kianja kyamutwara
JF-Expert Member
- Nov 4, 2020
- 200
- 206
Zote ulizotaja ni za kizaman sana hazina maajabuAcha utani broo, matvilla ya juzi kabisa hiyozilikuwepo nyingi tu kama silver sand, tembo beach, peninsula hotel na anext nk kibao, ww utakuwa umefika musoma miaka ya 2010 kuja huku!!!
kwani babu hapa si tunaongelea vya zamani au vya leo???Zote ulizotaja ni za kizaman sana hazina maajabu
ndio lkn mjaluo wa town [emoji3][emoji3]
Mzee kobasi alikuwa mtu wa CCM Sana mke wake alikuwa mwl kamunyonge watoto wake nawakumbuka ni Musa na kobas maana nimesoma nao kamunyonge.Vipi mzee Kobas unamfahamu ? Na yeye alikua anaishi karibu na kamnyonge primary.
Huyu mzee umaarufu wake sijui ulitokana na nn maana hata kwenye kugombea sikuwahi kumskia,Mzee kobasi alikuwa mtu wa CCM Sana mke wake alikuwa mwl kamunyonge watoto wake nawakumbuka ni Musa na kobas maana nimesoma nao kamunyonge.
Hauwezi kutaja wazee maarufu kwa pale musoma mjini usimtaje huyo mzee.Huyu mzee umaarufu wake sijui ulitokana na nn maana hata kwenye kugombea sikuwahi kumskia,
Anyway namkumbuka wakina Gloria na yule mdogo Jina limenitoka
Musa Kankan,balaa sana yule jamaaMzee kobasi alikuwa mtu wa CCM Sana mke wake alikuwa mwl kamunyonge watoto wake nawakumbuka ni Musa na kobas maana nimesoma nao kamunyonge.
Daa nafurahi Sana kupata hbr hizi nakbuka mbali Sana mwamba.Musa Kankan,balaa sana yule jamaa
Papaaa Barongo namkumbuka Sana na panki lake pia na siruali anavalia tumboni sio kiuononi utadhan mkongo kumbe ni kyoma.Barongo alisha farik?i!! Huyu Jamaa nasikia alisha wahi kuwa Afisa Utamaduni hapo Musoma.Mke wake mdogo alimchukua kwa Mzee Mbogola mtaa wa Shomolo upande wa kulia ukitoka Mjini kuelekea Nyasho.
Acha utani broo, matvilla ya juzi kabisa hiyozilikuwepo nyingi tu kama silver sand, tembo beach, peninsula hotel na anext nk kibao, ww utakuwa umefika musoma miaka ya 2010 kuja huku!!!
Baiskeli za maganga ukifaulu form1 lazima ununuliweNyakato Mtaa wa vibaka na walevi wa ngogo wachawi miaka hio tunaenda baruti kufata mapanki[emoji16] Disco Toto Mama Ester in, peninsula beach watoto wa kishua wanatokea kamnyonge biafla na kambi za FFU December tunaenda mwembeni kutafuta pisi Kali Enz hizo baskeli za maganga ndo dili Mjini Mistu wa Babu Kenge,
Nakumbuka enzi hizo kwenda Disco Toto Tembo Beach kila sikukuu za Mwisho wa mwaka, Wasanii wakija Karume Stadium tunasubiria mda wa fungulia mbwa ndipo tuingie wakati kiingilio ni 1000 tu watoto.
Watu maarufu kama Tajiri mwenye mbwembwe Nyakiteri, Dereva wa mbio za magari Mama's, Hussein Sokoni, Redio yetu pendwa Victoria FM hapo utawakuta wakina Boke Wambura, Maregesi Girishon, Emmanuel Chibasa, Issa Nundu, mzee wa Mafua Robson Wangaso na wengineo, mitaa ya Nyasho hapo ndilo chimbo la kujipatia mavazi.
Fujo za Musoma Tech na Songe hadi kupelekea Songe kuwa ya wadada, Mitaa maarufu kama Mukendo, Iringo, Mwigobelo, Majita Road bila kusahau vibaka wa Magamaga, na kila likizo tunakutana tuition Mwembeni hapo utakutana na watoto wa Isenye, Ikizu na sisi wa Bweri Makatani.
Kuna jamaa pale Baruti alikuwa amejenga nyumba muundo wa meli, sijui aliwaza nn
MabuimwerafuruBweri Makatani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Musoma wajuaji wengi ila wajanja wa maisha wachache, nimekaa musoma miaka kadhaa na Tarime pia, kwa miji ya Mara bora Tarime kuna aina fulani ya maisha kwa mtu mwenye kuitaji kutoka wajita wa musoma maneno mengi sana..
Kuna mmoja niliwai kumtoa jino katika gym ya pale pembeni ya uwanja wa karume.. nilikuwa mgeni kule ila kwa sababu napenda mazoezi nikaulizia nikaelekezwa mahala pa gym.. nimefika siku ya kwanza, pili ya tatu jamaa akaanza kuwa anafuatilia maisha yangu... alifikiri siwezi mfanya kitu nilimpa ngumi moja jino likadondoka mpk leo sitasahau hakuna aliyethubutu kunisogelea maana inaelekea yeye ndo alikuwa nunda pale.
Nilikaa miaka 2 hivi nikahamishwa kikazi. Ila wasichana tu wa kule mwanaume unatongozwa kabisa kulikuwa na hotel moja hivi kubwa tu ipo pembezoni mwa ziwa nimeishau jina, nimekula sana samaki pale na pombe sana. Matajiri wa pale ni akina matayo, hussein sokoni, ila wana maisha ya kishamba sana aise. Mitaa naikumbuka kamyonge, umoja, makoko nk, jamaa, zangu walikuwa huyu aliyegombea ubunge, akina Bailes na wengine nimewasahau. Ila sijawai kutamani kurudi kule.