Watu wa Sheria Nisaidieni kwenye hii ndoa ya Dada angu

Hapo mkuu wakiingia kwenye sheria huyo jamaa hana chake,na tuliotunga hizo sheria ni sisi wanaume wenyewe...
Jamaa hana chake kivipi wakati wameishi na mwanamke huyo kihawara na mwanamke ndiye anaishi kwa huyo jamaa?

Sheria za ndoa za '71 zinazotumika sasa zipo wazi kuhusu kipengele hicho.

Mwanamke atahesabika kuwa ana haki, kama watafunga ndoa ya aina yoyote, iwe ya dini, kiserikali ama ya kimila.

Kuishi kwa utaratibu wa 'sogea tukae', mwanamke ndiye hana chake.
 
Nashindwa namna ya kukujibu mkuu ila sijafika hapa kusimulia maisha ya dada angu , mm sijui wanaishije kwenye hiyo ndoa , sijui sababu ya jamaa kuoa mke mwingine , nimekuja hapa kuomba ushauri wa kisheria jinsi ya kumsaidia dada angu ,
Wewe kama huna msaada wa kisheria naomba kaa kimya usiniulize Kwann jamaa kaoa mke wa pili hayo sio maswali ya kisheria..
Niulize kuhusu uhalali wa Mali nitakujibu na mambo mengine ya kisheria
 
Mali zote nilizotaja hapo wamezichuma wakiwa wote , mwanzon walikuwa wanaishi Kwa wazazi , wakaanza ujenz wa nyumba mpaka wakahamia , kwenye ishu ya mashamba Kuna mashamba mume wake alipewa na wazazi wake lakini Kuna mashamba ambayo waliyanunua pindi anaishi na sister ,
 
Kufuatilia ndoa ya Dada yako ni wehu mkubwa sana, pambana na maisha yako mdogo wangu ukiona hivyo ujue kuna kasoro shemej yako alibaini kwa dada yako na labda anakaa nae kwa sababu ya watoto na huruma tu, hakuna mwanaume anaeweza kuoa mke wa pili kabla hajatoa mahari kwa mke wake mkubwa ambae wameanza nae maisha, hii ilishanikuta mimi, nikiwa chuo nilianzisha mahusiano na mnyakyusa mmoja hivi changamoto sana tukipishana kidogo mamayake ananitumia sms za matusi na ndugu zake yaani hakuna amani ila tayari katika haso zangu nilijenga nyumba nikiwa bado naishi nae na tukapata watoto wawili tangu 2019. Ila Bi dada huyu tatzo likitokea ni sim kwao na ndugu zake wanaanza kunitukana tena matusi ya nguoni hadi nikaona jau kwenda kwao nikamkaushia tu, kama mwanaume nina ham ya kuoa ila nilishaona ninaeishi nae sio mtu sahihi ikabidi niowe mke mwingine kwa siri mwaga ugali ni mwage mboga, nikampangia na alipogundua kwao wakawaka balaa matusi kama yote akaondoka na kuniachia watoto akarud kwao, ikabidi nimchukue B mdogo kahamia mjengoni maisha yakaendelea rasmi, kuna utofauti mkubwa sana niliuona na nikaanza kuexperience furaha ya ndoa. Baada ya life kumpiga Mnyakyusa na alitoka kwa mbwembwe na matusi kutoka kwa ndugu zake kuwa watamfungulia Biashara nikasema fresh tu, Amerudi kwao hamna walichomfanyia zaidi ya kumuweka amekaa ameona life haliendi ikabidi anitafte akiomba nimrejeshe hom na nyumbani tayar mjengo ushamilikiwa na B mdogo kwa huruma tu nimempangia chumba kimoja huko uswahilini anakaa ila namhudumia na nikijskia kwenda kumpelekea mto huwa naenda anajiona kama mke asiye na mamlaka na mimi tena kama awali, na hapo anakaa kwangu na kwao hawajui kama alisharudi kwangu kwa kunipgia magoti na nimempangia uswahilini, hapa nimemuweka katika kipindi cha uangalizi akae kama miaka 2 nikiona amerekebika nitamjengea na nitamlipa mahali ila atakuwa mke Mdogo na si mkubwa tena maana mke mdogo nilishamtolea mahari kabla yake.

