Watu wa Sheria Nisaidieni kwenye hii ndoa ya Dada angu

Watu wa Sheria Nisaidieni kwenye hii ndoa ya Dada angu

Dada angu kaolewa miaka karibia 10 Sasa , ana watoto watatu , wamejenga nyumba, na wanamiliki mashamba makubwa ambayo Yana mazao kila mwaka wanavuna.
Bwana ake (shemeji) mpaka Sasa hajamtolea mahali dada angu tumejaribu kufwatilia kama family bwana shemej anapiga Kona Kona nyingi sana , Hilo la kwanza .

Kitu cha pili ndo kilichonifanya nije niombe ushauri kwenu , Ni kwamba shemeji yangu mwaka huu kaoa mke wa pili na wanaishi nyumba moja ambayo dada angu anaishi (nyumba ambayo alijenga dada na huyo mume wake)
Baada ya kuingia huyu bi mdogo inaonekana bwana shemeji anamsikiliza sana bi mdogo na hata wazazi wa mume wanamsikiliza sana mke wa pili .

Kuna unyanyapaa dada angu anaupitia ikiwemo kupigwa pale ambapo anadai haki yake ikiwa pamoja na hela ya matumizi.

Kwa Sasa Dada anataka kuachana na huyo mwanaume na sisi kama kaka zake tunatamani iwe hivyo . Shida inakuja kwenye kupata haki zake za Mali walizochuma kama nyumba , pikpk na mashamba ,

Je mwanamke akiomba talaka anaweza akapata mgao wa Mali alizochuma na Mr ake ,
Au utaratibu Gani atumie hapa ili aachane na Mr ake bila kupoteza haki zake za umiliki wa Mali walizochuma??
Msaada wenu
MGAWO LAZIMA APATE SAWA KWA SAWA.

LAKINI KWANINI ALIKUBALI MKE MDOGO AJE AISHI NYUMBA ALOJENGA YEYE BILA KUSHITAKI?
 
Mtu hajatolewa mahari halafu unasema ameolewa! Ameolewaje sasa! Halafu ukome kufuatilia ndoa ya dada yako kama mmeolewa pamoja,utaolewa bure kwa tamaa ya mali isiyokuhusu.
Wewe dada yako akiteswa na mumuwe hutaona sababu ya kumsaidia? Halafu mahari na ndoa ni vitu viwili tofauti, mtu aweza kuolewa bila kutolewa mahari.
 
Nashindwa namna ya kukujibu mkuu ila sijafika hapa kusimulia maisha ya dada angu , mm sijui wanaishije kwenye hiyo ndoa , sijui sababu ya jamaa kuoa mke mwingine , nimekuja hapa kuomba ushauri wa kisheria jinsi ya kumsaidia dada angu ,
Wewe kama huna msaada wa kisheria naomba kaa kimya usiniulize Kwann jamaa kaoa mke wa pili hayo sio maswali ya kisheria..
Niulize kuhusu uhalali wa Mali nitakujibu na mambo mengine ya kisheria
Hiyo ndoa yao ipo kiaje mkuu? Ina makarqtasi yeyote?
 
Wewe dada yako akiteswa na mumuwe hutaona sababu ya kumsaidia? Halafu mahari na ndoa ni vitu viwili tofauti, mtu aweza kuolewa bila kutolewa mahari.
Siingilii uhusiano wa dada yangu,Ndoa ninayoijua mimi sharti mahari itolewe kwanza hata kama haijamalizwa ndiyo iwe ndoa hizo nyingine sizifahamu kwahiyo siwezi kuzisemea.
 
Marriage Act of 1971 haizungumzii mahari kama kigezo cha ndoa kuwa halali
Mimi kwangu ndoa siyo sheria tu bali sharti la kidini ndiyo muhimu zaidi,kuna nchi zimeruhusu ndoa za jinsia moja lakini kiuhalisia hiyo haiwezi kuwa ndoa japo sheria ya nchi husika imeruhusu.
 
Siingilii uhusiano wa dada yangu,Ndoa ninayoijua mimi sharti mahari itolewe kwanza hata kama haijamalizwa ndiyo iwe ndoa hizo nyingine sizifahamu kwahiyo siwezi kuzisemea.
Basi ndio ujue kuwa mahari sio lazima coz ndoa ni makubaliano ya watu wawili, hao wakisharidhiana ndoa inafungwa bila shida.
 
Basi ndio ujue kuwa mahari sio lazima coz ndoa ni makubaliano ya watu wawili, hao wakisharidhiana ndoa inafungwa bila shida.
Ndoa ninavyojua mimi mahari ni lazima ,bila mahari hakuna ndoa.
Mwanamke anayejipeleka mwenyewe kama mbuzi kwa mwanaume kwa kisingizio cha makubaliano huyo siyo mke ni hawara tu hata waishi miaka 100.
 
