Watu 8,476 kusaka nafasi 42 za ajira zilizotangazwa na Bunge

Tume ya utumishi ya bunge ilitangaza nafasi za kazi kwada mbalimbali ambapo watu 8000 ndio walioitwa kwenye usaili katika nafasi 42 za kazi zilizotangazwa.

kada zinazoongoza kwa waombaji ni uchumi, dereva, sheria na uhasibu huku kada zenye waombaji wachache zikiwa ni afya na maktaba.

source:mwananchi
Watu 8000 ndo waliochaguliwa kufanya intaviw? Walioomba je?
 
Hi habari iko kwenye gazati la nipashe, kama ni kweli hiyo hali anatupa taswira gani katika soko la ajira, hi ni timing bomb kuna haja ya vyuo kubadili mitaala ya hizi zisiokuwa na soko kwenye Market yetu.

======
Tume ya Utumishi ya Bunge imetangaza ajira za kada mbalimbali ambapo walioitwa kwenye usaili wako zaidi ya 8,000 kati ya nafasi za kazi 42 zilizotangazwa, huku kada zinazoongoza kwa idadi kubwa ni uchumi, udereva, sheria na uhasibu.

Kwa mujibu wa tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotolewa Mei 19, mwaka huu na Katibu wa Bunge jijini Dodoma, liliorodhesha jumla ya majina 8,476 ya waliovuka hatua va kwanza ya mchujo na kuitwa kwenye usaili kwa kada 21 za ajira kwenye Bunge la Muungano wa Tanzania.

April 21, mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitangaza nafasi za kazi 42 katika kada 21 mbalimbali ili kuim arisha utendaji wake.

Juzi, Bunge lilitoa tangazo lililosomeka: "Katibu wa Bunge, kwa niaba ya Sekretarieti ya Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Mei 27, 2023 hadi Juni 03, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo."

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kada zinazoongoza kwa waombaji wengi ni uchumi, sheria, udereva na uhasibu, huku kada zenye waombaji walio chini ya 100 ni afya na maktaba.

Tangazo hilo liliainisha kada hizo na idadi ya walioteuliwa kwenye usaili ikiwa kwenye mabano, ofisa hesabu daraja la II (538), msaidizi wa kumbukumbu daraja la II (279), udereva daraja la I (984), mhandi-si umeme daraja la II (234), ofisa usimamizi wa fedha daraja la II (492), mwandishi wa taarifa rasmi za Bunge darala la II (413), mchumi daraja la II (904), ofisa sheria dara-ja la I (302).

Nyingine ni ofisa Tehama daraja la II (310), msaidizi wa maktaba daraja la II (98), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II Sheria (831), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II uchumi (1,208), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II (afya ya jamii/menejimenti ya huduma za afya) 47

Pia soma: Bunge limetangaza nafasi 42 za kazi kwa Watanzania wasiozidi miaka 45
Hiyo ratio sio poa
 
Hii habari iko kwenye gazati la Nipashe, kama ni kweli hiyo hali anatupa taswira gani katika soko la ajira? Hi ni timing bomb, kuna haja ya vyuo kubadili mitaala ya kozi zisizokuwa na soko kwenye market yetu.

======
Tume ya Utumishi ya Bunge imetangaza ajira za kada mbalimbali ambapo walioitwa kwenye usaili wako zaidi ya 8,000 kati ya nafasi za kazi 42 zilizotangazwa, huku kada zinazoongoza kwa idadi kubwa ni uchumi, udereva, sheria na uhasibu.

Kwa mujibu wa tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotolewa Mei 19, mwaka huu na Katibu wa Bunge jijini Dodoma, liliorodhesha jumla ya majina 8,476 ya waliovuka hatua va kwanza ya mchujo na kuitwa kwenye usaili kwa kada 21 za ajira kwenye Bunge la Muungano wa Tanzania.

April 21, mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitangaza nafasi za kazi 42 katika kada 21 mbalimbali ili kuim arisha utendaji wake.

Juzi, Bunge lilitoa tangazo lililosomeka: "Katibu wa Bunge, kwa niaba ya Sekretarieti ya Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Mei 27, 2023 hadi Juni 03, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo."

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kada zinazoongoza kwa waombaji wengi ni uchumi, sheria, udereva na uhasibu, huku kada zenye waombaji walio chini ya 100 ni afya na maktaba.

Tangazo hilo liliainisha kada hizo na idadi ya walioteuliwa kwenye usaili ikiwa kwenye mabano, ofisa hesabu daraja la II (538), msaidizi wa kumbukumbu daraja la II (279), udereva daraja la I (984), mhandi-si umeme daraja la II (234), ofisa usimamizi wa fedha daraja la II (492), mwandishi wa taarifa rasmi za Bunge darala la II (413), mchumi daraja la II (904), ofisa sheria dara-ja la I (302).

Nyingine ni ofisa Tehama daraja la II (310), msaidizi wa maktaba daraja la II (98), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II Sheria (831), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II uchumi (1,208), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II (afya ya jamii/menejimenti ya huduma za afya) 47

Pia soma: Bunge limetangaza nafasi 42 za kazi kwa Watanzania wasiozidi miaka 45
Inasikitisha, hakuna hata mmoja ya hao atakayepata hizo nafasi, kwa Bunge lililojaa wezi, hata hizo nafasi zimeshaibwa!
 
Asichome vipi nauli?

wakamfanyie interview anapoishi au[emoji23][emoji23]

Mkuu kati ya watu 984 wa kada aliyoomba then wanahitajika watu 6….Kweli ya Mungu mengi ila muda mwingine usitumie hisia tumia akili zaidi.
 
Hahahahaha 🤣😂🤣😂😄😃😃 my foot. . . . Eti usitumie hisia

Haya sio ya kucheka ila for sure hali ni mbaya jamani
 
Ila Magu kwanini alikua haajiri watu Jamani?!dahh
Hata kama angeajiri asingewamaliza! Sema tu serikali ya akina Mwigulu imekuwa ya hovyo hovyo, haitaki kuinua sekta binafsi ili zote ajira nyingi! Kutengema serikali kwamba iajiri wote haitakaa itokee! Serikali za wenzetu zenye akili zinaboresha sekta binafsi ili zipunguziwe mzigo!
 
Back
Top Bottom