Inaendelea.
Labda kwa kuwakumbusha vijana wa JK pale musoma kulikuwa na meli ya abilia na mizigo Mv. Victoria ilikuwa ikitia nanga adhuhuri ya saa 12 ambapo abilia wake ni wale pangu pakavu wametoka Bongo au Tigite a.k.a Kigoma na wameshuka mwanza na kupakia kwenye meli mpaka musoma, kumbuka enzi hizo ukikata tiketi Dar unaenda Musoma kwa kutumia vyombo vya TRC.
Na nakumbuka kampuni za mabasi kama Nyanja Bus service, Maratco nk yalikuwa yakielekea huko majita.
Upande wa elimu kulikuwa na ushindani mkubwa kuanzia primary to secondary, walimu wengi hawakutaka shule zao zisionekane, waliosoma Kamunyonge miaka ya 1980 enzi za mwalimu mkuu Massanja mnaweza kukumbuka.
Enzi hizo kwa wanafunzi waliosoma shule kama Mara sec, Mkendo sec, Mara Tech nk, mnakumbuka ushindani wa kufa mtu kwa shule hizi kwanza kwenye kufaulisha, pili kwenye kabumbu ambayo ilikuwa ikipigwa hapo kwenye viwanja vya mara secondary, yaani mpira kabla haujaisha wenye roho nyepesi kwa timu yao iliyoshinda wanaondoka mapema.
Viwanja vya kujirusha vilikuwa vichache sana pale Metropole ilikuwa ni kukesha so mchana inapigwa show ya watoto, ukienda Musoma hotel (daa hii hotel inanisikitisha sana) maana hakuna hotel iliyojengwa kwa ustadi wa hali ya juu na muonekano mzuri kama ile lakini imejisa mwekezaji mwenye maono mazuri ya kuiendeleza matokea yake inekuwa gofu, [emoji116]
View attachment 1633494
Katika pitapita zangu nchini hii hotel ilikuwa ya kisasa pamoja na kuwa ilijengwa up on a time, ilikuwa ukiwa ziwani ukaiangalia hiyo hotel ilikuwa nzuri hata kuliko zinazojengwa leo sehemu kadhaa.
Hapo Musoma hotel kulikuwa na kiwanja kingine cha disco, linaligwa buzuku la maana ....
itaendelea...
holy holm