Ogopa sana kuoa familia ambayo wanadekeza binti yao ni hatari sana na mnamharibia dada yenu maisha nyie sisi wanaume hatukomolewi.
 
Pole sana mkuu, kwa ninavyofahamu ukiishi na mwanamke ndani kiunyumba kwa miezi 6 tu tayari huyo ni mke, sembuse dada yako ana watoto 3 kabisa.

Mali zote zilizochumwa akiwa na mke mkubwa, zinawahuhusu yeye mume, mke mkubwa na watoto.

Mke wa pili hausiki na mali alizozikuta, yeye atahusika na mali zitakazotafutwa baada ya yeye kuolewa (Lakini ikitokea huyu mke mdogo akapata watoto, basi watoto wake watahusika na mali alizozikuta mama yao, kisheria watoto wanathaminiwa zidi)

Iila huyo jamaa mbona kawafanyia dharau kubwa hivi? Yaani uoe mke mwengine halaf umlete nyumbani kwenye nyumba uliyojenga na mke mkubwa?

Changamoto za kutokujua haki za ndoa wahanga wakubwa hua ni wanawake.
 
Ukimkomalia shemeji,Mkomalie na dadako miaka yote kumi alikuwa wapi kushindwa kushawishi shem atoe mahari
 
inaonekana shida yenu ni mali zaidi kuliko amani ya dada yenu.
 
You are wrong.

Rejea kusoma tena Sheria hiyo pamoja na Kanuni zake, hususani kwenye Fungu linaloelezea kuhusu suala la Dhana ya Ndoa (Presumption of the Marriage).
Kifungu hiki kiliwekwa makusudi kwenye Sheria hiyo ili kulinda haki za Wanandoa(hususani Wanawake) kuhusu suala hili la haki ya Mali za Chumo la Ndoa (Matrimonial Property) kwa Wanandoa ambao hawajafunga ndoa rasmi inayotambulika na Sheria za Serikali, yaani ndoa ya Kanisani, Msikitini au Ndoa ya Bomani kwa Mkuu wa Wilaya.
 
Sheria ya Ndoa inaeleza wazi kabisa kuhusu haki ya kila mmoja endapo upendo umeisha na wanahitaji kutengana.

Mwanamke atapata haki zake zote walizochuma pamoja kisheria na watoto pia watapata haki zao.

Endapo ndoa imefika mwisho anzieni kwenye ofisi ya kata, baada ya hapo Mahakama ya Mwanzo na kuendelea mtapatiwa haki zenu Kisheria.
 
Haujamjibu wala kumsaidia kadiri ya utaratibu/sheria ila umeeleza kuhusu hasira zako tu.
 
Usibwabwaje pitia kwa wanasheria ww si fundi simu isijaribu kuifungua iPhone 16 kuangalia system charge nataka kusema kwamba ndo haiamuliwi kwa kufikiri na kudhani nenda kwa wanasheria wakupe tafsiri ya neno "consecutive two years" utabadoli unavodhani
 
Na wengi wamemuuliza aliolewa tena kwa Sheria gani anambwela mbwela watu wanataka kujua ni mke au hawara kwenye sheria hali ni mbili tu
 
Elekeza bila kukera(kubwabwaja maana yake ni nini?).Au unataka aende kwa wanasheria wa mwaka af-mbili awakute bado na hangover ya vikali/masters na visungura?
 
Nadhani swali la msingi hapa ni Sheria inamlindaje mwanamke au mwanandoa wa dhana ya ndoa (presumption of marriage).

Kwanza ifahamike hakuna Talaka kwenye dhana ya ndoa.

Pili anachoweza kufanya Mwanamke huyu, kama anatendewa vitendo vilivyokatazwa kisheria, kama ukatili, ni kufungua mchakato wa utenguzi (dissolution) au utengano (separation). Kwenye dissolution itafanana na Talaka na Haki zake za mgawanyo wa Mali walizochuma pamoja na pia Amri ya matunzo itatolewa.

Mchakato huo utaamua, ikiwa dhana ya ndoa imethibitika, kama ndio, ikiwa Kuna Mali za pamoja, kama ndio, mgawanyo wake utakuwaje, ikiwa Kuna wategemezi, kama ndio, watatunzwaje na nani n.k n.k.

Njia za kupitia ni zile zile za mwanandoa anayetaka Talaka.
 
Absolutely
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…