Uchaguzi 2020 Watu wakijitokeza kwa wingi kupiga kura kesho, itakuwa ni dalili ya awali ya Lissu na upinzani kwa ujumla kuzoa kushinda huu uchaguzi

Uchaguzi 2020 Watu wakijitokeza kwa wingi kupiga kura kesho, itakuwa ni dalili ya awali ya Lissu na upinzani kwa ujumla kuzoa kushinda huu uchaguzi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Wandungu, kesho mkiona watu wamejitokeza kwa wingi kupiga kura, basi mtambue hiyo ni dalili ya mapema kabisa kuwa Lissu na wagombea wengine wa upinzani wanakwenda kupata kura nyingi na za ushindi ingawa tatizo linaweza kuwa katika kuwatangaza.

Sababu kubwa ni kuwa,siasa za kuhamahama kwa kile kilichoitwa kuunga mkono juhudi, na kuvurugwa kwa chaguzi za marudio pamajo na ule uchaguzi wa mwaka jana wa serikali za mitaaa, ni mambo yaliyowakatisha tamaa sana wananchi wengi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Tukumbuke watu wengi(hata hapa JF wapo) waliokuwa wameapa kutojisumbua kwenda kupiga kura wakiamini hakutana tena uchaguzi wa maana chini ya utawala huu.

Hivyo,kesho mkiona kuna idadi kubwa ya watu wamejitokeza katika vitu vya kupiga kura,mjue ni Lissu na wapinzani kwa ujumla ndio wamefanya watu wawe na hamu/hamasa ya kwenda kupiga kura na wote hao watampigia kura Lissu na wagombea wengine wa upinzani.

Vile vile,turnout ikiwa kubwa,ni ishara nyingine ya wapiga kura kuwa teyari kulinda kura kama wanavyohimizwa na wanasiasa wa upinzani.

Vile vile idadi ya wapiga kura ilkiwa ndogo ni ishara ya CCM kulataliwa kwa kushindwa kutimiza kila wananchi walichokitaka na pia itakuwa ni dalili ya upinzani kushinda ila by narrow margin .

Kwahiyo, watu wakijtokeza kwa wingi hiyo kesho, CCM bado itakuwa katika wakati mgumu na wakijitokeza wachache, CCM bado tu itakuwa katika hali ngumu zaidi.

Hata hivyo,mpaka sasa dalili zinaonyesha hamasa ya kupiga kura iko juu, na kwamba wengi watajitokeza hiyo kesho kupiga kura kwa lengo la kumpumzisha Magufuli na CCM yake.

Habari ndio hio.
 
Mujifunzew kufikiri kabla hamjaamua kuweka mabandiko humu!upuuzi gani huu?
 
Nikwambie tu,kwa hali tuliyopitia watanzania wa makundi mbalimbali ndani ya hii miaka mitano ya Magufuli, wengi watakuwa na hofu/woga wa kumpigia kura Magufuli sawa na hofu aliyonayo mtu alieumwa na nyoka aguswapo na jani.
 
Kwahiyo hao watu watakuwa automatically wameenda kumpigia kura Lisu?
 
Nikwambie tu,kwa hali tuliyopitia watanzania ndani ya hii miaka mitano ya Magufuli, wengi watakuwa na hofu/woga wa kumpigia kura Magufuli sawa na hofu aliyonayo mtu alieumwa na nyoka aguswapo na jani.
Ni nyie hapo chadrama ndio mnahofu! Siyo watanzania
 
Ivi ishu ya kuwepo mbali na kituo chako ndo hupigi hivi au maan sielewi kila siku nasikia jipya...
 
Ukiona watu ujue ndo wameenda kumuongezea tena 5 Tenaaa Rais Magufuli....kesho tunaenda kumchagua Magufuli kwa upendo mkubwa.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Ukweli ni kwamba kesho sitoweza kupiga kula kwa mara yangu ya kwanza tangu nifikishé miaka 18, sikuweza kujiandikisha coz sikuwepo nchini na nafsi yangu inauma sana kwa kukosa nafasi hii kuweza kusisulubu CCM.
 
Ukweli ni kwamba kesho sitoweza kupiga kula kwa mara yangu ya kwanza tangu nifikishé miaka 18, sikuweza kujiandikisha coz sikuwepo nchini na nafsi yangu inauma sana kwa kukosa nafasi hii kuweza kusisulubu CCM.
endelea kuombea HAKI , amani itakuja automatic
 
Back
Top Bottom