Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Nakumbuka enzi hizo kwenda Disco Toto Tembo Beach kila sikukuu za Mwisho wa mwaka, Wasanii wakija Karume Stadium tunasubiria mda wa fungulia mbwa ndipo tuingie wakati kiingilio ni 1000 tu watoto.

Watu maarufu kama Tajiri mwenye mbwembwe Nyakiteri, Dereva wa mbio za magari Mama's, Hussein Sokoni, Redio yetu pendwa Victoria FM hapo utawakuta wakina Boke Wambura, Maregesi Girishon, Emmanuel Chibasa, Issa Nundu, mzee wa Mafua Robson Wangaso na wengineo, mitaa ya Nyasho hapo ndilo chimbo la kujipatia mavazi.

Fujo za Musoma Tech na Songe hadi kupelekea Songe kuwa ya wadada, Mitaa maarufu kama Mukendo, Iringo, Mwigobelo, Majita Road bila kusahau vibaka wa Magamaga, na kila likizo tunakutana tuition Mwembeni hapo utakutana na watoto wa Isenye, Ikizu na sisi wa Bweri Makatani.
Vipi Chikwakara bado yupo hadi naondoka 2009 alikuwa nikati ya washua wenye pesa pale Musoma alikuwa na ghorofa yake inajengwa opposite na Mwembeni
 
Hapana mkuu musoma kwasasa imebadilika sana yan saiv uwezi ilinganisha musoma na mikoa km kigoma, shinyanga, tabora, lindi na singida
musoma saiv inaikaribia moshi kwa uzuri wa mji Over

Musoma hata zamani mwaka 2005 tu ilivokuwa bado imezidi mikoa ya kigoma ,singida ,tabora na shinyanga ilivyo sasa
nadhani sasa hivi imeizidi Moshi ni vile tu sijaenda Musoma toka mwaka 2011
 
Unajua kila mtu anaweza kuwa na mtizamo tofauti juu ya jambo moja. Kama unasema Musoma mjini ni pa kishamba basi labda utupe tafsiri sahihi ya neno ushamba. Kama ni lafudhi makabila yote duniani wana lafudhi tofauti na huo si ushamba, ni sehemu ya utamaduni wa jamii zote, umezaliwa na kukulia mahali fulani muda mwingi wa maisha yako utakuwaje na lafudhi ya jamii nyingine mbali kabisa na wewe? Ushamba ni nini mkuu.

hata mimi sijamuelewa jamaa,hivi kuna sehemu watu wana lafudhi kuzidi Moshi,Arusha na Mwanza kweli ?
by the way lafudhi hata waingeteza wanayo lakini hawajaitwa washamba
 
Hapana mkuu musoma kwasasa imebadilika sana yan saiv uwezi ilinganisha musoma na mikoa km kigoma, shinyanga, tabora, lindi na singida
musoma saiv inaikaribia moshi kwa uzuri wa mji Over

Asee nimekaa Musoma 19 years na nimekaa Moshi 5 years ila uwezi linganisha Moshi na Mass Town asee.

Musoma linganisha na Shinyanga, Tabora, Singida, Kagera, Lindi, Songea maana kwa mikoa iyo Musoma inawakimbiza sana Ao
 
Asee nimekaa Musoma 19 years na nimekaa Moshi 5 years ila uwezi linganisha Moshi na Mass Town asee.

Musoma linganisha na Shinyanga, Tabora, Singida, Kagera, Lindi, Songea maana kwa mikoa iyo Musoma inawakimbiza sana Ao
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
[emoji3][emoji3][emoji3]

Kweli kaka Moshi ni habari nyingine wachaga sio watu poa ukiondoa majiji kama Dar, Mwanza na Arusha sidhani kama kuna Halmashauri au wilaya zinazoikimbiza Moshi.

Yani kuanzia town mpaka vijijin kwao pote ni Barabara za kiwango cha rami, mji uko very well organized asee na Maisha yao yako very simple maana kule ukiwa na buku jero unapata mkungu wa ndizi mzuri kabisa mixer parachichi na Karoti ndio kwao uko.

Kila kijiji sijui machame, Uru,oldmoshi, Rombo kote kuna huduma za maji na hospital sasa kama mjini tu kuna hospital zaidi ya 5 apo uwezi linganisha na Mass town asee afu mzunguko wa pesa Moshi ni mkubwa kuliko Mass town.

Njoo masstown kwanza kwenda popote mjini boda ni 500 afu maeneo yaliendelea ni ya pale pale katikat ya mji sogea pembeni uko kama nyamatare, songe uko hakuna huduma muhimu, ukienda tu pale machinjioni unaona mpka Aibu, Mass town mzunguko wa pesa mdogo kulinganisha na moshi kumbuka moshi wako na sector ya utalii, Masstown sehemu za starehe zinajulikana ni zile zile afu ukiwa na pesa kidogo tu utaona umekua maarufu ghafla full wapambe, vijana hawapendi kufanya kazi zaidi ya usela wa kijinga jinga na makundi ukiwa mgeni au ukiondoka siku ukirudi vijana wanajua unaela wao ni kukupiga virungu tu vya pesa za sigara na pombe.
 
Marehemu Barongo alijenga nyumba na kuzungushia ukuta ukiwa na mfanano wa meli ya MV. BUkoba kama kumbukumbu ya kumpoteza mke wake katika ajali hiyo mwaka 1996....
Barongo alisha farik?i!! Huyu Jamaa nasikia alisha wahi kuwa Afisa Utamaduni hapo Musoma.Mke wake mdogo alimchukua kwa Mzee Mbogola mtaa wa Shomolo upande wa kulia ukitoka Mjini kuelekea Nyasho.
 
Naona mnakumbushana mambo ya juzi ambayo hata sijui kama yametokea, naangalia comments za miaka ya 1991 kurudi nyuma sioni cha kukumbuka, nawapa yangu ya zilipendwa in up on a time.

Mfano, pale Musoma kulikuwa na eneo maarufu sana kwa uuzaji wa samaki wa kukaanga eneo lile liliitwa kwa MZEE CABIN (tamka kibini), ukiachilia majita road hapo nyasho cabin ambapo kwa sasa hilo jina limebatizwa mtaa wa kibini lilitokana na mzee mmoja aliyekuwa na Bar iliyotamba miaka ya 1978-1988 ikiitwa New Embakasy Bar and Lodge na baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Cabin Bar.

Enzi hizo musoma ilikuwa musoma, air Tanzania ilikuwa ikija mara mbili kwa wiki, jumapili na katikati mwa wiki, siku ya jumapili saa 4am ikikaribia kutua tunakimbia stendi kuwahi magazeti na pale Cabin nakumbuka wadau wa kutoka Dar tulikutana hapo kununua samaki wa kurudi nao BONGO 😁.

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom