Watoto wengi hasa waliokulia mjini hawatakua na kumbukumbu nzuri ya utotoni.

Watoto wengi hasa waliokulia mjini hawatakua na kumbukumbu nzuri ya utotoni.

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
1,572
Reaction score
3,863
Kwa tuliobahatika huwa kuna muda unakaa, unakumbuka nyumba yenu/ kijiji chenu utotoni wakati unakua, watoto wenzio uliokua ukicheza nao na maisha ya ujumla ya utotoni.

Kwa bahati mbaya kwa sasa watoto wengi wanalelewa kwenye nyumba lakini hawana nyumbani. Wazazi wanahama nyumba za kupanga mara kwa mara, shule na hata mikoa kabisa.

Hadi mtoto anamiza la saba, wameshahama nyumba za kupanga mara kadhaa, hata kua na marafiki wa utotoni inakua ngumu, memory yenyewe inavurugika.

Kingine ni utandawazi, watoto hawana michezo ya nyumbani, wanaangalia michezo ya kwenye simu au tv ambayo ni ngumu kuikumbuka hata.

Hasara nyingine ni sanaa zisizodumu, wale wenye umri mkubwa kidogo au zaidi, kuna nyimbo ukizisikia, unakumbuka mbali sana, zinaguza ile inner retrieval que, lakini sasa hata sanaa has nyimbo hazidumu, week moja kisha imepotea

I feel sorry for them. Kids now do not understand that the full moon in village was a special time for night play.

Mabadiliko hayazuiliki ila yanaondoka na vingi

1752622983302.jpeg
 
things will never be the same. Kilicho kupa maana na ukakiona cha thamani jana, leo kitakua cha kawaida. Pia tambua kilikua na thamani kwako wewe, sio kwangu, sio kwetu na wala sio kwao, ilikua ni kwako.

unaweza ukakuta wewe ndo unatakiwa kuonewa huruma, maana kipindi unavokua ulikua unacheza kwenye mavumbi chini ya mwanga wajua, sahizi watoto wa mjini wanajifunza mambo ya kiteknolojia..

Mtu mmoja mwenye busara alisema "Pamenifaa Pasikutambize Maprodian".

.illumination
 
yeah kuna nyimbo nikisikilizaga huwa nakumbuka maisha ya zamani

Killing Me Softly With His Song by fugees hii nyimbo unikunbusha mdada fulani marehemu hivi sasa 1997 yupo makongo form 4
alikuwa kwenye COUNTERBOOK yake kaiandika yote mpk mwisho na anaaiimba yote mpk mwisho ikipigwa radion anaifatilia
hiyo nyimbo ataniisikie usiku wa manane nimelala basi unirudisha miaka 30 nyuma na kumkumbuka huyu dada ambaye tulikuw tunaishi mtaa mmoja kinondoni miaka 90s
zipo nyingi sana lkn hii ni moja wapo
alikuwa na nyimbo nyingi sana hila hii ilikuwa ndio nyimbo anaipenda sana
 
Hilo nakuunga mkono hasa kwa familia za mjini tena wale wanaoishi maeneo ya watu wenye vipato vya kati na juu mtaa umejaa nyumba za mageti.

kuna route 2 , Shule > Nyumbani na Nyumbani > Shule, tena ni kwa school bus.

Kuamka saa 11 kwenda shule kurudi kufika nyumbani saa 11 jioni,

Wakifika nyumbani ni cartoon, games, simu, homework. hakuna kutoka nje !

Hata wakivizia vizia kutoka nje hakuna watoto wengi wa kucheza nao sababu wengi wanakatazwa kutoka ama familia zina uwezo wa kifedha kuwasomesha boarding.

Nashukuru nilikulia mjini, nilisoma shule za mabasi ya njano lakini enzi hizo tulikuwa free sana, shule runawahi kutoka, mageti yapo ila hakuna kubaniwa kutoka, sehemu kibao kulikuwa na maeneo ya wazi tunakutana kucheza michezo iliyotuunganisha wengi wa matabaka tofauti na kutuachia kumbukumbu mpaka leo.

Michezo nayoikumbuka kombolela, kuangushana mitama, tule tumbakizie baba, magoli madogo, kuogelea mtoni, kuwinda ndege, n.k.

