na Mungu sana . Piga Dua kwa Imani kubwa kaka . Pole sana kaka Naomba Mungu akusaidie hio hali iishe na amini inawezekana kupata watoto kaka kwa Mungu hakuna lisilowezekana kaka
 
Huyo Rafki yako Ana Laana!! Amempa mimba Mschana asiempenda akamforce atoe mimba ila Dada WA watu alikataa akaishia kufariki siku ya Kujifungua! Hajajifunza wala Hajakoma eti sshv anaendelea Kumwagia Ndani kila anaekutana nae eti liwalo na Liwe, huyo atakuja kuishia kupata UKIMWI. Mwambie akaombe Msamaha kwenye Kaburi LA huyo Binti na Kichanga chake[emoji57]
Sahii kabisa,
Kuna Vitu haviko sawa kwenye past yake
 
Wakuu poleni na majukumu ya kujenga nchi..

Nimekuja kwenu kama mwana Jamii Forums nikiwa na uzoefu wa takriban miaka 10 na huu mtandao wetu pendwa unatusaidia kwenye mambo mbalimbali kwenye maisha. Nipo mkoani Dodoma kwa sasa ambapo nafanya biashara zangu na kupata riziki.

Nikiwa kama kijana na approach 30's nimekumbwa na matukio mfululizo ya kufiwa ama kuondokewa na watoto wangu punde tu wanapozaliwa wengine kabla ya kuzaliwa au hata muda mrefu baada ya kuzaliwa

Miaka ya hivi karibuni nilipita kwenye mahusiano na wasichana kadhaa, kati ya hao watano niliwapa ujauzito na mchanganuo wake ulikuwa kama ifuatavyo..

Wa kwanza alitoa mimba ikiwa na miezi minne ilimsumbua sana nusu na yeye aondoke na hakunipa taarifa juu ya hilo hadi nilipobaini na nikamuacha papo hapo.

Wapili aliharibikiwa mimba ikiwa na mwezi mmoja(huyu alikuwa na matatizo ya tumbo kabla ya kukutana na mimi alikuwa hashiki ujauzito hivyo alikuwa anajaribu kama amepona bila mimi kujua badala yake mimba ikaharibika).

Watatu alijifungua mapacha wanne kwa vipindi viwili tofauti na wote walifariki ndani ya wiki moja baada ya kujifungua.Yeye ni mwenyeji wa Tanga na ana uzao mzuri wa watoto mapacha.

Wanne alijifungua mtoto wa kiume mwaka mmoja uliopita na amekaa naye huku akimsumbua sana kwa homa za hapa na pale na wiki moja iliyopita nilipewa taarifa kuwa amefariki baada ya kuugua mfululizo.

Watano alishika ujauzito wa mapacha uliodumu kwa miezi sita na mimba ikaharibika pasi na kutegemea. Alichanganyikiwa sana maana alikuwa na matarajio mengi juu ya hao watoto pindi watakapozaliwa..

Kiujumla nimepoteza watoto 9 ndani ya miaka mitatu kwa sababu mbalimbali, hii kitu imekuwa ikinitesa sana na nashindwa kuelewa tatizo hasa ni nini na nini suluhisho lake maana napoteza viumbe wasio na hatia inaniumiza sana[emoji22]

Naombeni ushauri wenu juu ya hili tatizo linalonikumba nifanyeje niweze kuepukana nalo na kama ni mpango wa Mungu kwanini kila siku mimi ukizingatia umri nao unakwenda wazazi wanataka wajukuu.

Naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri juu ya suala hili
Acha zina wewe,owa kwanza then uje huku tukushauri vitu vya kukusaidia...
 
Andaa sadaka nzuri na ukamtolee Mungu anayetupa uhai.
Pia ni vizuri upate mke na ufunge ndoa kwa mujibu wa imani yenu.
Sio kunyandua kila aliye mbele yako.
Sadaka inavunja agano na laana.
Pole sana aisee.
 
dah[emoji22],,huwezi amini mkuu nina hicho kinyama sehemu ya haja kubwa na kimenitokea miezi kadhaa iliyopita
Pole kama kuna wazee kwenu waeleze hili watakusaidia kuna dawa zake inategemea na koo na kabila hivyo waone wazee wako washirikishe hili tatizo sio maarufu sana ila lina athari kubwa na bbn linatibika kumbuka sio bawasiri ni tatizo tofauti ila hufanana na bawasiri
 
Back
Top Bottom