Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Hoja nyepesi mno hazina hata mashiko wala ushawishi.
Kuna watu humu wakiandika hoja zao kuhusu kutokuwepo kwa Mungu usipojiangalia utajikuta umeelekea kibla ila kwa vihoja hivi vyako vyepesi namna hii kajipange upya pengine ukawa na ujinga mwingi kichuani kuliko uerevu unaojifikiria.
 
Mkuu dini zote zina sifa zilizo sawa kumhusu Mungu.

Dini zote zina amini kwamba Mungu ni muumbaji, mkuu na ni mkamilifu.

Dini zote zina amini kwamba Mungu ni muweza wa yote.

Dini zote zina amini kwamba Mungu ni mwenye kujua yote.

Sasa kama kuna dini inayo amini Mungu mwenye sifa tofauti na hizi hebu nitajie.
Labda hujaelewa point yangu. Sasa hapo na wasio na dini ila wanaamini Mungu nao unawaweka nafasi gani?
 
Vipi watoto wadogo wanaokufa kwa baa la njaa maeneo mbalimbali duniani lakini Mungu huyo hajawahi kuwapa msaada wowote ule?

Watoto wadogo tu hawana uhakika wa kula na huyo Mungu hana msaada wowote kwao, wengi wamekufa, wanakufa na wanaendelea kufa.

Fuatilia vifo vya watoto wadogo wanaokufa kwa njaa nchi za Ethiopia, Somalia, Afghanistan, Kaskazini kwa kenya n.k

Sasa kama Mungu huyo Kashindwa tu kuwapa uhakika wa kula watoto wadogo kama hawa, Sembuse mimi mtu mzima?

Mungu huyo hana msaada wowote ule kwenye uhakika wa kula kwa wanadamu.

Mungu huyo hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Israel huko mamia ya watu wanakufa eti kisa wanampigania Mungu wao, it doesn't make sense
 
Huwa naona kama kutokuamini Mungu kuna husishwa moja kwa moja na kuwa na akili sana, hivi kwa nini inakuwa hivyo japo kwenye maisha ya kawaida hakuna huo utofauti kuonyesha kuwa wasioamini Mungu ndio wenye akili kuliko wenye kuamini Mungu?
Kufikiri tofauti kunahitaji utulivu wa akili.
 
Sawa.

Wewe huamini kama mungu yupo, mimi naamini, je, una uhakika umenizidi akili?? Una uhakika umenizidi uwezo wa kufikiria??

Kwa ulichoandika hata Isaac Newton(aliyekuwa anasoma sana bible) hana akili na ana uwezo mdogo wa kufikiria sio??
Siwezi kusema unanizidi au nakuzidi ila naweza sema hujapenda kufikiri tofauti, kuna tofauti kati ya kufikiri sana na kufikiri tofauti.
 
Kwahiyo wewe ndio unajiona unauwezo wa kufikiri wakati ndio kiraza namba Moja

Umeka katika aridhi ambayo inazunguka na kutembea Kwa Kasi lakini wewe ahuhisi chochote Wala ukishika maji katika glasi hayamwagiki kwakuwa wewe kilaza unahisi hivi vitu vimejiplani vyenyewe tu

Na katika uchunguzi wangu nimegundua wengi wenu mnaopinga uwepo wa Mungu ni vijana ambao mmelelewa katika familia za Kikristo

Kwa sababu mlipokuwa wadogo mlionyeshwa kisanamu Kina mtu amevaa kitaulo ametundikwa msalabani alafu mkaambiwa huyu ndio Mungu wenu

Sasa mnapokuwa wakubwa mnagundua kuwa hapo mmedanganywa mnachanganyikiwa na kusema hakuna Mungu wazungu wajanja sana lengo lao limetimia