Kila mtu tulikuwa tunapajua kwao kwa kutembeleana, hakuna wa kujifungia ndani ya mageti

ule muunganiko wa kupiga story mida ya jioni hata kama kwenu mna tv unaiacha.
 
Duh Nini chanzo Cha kifo chake?
yeah kuna nyimbo nikisikilizaga huwa nakumbuka maisha ya zamani

Killing Me Softly With His Song by fugees hii nyimbo unikunbusha mdada fulani marehemu hivi sasa 1997 yupo makongo form 4
alikuwa kwenye COUNTERBOOK yake kaiandika yote mpk mwisho na anaaiimba yote mpk mwisho ikipigwa radion anaifatilia
hiyo nyimbo ataniisikie usiku wa manane nimelala basi unirudisha miaka 30 nyuma na kumkumbuka huyu dada ambaye tulikuw tunaishi mtaa mmoja kinondoni miaka 90s
zipo nyingi sana lkn hii ni moja wapo
alikuwa na nyimbo nyingi sana hila hii ilikuwa ndio nyimbo anaipenda sana
 
Umenikumbusha mbali sana mzee.
Mwaka 2006 kipindi nipo sekondari kuna nyimbo ile ya matonya ya vaileti ndio ilikuwa imebamba sana.

Kuna demu mmoja anaitwa sofia tulikuwa darasa moja aise alikuwa anauimba huo wimbo wote basi tulikuwa tukikaa nae ananiimbia wimbo wote.

Hadi nikiwa geto wimbo huo ukipigwa redioni nashtukia nauita sofia badala ya vaileti.
Huyu demu nilimpenda sana nayeye alinipenda sema sikuwahi kumtongoza alikuwa kama rafiki yangu.

Popote ulipo nimekukumbuka sofia sijui ukowapi ila najua upo mkoani kwetu Tabora.
Hadi leo wimbo huo ukipigwa namkumbuka sana sofia
 
Tumsapoti kijana bwashee, leo kakaza sio kitoto.
Mimi navyojua Mara ya kwanza kuona na kusikia habari za kishoga ni siku nimeenda kijijini .

Watu wengi ambao wamepinda background zao ni uswahilini na kijijini Changanyikeni na vijijini hayo maeneo usithubutu kulelea mtoto huko utajuta Sana .
 
Kwa tuliobahatika huwa kuna muda unakaa, unakumbuka nyumba yenu/ kijiji chenu utotoni wakati unakua, watoto wenzio uliokua ukicheza nao na maisha ya ujumla ya utotoni.

Kwa bahati mbaya kwa sasa watoto wengi wanalelewa kwenye nyumba lakini hawana nyumbani. Wazazi wanahama nyumba za kupanga mara kwa mara, shule na hata mikoa kabisa.

Hadi mtoto anamiza la saba, wameshahama nyumba za kupanga mara kadhaa, hata kua na marafiki wa utotoni inakua ngumu, memory yenyewe inavurugika.

Kingine ni utandawazi, watoto hawana michezo ya nyumbani, wanaangalia michezo ya kwenye simu au tv ambayo ni ngumu kuikumbuka hata.

Hasara nyingine ni sanaa zisizodumu, wale wenye umri mkubwa kidogo au zaidi, kuna nyimbo ukizisikia, unakumbuka mbali sana, zinaguza ile inner retrieval que, lakini sasa hata sanaa has nyimbo hazidumu, week moja kisha imepotea

I feel sorry for them. Kids now do not understand that the full moon in village was a special time for night play.

Mabadiliko hayazuiliki ila yanaondoka na vingi

View attachment 3407476
Nyakati zinabadilika lazima ukubali. Kila kizazi na wakati wake
 
Greatest love of all,, niliimba huu wimbo kwenye concert moja hivi .
Nawamiss rafiki zangu wa utotoni na kundi letu la five dadaz mwenge maghorofani!!!!!
Upendo, Binti, Jackline (rip) Oliver na Mimi. na miss zile moment.
Nakumbuka harusi moja ya kishua maharusi walipanda farasi..... Basi tulizikimbilia zile farasi ilimradi tuwashike tu.
 
things will never be the same. Kilicho kupa maana na ukakiona cha thamani jana, leo kitakua cha kawaida. Pia tambua kilikua na thamani kwako wewe, sio kwangu, sio kwetu na wala sio kwao, ilikua ni kwako.

unaweza ukakuta wewe ndo unatakiwa kuonewa huruma, maana kipindi unavokua ulikua unacheza kwenye mavumbi chini ya mwanga wajua, sahizi watoto wa mjini wanajifunza mambo ya kiteknolojia..

