Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Sawa.

Wewe huamini kama mungu yupo, mimi naamini, je, una uhakika umenizidi akili?? Una uhakika umenizidi uwezo wa kufikiria??
Akili kila mtu anazo.

Hakuna uhusiano wowote ule wa kuamini Mungu na kuwa na akili na kutokuwa na akili, Au kutomwamini Mungu na kutokuwa na akili na kuwa na akili.
Kwa ulichoandika hata Isaac Newton(aliyekuwa anasoma sana bible) hana akili na ana uwezo mdogo wa kufikiria sio??
 
Akili wanazo.

Ila akili yao wame ijengea imani ya kufikirika tu kwamba kuna invisible creature beyond the sky anaitwa Mungu.

Sasa imani hiyo iliyopo akilini mwao sio sawa.
 
Sifa za Mungu unazijua?

Au huzijui?
Kuna watu wanaamini uwepo wa Mungu ila hawaamini katika dini hivyo hutofautiana kwenye hayo masuala ya sifa za Mungu na watu wenye kuamini katika dini, na hata humu utaona wenye kuamini Mungu pasina kuamini katika dini huwa hawana shida sana na hoja za atheists humu kwa sababu sehemu kubwa ya hoja za atheists humu zinagusa zaidi masuala la dini kuliko msingi wa imani ya kuwepo Mungu.

Je, unataka kujadili uwepo/kutokuwepo kwa Mungu au sifa Mungu?
 
Mungu huyo ni nini?

Tuanze kwanza hapa.
 
Kwahiyo wewe ndio unajiona unauwezo wa kufikiri wakati ndio kiraza namba Moja

Umeka katika aridhi ambayo inazunguka na kutembea Kwa Kasi lakini wewe ahuhisi chochote Wala ukishika maji katika glasi hayamwagiki kwakuwa wewe kilaza unahisi hivi vitu vimejiplani vyenyewe tu

Na katika uchunguzi wangu nimegundua wengi wenu mnaopinga uwepo wa Mungu ni vijana ambao mmelelewa katika familia za Kikristo

Kwa sababu mlipokuwa wadogo mlionyeshwa kisanamu Kina mtu amevaa kitaulo ametundikwa msalabani alafu mkaambiwa huyu ndio Mungu wenu

Sasa mnapokuwa wakubwa mnagundua kuwa hapo mmedanganywa mnachanganyikiwa na kusema hakuna Mungu wazungu wajanja sana lengo lao limetimia

Lakini mtoto aliyelelewa katika uislam hata akiwa mkubwa hauwezi kumdanganya kitu kuhusu Mungu na ukimwambia hakuna Mungu ndio kabisa anakuona kilaza wa vilaza
 
Akili wanazo.

Ila akili yao wame ijengea imani ya kufikirika tu kwamba kuna invisible creature beyond the sky anaitwa Mungu.

Sasa imani hiyo iliyopo akilini mwao sio sawa.
Kumbuka niliuliza swali kwa nini kupinga uwepo wa Mungu kunahusishwa na kuwa na akili sana na kuamini Mungu kunahusishwa na kutokuwa na akili sawa sawa? Na hata wewe kuna sehemu umesema kuwa hata mtoto mdogo anatambua kuwa Mungu huyo hayupo, maana yake wenye kuamini Mungu wana upungu wa akili ndogo hata kiwango cha mtoto.
 
Na huyo Allah wenu aliji plan mwenyewe tu?
 
Kuna kipimo cha kupima akili?

Uwingi na udogo wa akili unapimika vipi?
 
Kujadili uelewa wangu binafsi kuhusu Mungu sidhani kama ina msaada kwenye huu mjadala.
Sasa kwa nini unasema huyo Mungu hausishwi na sifa zake?

Weka hapa mtazamo wako na uelewa wako wa Mungu bila kuhusisha sifa zake.
 
Sasa kwa nini unasema huyo Mungu hausishwi na sifa zake?

Weka hapa mtazamo wako na uelewa wako wa Mungu bila kuhusisha sifa zake.
Nimeeleza huko juu kuwa watu wa dini hutofautiana baadhi ya mambo kuhusu Mungu ikiwemo hizo sifa za Mungu ila wote kwa pamoja wanaamini uwepo wa Mungu na wengine hawaamini kabisa maelezo ya dini kuhusu Mungu ila wanaamini Mungu, sasa wewe ukija hapa ukaanza kuchambua hizo sifa za Mungu na ukaonyesha makosa inakuwa haujafanya kitu cha tofauti na wenye kuamini Mungu. Ndio maana nasema kuna uwepo wa Mungu na mambo yenye kuhusishwa na huyo Mungu.
 
Neno Mungu hutumika kwa anayeaminika kuwa ni muumbaji wa huu ulimwengu, na pia mungu hutumika kwa chochote chenye kuabudiwa na binaadamu.
Mungu Anaaminika tu yupo,lakini si kwamba anathibitishika yupo.

Hivyo Mungu huyo hayupo katika uhalisia ila katika dhana ya kufikirika tu.
 
Mkuu dini zote zina sifa zilizo sawa kumhusu Mungu.

Dini zote zina amini kwamba Mungu ni muumbaji, mkuu na ni mkamilifu.

Dini zote zina amini kwamba Mungu ni muweza wa yote.

Dini zote zina amini kwamba Mungu ni mwenye kujua yote.

Sasa kama kuna dini inayo amini Mungu mwenye sifa tofauti na hizi hebu nitajie.
 
Kwahiyo mkuu ulitoa mfano wa kwamba hata mtoto mdogo hawezi kukubali huyo Mungu ulikusudia nini?
Yani kwamba hata mtoto mdogo anaye teseka na shida za dunia ukimwambia kwamba Mungu ni mwema na mwenye Upendo na huruma atabaki na maswali mengi yasiyo na majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…