Watu wa Mbeya (Wanyakyusa) ni watu makini sana, akili kubwa na hawaogopi kitu

Watu wa Mbeya (Wanyakyusa) ni watu makini sana, akili kubwa na hawaogopi kitu

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Hawa watu ni wenye akili sana licha ya kwamba ndani mwao kuna michawa, ambayo kamwe haitakuja kuacha legacy yoyote kwenye uongozi wao.

Boniface Mwabukusi: Mwanasheria msomi, mweledi, ambaye amediriki kuupinga kwa dhati hadi mahakamani mkataba mbovu wa bandari ametokea Mbeya.

Dr. Ulimboka: Daktari aliyeendesha mapambano ya kupigania haki za madaktari na kuboreshewa stahiki zao alitokea Mbeya.

Mwabulambo: aliongoza maandamano chuo kikuu cha mlimani, akamchachafya Nyerere, hadi Nyerere akaamua kupunguza mshahara wake wa shilingi 4,000 bila kodi. Yeye na Baraza lake la Mawaziri.

Hao ni kwa uchache.

NB: Kuna haja ya kukaa chini na kuyarekebisha haya mambo kidiplomasia, hakika inawezekana kwenye meza ya duara. Watu wa Mbeya ni waelewa sana.

Mitume, Wachungaji na Manabii, wengi wanatokea huko. Pia wanamuziki wengi wa nyimbo za dunia na za injili wanatokea huko.

Huko huenda ndio Mlima Sayuni, mlima wa Ukombozi uliko.
Gin Ja Wa
Shincheonji
 
Ukishaona Mchaga anakusifia, 'wewe una akili, unajitambua' basi ujue wewe ni chambo na kibaraka kwao!
 
OK, kumbe CHADEMA sio ya Wachagga tu, Bob Makani ni Msukuma naye alikuwemo.
CCM wanatulisha matango pori. CHADEMA ni ya Watanganyika
Kwa ufupi sana
Mtei - Mchagga

Ngaiza - Muhaya

Mwaikambo - Mnyakyusa

Bob Makani - Musukuma

Tuntemeke Sanga - Mkinga

Ndesamburo - Mchagga

Ndio unawapata sasa akina Mbowe, Mnyika, Mbilinyi, Msigwa, CPA Ruge, BoniYai nk...nk 😂🔥
 
Ni kama inapendeza na kushangaza kwa wakati mmoja, pale ambapo ndani ya mkoa mmoja, wa Mbeya, anakuwepo jasiri muongoza njia, asiyeogopa vitisho vya watawala, asiye na unafiki, aliye tayari kuweka rehani vyeti vyake, hata aipoteze ajira yake, anayesimamia kweli muda wote, akiamini kweli hiyo ndio itamuweka huru, hata kama kwa sasa yupo mikononi mwa askari wa msaliti, lakini naamini ndani ya nafsi yake, yuko huru zaidi ya yule .....

Mnafiki mwingine, anayetokea Mbeya hapo hapo, aliyeamua kujitoa akili makusudi, akakumbatia unafiki, ili kumfurahisha bosi wake msaliti, asiyeona aibu kusema uongo mbele za watu, anayeona sifa kujipendekeza, anayefurahia maisha ya anasa bila kujali wengine, ambaye naamini kabisa, ndani ya nafsi yake anaishi kwa aibu kuu, kwasababu anajua vizuri sana watanganyika sio wajinga, hawadanganyi wao, bali anajidanganya mwenyewe.
 
Hawa watu ni wenye akili sana licha ya kwamba ndani mwao kuna michawa, ambayo kamwe haitakuja kuacha legacy yoyote kwenye uongozi wao...
Aisee, tunapakuliwa Minyama huku balaa. Ila usisahau kuwa Cool Akson naye anatokea Mbeya. Ingawa alipotaka jimbo la Rungwe akaja na ile project yake ya utamaduni akawa anaipeleka mashuleni kuchezesha watoto ngoma, wazee wakam mind na kumwambia huo ubunge anaoutafuta kwa kuwachezesha watoto wetu ngoma asahau.

Wakamuuliza wewe hapo ulipoffika hadi kuwa na PhD , hadi kuwa nsibu Spika ulifika kwa kucheza ngoma? Wewe umesoma, watoto wako umesomesha huko, halafu watoto wetu ndiyo umeona ndiyo wa kuchezeshwa ngoma?

Kusikia hivyo akalazimika kukimbilia Mbeya Mjini.
 
Wakina mwa wamegawanyika pande mbili wa Rungwe na wa Kyela Hawa watu ni chui na paka.
Mwa wa kyela Hawa ni wamalawi au wanyasa chakula Chao kikuu ni wali na samaki wakulima wazuri wa mpunga,cacao ni wajuaji,vichwa ngumu, Wana miili midogo sababu ya joto,wanawake wao weupe.

Hawa kina Mwa wa Tukuyu Hawa ni wasomi, waungwana,Wana miili mikubwa weusi sababu ya baridi,wameshiba sababu ya vyakula vingi wakarimu dhehebu lako kuu ni Moravian,waimbaji wa injili, wachungaji wengi wanatoka huku,kinamama ndio wachapa kazi walea familia wasomi wote ni juhudi za mama zao kuchakarika.

Chakula chao kikuu ni ndizi,viazi chips, kitimoto.

Ni wakarimu watulivu hawana makuu, ukoo mzima wanakusindikiza stand unapungiwa mkono hadi basi litakapotea machoni mwao.

Maharage ya Mbeya maji Mara moja, kina niangusage sambi zako.

Lafudhi Yao mcheki senga Cha pombe rafiki yake pembe.
 
Ingawa alipotaka jimbo la Rungwe akaja na ile project yake ya utamaduni akawa anaipeleka mashuleni kuchezesha watoto ngoma, wazee wakam mind na kumwambia...
Kichekesho cha mwaka, alikuwa hajui akili za wana Rungwe, idhani ni sawaa na za wale òmbaomba wenye trachoma, ukoma na magonjwa ya akili?
 
Back
Top Bottom