Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Mkuu ni kwel naamin ata sisi tukiamua basi tunaweza ibadilisha musoma yetu ikawa jama moshi au nakuipita kabisa
 
Tunasubir muendelezo
 
Inaendelea.

Labda kwa kuwakumbusha vijana wa JK pale musoma kulikuwa na meli ya abilia na mizigo Mv. Victoria ilikuwa ikitia nanga adhuhuri ya saa 12 ambapo abilia wake ni wale pangu pakavu wametoka Bongo au Tigite a.k.a Kigoma na wameshuka mwanza na kupakia kwenye meli mpaka musoma, kumbuka enzi hizo ukikata tiketi Dar unaenda Musoma kwa kutumia vyombo vya TRC.

Na nakumbuka kampuni za mabasi kama Nyanja Bus service, Maratco nk yalikuwa yakielekea huko majita, Butata mpaka Bukima.

Upande wa elimu kulikuwa na ushindani mkubwa kuanzia primary to secondary, walimu wengi hawakutaka shule zao zisionekane, waliosoma Kamunyonge miaka ya 1980 enzi za mwalimu mkuu Massanja mnaweza kukumbuka.

Enzi hizo kwa wanafunzi waliosoma shule kama Mara sec, Mkendo sec, Mara Tech nk, mnakumbuka ushindani wa kufa mtu kwa shule hizi kwanza kwenye kufaulisha, pili kwenye kabumbu ambayo ilikuwa ikipigwa hapo kwenye viwanja vya mara secondary, yaani mpira kabla haujaisha wenye roho nyepesi kwa timu yao iliyoshinda wanaondoka mapema.

Viwanja vya kujirusha vilikuwa vichache sana pale Metropole ilikuwa ni kukesha so mchana inapigwa show ya watoto, ukienda Musoma hotel (daa hii hotel inanisikitisha sana) maana hakuna hotel iliyojengwa kwa ustadi wa hali ya juu na muonekano mzuri kama ile lakini imejifia, imekosa mwekezaji mwenye maono mazuri ya kuiendeleza matokea yake imekuwa gofu, 👇



Katika pitapita zangu nchini hii hotel ilikuwa ya kisasa pamoja na kuwa ilijengwa up on a time, ilikuwa ukiwa upande wa ziwani na kuiangalia hiyo hotel ilikuwa nzuri hata kuliko zinazojengwa leo sehemu tofauti.

Hapo Musoma hotel kulikuwa na kiwanja kingine cha disco, linapigwa buzuku la maana ....


itaendelea...
holy holm
 
Basi kumbe wewe ni mkongwe Musoma sisi ni watoto wa juzi hayo uliosema ndo nayasikia
 
Hata mimi hiyo Musoma hotel huwa inanisikitisha sana, sijui kwnn imekosa wawekezaji na wakati ipo sehem nzuri kabisa ya mwambao wa ziwa.
 
UUmenikumbusha miaka ya 94/95, nilienda musoma nikiwa na Land Rover 109,ilikuwa week end kulikuwa na hkumbi Wa disco sikumbuki jina,niliingia hill disco usiku kutoka nkakuta ndondo limevunjwa vioo na wamepora kila kitu na walinzi wapo.
Kesho yake nikariport police wezi wakajulikana,polisi wakaanza kuwafukuza wakazama ziwani wakanza kuwatukana polisi.dah toka Sikh hiyo mpaka Leo musoma sipapendi kabisa.
Nakumbuka jina LA mmojawappo Wa wale wezi mpaka Leo alikuwa anaitwa MAHERI.sijui kama bado yuko hai Huyo mwamba.
 
Musoma tunaita Magido, Mapanki watu wa Mwanza ndiyo wanaita hivyo kipindi hicho pale walipojenga shule ya Baruti secondary ndipo kilikuwa kiwanda cha kukaangia
Madude yana Soup nzito kinyama yaani 🤣🤣🤣🤣

Hivi bado yapo. Enzi hizo tunaenda kuyanunua kwa kujifichaficha.

Na Madon pia walikuwa wanawanunulia mbwa wao.
 
Nadhani hao askali walikuwa wadau wa hao wezi, haiwezekani askali wa miaka hiyo amkimbize mwizi alafu anamuacha aelee majini, NO!
 
Musoma tunaita Magido, Mapanki watu wa Mwanza ndiyo wanaita hivyo kipindi hicho pale walipojenga shule ya Baruti secondary ndipo kilikuwa kiwanda cha kukaangia
Kutokana na ugumu wa maisha haya mapanki yamenikuza aisee.

Kiwanda kwa Teco (nalikumbuka hili jina) tunapanga foleni sh 50 .


Maisha haya.

God bless wamama wote wanaopambania familia zao.
 
Nadhani hao askali walikuwa wadau wa hao wezi, haiwezekani askali wa miaka hiyo amkimbize mwizi alafu anamuacha aelee majini, NO!
Inawezekana walikuwa wanajuana.
Maana walikuwa wanawambia pigeni hizo risasi kama nyie wanaume.
Nkaja kusikia huyo mwamba maheri alikuwa tishio hapo musoma,mwisho wq siku nkaachana na hyo issue nkaondoka kesho yake mpaka leo.
 
Musoma Hotels ilokuwa inamilikiwa na Railways corporation ilikuja kununuliwa na tajiri Mazara sijui aliifikisha wapi
 
Musoma Hotels ilokuwa inamilikiwa na Railways corporation ilikuja kununuliwa na tajiri Mazara sijui aliifikisha wapi
Mazara hakuwa tajiri ila pesa ilipitia kwake, kwa ufupi tajiri huwa hafirisiki ndani ya 10yrs ila utajiri unaendelea hata kwa kurithiwa.

Huyo jamaa sijui mazara hakuwa na uwezo wa kuhimudu ile hotel na sijui kwa nini serikali ilimpa wakati marehemu Mengi walimnyima Kilimanjaro Hotel.

Angalia hotel kadhaa walizopewa wawekezaji wa nje kama Mount Meru, Kilimanjaro Kempinski, Arusha Hotel, nk zinatamba kwenye ushindani wa hotel mpya.
 
Na pale soko kuu kulikuwa na sheikh mmoja ana duka kubwa sana alikuwa mzee alipenda sana kuwapa pipi watoto.
Kma sijakosea aliitwa Mzee Makumpira< sijui kama bado yuko hai, nyumbani kwake kulikuwa kunauzwa kahawa halafu kila ijumaa tukitoka msikitini tunaenda kwake kula pilau!!!!
 
Hotel nzuri kuliko zote ilikua mativila hotel pale karibu na mskiti mdogo..

Kwakweli musoma iko nyuma Sana
Acha utani broo, matvilla ya juzi kabisa hiyozilikuwepo nyingi tu kama silver sand, tembo beach, peninsula hotel na anext nk kibao, ww utakuwa umefika musoma miaka ya 2010 kuja huku!!!
 
Kuna mwamba mmoja alikuwa mtoto wa polisi wanakaa line polisi huku magereza dahh alikuwa mbabe sana, nadhani aliitwa Six, sijui yuko wap siku hizi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…