Watu aliowasema Rais Samia kuhujumu Bwawa la Nyerere ni kina nani?

Watu aliowasema Rais Samia kuhujumu Bwawa la Nyerere ni kina nani?

Kulikuwa na umuhimu gani kuandika ..."awataja waliohujumu mradi"...halafu hakuna aliowataja?

Rais Samia anawajuwa Wahujumu wa mradi lakini hawezi kuwataja kwani hao wahujumu wa mradi wapo ndani ya Serikali yake na yeye mwenywe amewapa vyeo vya Uwaziri. Na hao hao Wahujumu wa Mradi wameleta Majenereta ya umeme wanayauza ili wapate pesa .
 
Serikali inajihujumu😂
Kabisa chief, nakumbuka waziri wa sasa wa stima alivyokuwa kikwazo eti leo naye ana audacity ya kuwa upande wa wakemeaji… kweli saa mbovu ni mbovu tu hata kma inakuwa right four times in a day…vipi kwa hayo masaa 20?
 
Kabisa chief, nakumbuka waziri wa sasa wa stima alivyokuwa kikwazo eti leo naye ana audacity ya kuwa upande wa wakemeaji… kweli saa mbovu ni mbovu tu hata kma inakuwa right four times in in a day…vipi kwa hayo masaa 20?
Spin doctors..ndio maana wanasema usikimbize mwizi peke yako,anaweza akageuka akakuitia mwizi ww. Hawa jamaa wako peke yao bungeni na Serikalini alafu wanasema wamehujumiwa,,ni mambo ya ajabu..
 
Rais Samia anawajuwa Wahujumu wa mradi lakini hawezi kuwataja kwani hao wahujumu wa mradi wapo ndani ya Serikali yake na yeye mwenywe amewapa vyeo vya Uwaziri. Na hao hao Wahujumu wa Mradi wameleta Majenereta ya umeme wanayauza ili wapate pesa .
Kwa hiyo kulikuwa na umuhimu gani kuanzisha thread!?
 
Wanapenda tubaki kunyoosha mabakuli, Wasiopenda kuona Nchi za Kiafrika zinapiga hatua za kujikimu, kwa Ufupi ni Mabepari na wote wanaonunulika kuendeleza Hujuma Afrika kwa Visingizio lukuki.

Aluta Continua.
 
Kulikuwa na umuhimu gani kuandika ..."awataja waliohujumu mradi"...halafu hakuna aliowataja?
Hata hujuma zenyewe zilizofanywa hazijulikani!

Kuna watu hupenda sana kuuza maneno wakidhani wanaowauzia maneno hayo hawana akili timamu za kufikiri.

Hapa alikuwa akizungusha maneno tu kujazia muda wa hotuba ambayo haikuwa na maana yoyote.
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema katika awamu ya 5 chini ya Hayati Dk John Pombe Magufuli waliamua liwalo na liwe ila Bwawa la Nyerere lijengwe licha ya hujuma kubwa zilizofanyika na baadhi ya watu ili mradi huo usitekelezwe.

“Awamu ya tano tukasema liwalo na liwe lakini azma hii ya Mwalimu lazima tuitekeleze hatuwezi kuzungumzia mafanikio haya bila kutaja fikra za Mwalimu na aliyeanzisha utekelezaji wa mradi huu”

“Nakumbuka mikiki mikiki iliyokuwepo wakati ule, nakumbuka sabotage zilizofanywa wakati ule lakini kwa umahiri na ukakamavu Marehemu” Rais Samia Suluhu Hassan 22 Disemba 2022# Uzinduzi Ujazaji maji Bwawa la Nyerere

Kwa kuwa nchi yetu ni ya uwazi na ukweli ni muhimu tukawajua kwa majina watu waliokuwa wanakwambisha Mradi wa JNHPP usitekelezwe ambao Rais Samia amewasema
View attachment 2463531
Katizame clip za nyumba za Nape na Mwenzake Mathread wakilalamika Bwawa lisijengwe litaharibu mazingira, uzuri clip zipo.
 
WA KWANZA ALIKUWA NAPE NAUYE, MAKAMBA,WATUY WA KUZAISHA UMEME KWA GAS
Okay, walikuwa wanahujumu vipi ?

Kitu kilikuwa kipo kwenye planning, na mwenye plan ndio kashikilia hela, na ndio yeye mwenye maamuzi ya kujenga au la....

hujuma hapo inafanywa fanywaje na muuza umeme wa gas?
 
Umeuliza maswali ya msingi kabisa.

Je, maana ya "Hujuma" ni nini?

Kusema tu kwamba mradi utaathiri mazingira ni hujuma?

Na kama lengo la mtoa hotuba ni hao waliotajwa, Nape na January, kwamba ni wahujumu; hizo hujuma zilizofanywa dhidi ya mradi ni zipi?

Samia sasa anajulikana huwa anajisemea maneno tu bila ya kuwa na lengo lolote juu ya anachokiwasilisha kwa wanaomsikiliza.
 
halafu akasema "sisi tukaona litakalokuwa na liwe."

badala ya kusema sisi tulikuwa na upembuzi yakinifu wetu tukaona hoja za wakosoaji, wataalam wenzetu, tuna majawabu nazo; anasema tukaona litakalokuwa na liwe!

kama mradi ni hasara na liwe ?? kama maji hayatajaa kwa ukame na liwe ?? wanyama na mimea ikifa na liwe ??

Very unpresidential, unprofessional, mindless and inarticulate response to concerns of critics. Anahitaji mtu mweledi zaidi wa kumwandikia hotuba.
 
Back
Top Bottom