Mtu mmoja mwenye busara alisema "Pamenifaa Pasikutambize Maprodian".

.illumination
Maybe you are right based on your own perspective
 
yeah kuna nyimbo nikisikilizaga huwa nakumbuka maisha ya zamani

Killing Me Softly With His Song by fugees hii nyimbo unikunbusha mdada fulani marehemu hivi sasa 1997 yupo makongo form 4
alikuwa kwenye COUNTERBOOK yake kaiandika yote mpk mwisho na anaaiimba yote mpk mwisho ikipigwa radion anaifatilia
hiyo nyimbo ataniisikie usiku wa manane nimelala basi unirudisha miaka 30 nyuma na kumkumbuka huyu dada ambaye tulikuw tunaishi mtaa mmoja kinondoni miaka 90s
zipo nyingi sana lkn hii ni moja wapo
alikuwa na nyimbo nyingi sana hila hii ilikuwa ndio nyimbo anaipenda sana
rip kwa dada
 
Mimi navyojua Mara ya kwanza kuona na kusikia habari za kishoga ni siku nimeenda kijijini .

Watu wengi ambao wamepinda background zao ni uswahilini na kijijini Changanyikeni na vijijini hayo maeneo usithubutu kulelea mtoto huko utajuta Sana .
Mambo ya kishoga nimeyasikia mjini hasa nilivyo fika Arusha na dasalama,,

Vijijijni duuh 🤔 maybe tunatofautiana maeneo
 
Duh Nini chanzo Cha kifo chake?
huyu dada walikuwa ni wale watu wa mwanzo kabisa kusoma zile kozi za hotel management miaka ile 90 mwishoni alupomaliza tu form 4 akaenda kusomea hizo

miaka 2000 mwanzoni wakawa wamehama kinondoni MZEE WAO akawa amejenga KIMARA

kutokana na kuwa uwezo mkubwa kuzungumza kiingeleza na french
miaka yake yote alikuwa akifanya kazi kwenye hoteli hizi za kubwa za kitalii haswa NZANZIBAR na ARUSHA
hadi kufikia miaka ya 2010 nikawa nashangaa mbna mpk muda huu sijasikia kuwa ana mtoto wakati wadogo zake wawili walikuwa na watoto na waliolewa
ndio baadae sana MAMA katika maongezi akaniambia kuwa FULANI amekutwa na kansa amefanyiwa OPERESHENI na ametolewa kizazi
kbla ya hapo aliangaika sana kwa waganga kutafuta tiba ya kupata mtoto mana mdada alikuwa ni mweupe wa asili na shape la haja si unajua WACHAGA ukiikuta pisi kali basi inakuwa PISI kweli kweli nadhani ndio 7bu pia ilimfanya akasita hata kuolewa
ndipo mwaka 2021 katikati napigiwa SIMU fulani kalazwa KCMC MOSHI ana hali mbaya shida kansa ilisambaa mpk kwenye ORGANI zingine tumboni
toobad hadi kufikia mwezi wa 12 siku 5 kbla mwaka mpya akafariki
tukaenda kumzika moshi
R I P dada

nina picha tumepiga picha mimi na yeye STUDIO pale kinondoni kwenye hichohicho kituo kinachoitwa STUDIO basi kwenye hiyo STUDIO ndani
na nyingine tulipiga mwaka 1993 tukiwa baradhani mwa nyumba tunayoishi mm nikiwa bado mdogo mno siku ya sikukuu ya EID

tulikuwa tunaiva sanana huyu dada kutokana na mimi nilikuwa napenda hizo nyimbo akiwa anaimba mimi huwa. namsikiliza
b mkubwa alikuwa ananiambia wakati nipo mchanga huyo dada ilikuwa akitoka shure tu huwa alikuwa anashinda chumbani kwa mama akichezana mimi mpk jioni
tulikuwa kama tunabondi ndio hata kwenye kifo chake nilisafiri mpk moshi kwenda kumzika
 
Back
Top Bottom