Walivamia kata yetu kwa fujo, kumbe walimpa diwani 13M, Ili aruhusu wawe wanaingia kwenye maeneo holela.
Bas wakawa wanaingiza kwenye mashamba ya watu wanakula mazao hovyoo, afu ukiwa elekeza wanapaniki na kutumia silaha za mkuki na mishale na sime.
Siku hiyo waliingia kwenye shamba la mzee fulani wa kijijini kwetu, na hilo shamba liko njiani kuelekea shambani kwetu sie.
Jamaniii sio kwa ming'ombe ile, sijawahi ona msururu km ule live, tangu nizaliwe zaidi ya picha au mtandaoni au kwa TV.
ile ming'ombe 200 ilipita, heka 6 za mahindi, dkk chache pako empty yaan buli buli.
Bahati nzuri kuna mtu akawa anapita hapo akakuta huo msururu wee asirudi alikotoka kutoa taarifa, dkk chache, watu wakaja pale, likaanza zogo wale wafugaji wasianze kutoa mikuki na mishale, watu tukakimbiana hapo, kumbe kuna baadhi walijeruhiwa, na m1 alikufa pale pale.
Wananchi kumfata mwenyekiti hana anachosema kumbe kashapata mgao, siku hiyo hiyo Taarifa hadi kwa Diwani akaja pale, nae analeta blah blah, mara tuwe wapolee, , tuwe wapolee wakati mazao yamepotea, mtu kapoteza maisha na kuna majeruhi wanapigania uhai wao.
Tukasema hawa sisi kwa vita hatuwawezi, ngoja tufanye tunavyoeweza, watu wataalamu wakafanya mafekechee, ng'ombe wanajifia km wana kideli vile.
Mbona walihama wenyewe, hawa sio wa kuwachekea, ni wabishi na wajeuri, wakorofi pia.