RoadLofa
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 1,509
- 3,313
Aisee kuna mafuriko ya hatari yanaendelea muda huu Morogoro mjini tangu saa 10 usiku hadi sa hivi bado yanaendelea.
Mimi nipo Kihonda huku watu kibao hawajalala wanapambana kutoa maji yalioingia ndani na kuokoa vitu vyao.
Mvua likikata tutegemee habari za vifo na watu kubomokewa nyumba tu, mvua inapiga kwa sifa kama haitopiga tena. Aisee ni balaa!
PICHA/VIDEO
----- --- -------
Mvua yasababisha mafuriko, foleni Morogoro
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro kuanzia saa 9 alfajiri, zimesababisha madhara mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na mafuriko na foleni ya magari Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amewasili mapema asubuhi leo Ijumaa Januari 13, 2023 eneo la Kihonda mahali ambako wananchi wameathirika zaidi huku akisaidia kuokoa watu na mali zao.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapo kwenye maeneo mbalimbali Manispaa ya Morogoro wakiendelea kuokoa watu na mali zao.