Je, una uhakika kuwa Mali hizo ulizozitaja hao Watu walichuma wote kwa nguvu ya pamoja, yaani mali hizo ni Chumo la Ndoa?? Dada yako hakumkuta nazo hizo Mali huyo mtu unayedai kuwa ni mume wake??? Huyo mke wa Pili aliingia na kuishi kwenye nyumba waliyojenga kwa makubaliano gani kati ya huyo dada yako na huyo mume wake??

Endapo kama kweli Mali hizo ni Chumo la Ndoa, Basi hakuna wasiwasi kwamba dada yako anaweza akadhulumiwa endapo kama ataamua kuomba talaka na kudai haki yake kuhusiana na Mali hizo.

Kwa Sheria za Tanzania, uwepo wa ndoa kati ya mume na mke hauthibitishwi kwa kuwepo kwa vyeti vya ndoa tu peke yake, Bali hata kwa kitendo cha watu hao wawili kuishi pamoja 'pika na kupakua' kwa muda usiopungua miaka miwili mfululizo na majirani (jamii) ikiwa inafahamu kuwa watu hao ni mume na mke. Kitendo hiki peke yake ni uthibitisho tosha kabisa kwamba kuna ndoa Kati ya Watu hao wawili. Rejea kwenye Sheria ya Ndoa ya 1971 (na Marejeo yake) kuhusu kitu kinachoitwa "Dhana ya Ndoa" au Presumption of Marriage.
Asuming kuna huo msingi wa "ndoa ya dhana", je talaka inatokaje hapo? Inabidi ku-petition for talaka au huyo mama aende kuomba machumo ya ndoa moja kwa moja?
 
Msaada unaomba wewe halafu ndoa ni ya dada yako. Kuna kitu hakiko sawa kwa upande wenu wa kike, si ajabu jamaa kawaolea mke mwenza.
 
Vijana wa siku hizi Bure kabisa yaani

We kenge unakaa na kende zako umening'iniza unawazia mgao wa pikipiki dada akiachika

Watu wengine sijui mkoje asee. Hebu acha ujinga katafute kazi huko!
 
Vijana wa siku hizi Bure kabisa yaani

We kenge unakaa na kende zako umening'iniza unawazia mgao wa pikipiki dada akiachika

Watu wengine sijui mkoje asee. Hebu acha ujinga katafute kazi huko!
🤭😊😊
 
Vijana wa siku hizi Bure kabisa yaani

We kenge unakaa na kende zako umening'iniza unawazia mgao wa pikipiki dada akiachika

Watu wengine sijui mkoje asee. Hebu acha ujinga katafute kazi huko!
😀
 
Dada angu kaolewa miaka karibia 10 Sasa , ana watoto watatu , wamejenga nyumba, na wanamiliki mashamba makubwa ambayo Yana mazao kila mwaka wanavuna.
Bwana ake (shemeji) mpaka Sasa hajamtolea mahali dada angu tumejaribu kufwatilia kama family bwana shemej anapiga Kona Kona nyingi sana , Hilo la kwanza .

Kitu cha pili ndo kilichonifanya nije niombe ushauri kwenu , Ni kwamba shemeji yangu mwaka huu kaoa mke wa pili na wanaishi nyumba moja ambayo dada angu anaishi (nyumba ambayo alijenga dada na huyo mume wake)
Baada ya kuingia huyu bi mdogo inaonekana bwana shemeji anamsikiliza sana bi mdogo na hata wazazi wa mume wanamsikiliza sana mke wa pili .

Kuna unyanyapaa dada angu anaupitia ikiwemo kupigwa pale ambapo anadai haki yake ikiwa pamoja na hela ya matumizi.

Kwa Sasa Dada anataka kuachana na huyo mwanaume na sisi kama kaka zake tunatamani iwe hivyo . Shida inakuja kwenye kupata haki zake za Mali walizochuma kama nyumba , pikpk na mashamba ,

Je mwanamke akiomba talaka anaweza akapata mgao wa Mali alizochuma na Mr ake ,
Au utaratibu Gani atumie hapa ili aachane na Mr ake bila kupoteza haki zake za umiliki wa Mali walizochuma??
Msaada wenu
Umeoa
Kama umeoa
Talaka achana nayo unatesa wajomba zako
Kama dada mshauri avumilie tu kikubwa asinyim.we mshededeee basi
...inaendelea
 
Dada ako atapata mgao wa mali endapo atathibitisha alichangiaje upatikanaj wa hizo mali. Akishindwa kutoa vielelezo hapat kitu.
 
Back
Top Bottom