Lakini mtoto aliyelelewa katika uislam hata akiwa mkubwa hauwezi kumdanganya kitu kuhusu Mungu na ukimwambia hakuna Mungu ndio kabisa anakuona kilaza wa vilaza
Galileo Galilei aliuawa na wakatoliki sababu alisema ukweli kuwa dunia inazinguka jua, alifikiri tofauti
Wanachoamini wengi haimaanishi kuwa ndio sahihi
 
Siwezi kusema unanizidi au nakuzidi ila naweza sema hujapenda kufikiri tofauti, kuna tofauti kati ya kufikiri sana na kufikiri tofauti.
Mzee usikariri, eti kufikiria tofauti, kivipi??unafikiriaje tofauti?? Unadhani kila mtu anayeamini katika mungu ni mwoga wa moto?? Au ana hofu ya neno liitwalo "dhambi"?? some of us tushawahi kuwa atheists na bado tukarudi kuamini katika mungu, USIKARIRI MZEE.
 
Mungu ana akili sana.

Ulimwengu wa Roho hauwezi kuuingia kwa kutumia mbinu za kimwili. Imani (ambayo huonekana ujinga kwa waliojaa 'hekima, uwezo wa kufikiri) ndio kianzio. Ukijishusha, ukasema 'Naamini', ndio unaanza kuona hadi maono wazi wazi.

Rejea andiko hili:

”bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;“
‭‭1 Kor‬ ‭1‬:‭27‬ ‭SUV‬‬
Unawezs kuthibitisha ulimwengu wa kiroho kama upo?
 
Kuna tofauti kubwa kati ya uwezo wa kufikiri na uwezo wa kukariri.

Ubongo usiokuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri unapenda majibu mepesi.

Mfano unaweza kumwambia mtu mwenye akili ya kutosha kuwa, kuiba sio vizuri kwa sababu kuna matokeo mabaya kama kufungwa, kupigwa n.k na akakuelewa,

Ila mjinga ni lazima umuogopeshe kuwa kuiba ni dhambi, hivyo hataiba kwa kuhofia anatenda dhambi.

Hivyo ni rahisi sana kumuaminisha mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri kuwa kuna nguvu isiyoonekana na akaamini.

Sababu nyinginezo ni kama
  • Kurithishwa utamaduni, pale mtoto anapozaliwa analazimishwa aamini imani ya wazazi kwa kubatizwa n.k
  • Woga, watu wengi wanaogopa kutokana na vitisho mbalimbali mfano kutengwa kwenye jamii zao
  • Kifo, wengi hawakubaliani na ukweli kwamba ni lazima kiumbe hai afe, hivyo wanatamani wapate maisha mengine baada ya kifo.
  • Majibu ya kisayansi hayafariji kama ya kidini n.k.
GEITA:
Mwanamke aliyefariki mwaka 2020 'KWA KUGONGWA NA GARI' (Na kufia pale pale), amepatikana mwaka huu 2024 akiwa hai.


Tumia ubongo wako kufikiri kisha tuelezee hii scerio kisayansi or however.
 
Mzee usikariri, eti kufikiria tofauti, kivipi??unafikiriaje tofauti?? Unadhani kila mtu anayeamini katika mungu ni mwoga wa moto?? Au ana hofu ya neno liitwalo "dhambi"?? some of us tushawahi kuwa atheists na bado tukarudi kuamini katika mungu, USIKARIRI MZEE.
Ukweli ni ukweli tuu haijalishi unauma au la
 
Mungu ana akili sana.

Ulimwengu wa Roho hauwezi kuuingia kwa kutumia mbinu za kimwili. Imani (ambayo huonekana ujinga kwa waliojaa 'hekima, uwezo wa kufikiri) ndio kianzio. Ukijishusha, ukasema 'Naamini', ndio unaanza kuona hadi maono wazi wazi.

Rejea andiko hili:

”bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;“
‭‭1 Kor‬ ‭1‬:‭27‬ ‭SUV‬‬
Vinamsaidia nini sasa hivyo vitu?
 
Back
Top Bottom