Watu 11 wamepoteza maisha ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar, Morogoro

Watu 11 wamepoteza maisha ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar, Morogoro

OSHA walipita karibuni kukagua mazingira ya kazi? Hizi ajali huenda zikaleta majibu ambayo wengi hatukuraji
 
Aisee, tunasema Safety first.

OSHA na NEMC pelekeni vijana wenu wakajifunze working standards and safety on mining, construction and industrial katika nchi hizi Australia, Canada, USA nk. Kuna gap kubwa sana la utalaam katika usimamizi wa hivi vitu kwa watu.

Tuache kuentertain Indians, Arabs and Chinese in business hasa kwenye hayo maeneo niliyoyataja hapo juu, hawa watu sio safety conscious na matokeo yake wanaua sana watu wetu kwenye tragedy kama hiyo na wengi pia hufa kwenye occupational diseases na hakuna compensation yeyote.

Maeneo haya watu wetu wengi hufa masikini sana pia maana hata mishahara ni midogo sana.
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mtu wangu wa karibu anadai Watu 11 wamefariki Dunia ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar kilichopo Morogoro kutokana na hitilafu za kiufundi.

Wenye taarifa kamili tujuzeni

==== ===


Watu 11 wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefariki dunia na wawili wamejeruhiwa kwa ajali iliyotokea katika kiwanda cha uzalishaji wa sukari cha Mtibwa baada ya kutokea kwa hitilafu ya mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo Mei 23,2024.

Kamanda Mkama amesema raia wa kigeni waliofariki ni kutoka nchini Kenya, India na Brazili

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mtibwa Sugar na majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala.

Waliokufa ni wataalamu wa umeme na mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo.

Chanzo: AZAM TV
Watanzania hawana ajira, huko mtibwa Kuna raia wa Brazil, Kenya na India wameajiriwa.
Kama sio huo mlipuko kutokea tusingekaa tujue ya huko mtibwa.
 
Poleni kwa waifwa wote Hiyo fine mtibwa atakayopigwa anaweza akafilisika kabisaa yaani hela atatoa nyingi saana
 
Daaaah,ni tukio la ukweli kabisa nimempigia mtu anayefanya kazi pale,amesema ni msiba mzito wamefariki watu 11.

Poleni sana wahanga na ndugu zao
 
WATU 11 wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Misheni ya Bwagala kwa matibabu baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika kiwanda cha Sukari cha Mtibwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Hitilafu hiyo ya Umeme imedaiwa kutokea kwenye mtambo wa kupitisha mvuke wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama akiwa eneo la tukio amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba na nusu, Mei 23 mwaka huu, yaani usiku wa kuamkia leo.
 
OSHA walipita karibuni kukagua mazingira ya kazi? Hizi ajali huenda zikaleta majibu ambayo wengi hatukuraji
OSHA ni Kenge kama Kenge wengine tu , hali za safety , environment and health kwenye viwanda vya Bongo ni ya ovyo ovyo
 
Poleni kwa waifwa wote Hiyo fine mtibwa atakayopigwa anaweza akafilisika kabisaa yaani hela atatoa nyingi saana
Aagh wapi ?
Hao Maafisa wa OSHA ndio wanaoongoza kwa rushwa ,huo ukaguzi sijui huwa wanafanya ukaguzi gani .
Upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom