Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Hapo kuna Rais na kuna Ikulu, ni kweli makazi ya rais ni ikulu ila kwa nini tufikiri kuwa isipokuwepo ikulu na uwepo wa rais unapotea?
Kwasababu, nimekuuliza wewe raisi yuko wapi? Ukaniambia nenda ikulu utamkuta(kumbuka hapa mimi nilishaukataa uwepo wa huyo raisi ) okay! Ili kuthibitsha maneno yako Nikatumia gharama zangu kufika huko ikulu, sasa, sijaikuta na hiyo ikulu, raisi nitamkuta? , labda tutumie huu mfano, umeambiwa, samia hassan suluhu ni raisi wa tanzania let say wewe upo Mexico ukamuuliza huyo mtu tanzania ilipo akakuelekeza njia ya kufika lakini hata hiyo tanzania kumbe haipo je huyo raisi wa tanzania atakuwepo?
 
Unachanganya mambo mkuu.

Kilichozungumziwa ni makazi ya Rais ambayo ni ikulu na si nchi, Mungu ambaye inaaminiwa kuumba huu ulimwengu tuliyopo ndio tunazungumzia hayo makazi yake ambayo inaaminika ni mbinguni.

Sasa ukienda ikulu na usimkute rais hiyo haina maana hakuna huyo rais au kama hakuna ikulu pia hatuwezi kusema hiyo nchi haina rais.
 
Nimekuelewa mkuu ,Mungu wa kwenye dini na vitabu vyake hayupo kutokana na mkanganyiko ,tumegundua ni story tu za watu.

Ebu tufafanulie kidgo dhana ya Mungu njee ya dini .
 
Nimekuelewa mkuu ,Mungu wa kwenye dini na vitabu vyake hayupo kutokana na mkanganyiko ,tumegundua ni story tu za watu.

Ebu tufafanulie kidgo dhana ya Mungu njee ya dini .
Umenielewa vibaya tu mkuu wala sijakusudia hivyo ulivyoelewa.
 
Umenielewa vibaya tu mkuu wala sijakusudia hivyo ulivyoelewa.
Wewe ndio umeelewa vibaya , mimi namaanisha Mungu hayupo kwel kulingna na dini

Ila ningependa kusikia Sifa za Mungu njee ya dini.
 
Wewe ndio umeelewa vibaya , mimi namaanisha Mungu hayupo kwel kulingna na dini

Ila ningependa kusikia Sifa za Mungu njee ya dini.
Mimi hapa najaribu kuelewa hizo hoja au madai ya kupinga dhana ya uwepo wa Mungu. Wenye kuamini Mungu nje ya dini wataeleza sifa za Mungu nje ya dini.
 
Mimi hapa najaribu kuelewa hizo hoja au madai ya kupinga dhana ya uwepo wa Mungu. Wenye kuamini Mungu nje ya dini wataeleza sifa za Mungu nje ya dini.
Haya mambo ni imani tu ila kiuhalisia hayapo , Mungu anakuwepo kichwani kwa anae amini tu .
 
Sasa hao waislam unaona wanatumia akili vizuri.
Hao wazungu wameleta dini kutushika akili tu.
Uliwahi kujiuliza kama tusingetawaliwa hizi dini zisingekuwepo!

kweli ukiwa mtoto unadanganywa vitu vingi lengo usivisahahu na kuviacha ndicho wanachofanya hao Waislam huko chuo.(madrasa).

Ebu niambie kama watu wasipotumia akili tukategemea miujiza tunaweza kukabiliana na changamoto za maisha kweli? Njaa, magonjwa, kazi ngumu, n.k.

Anyway kila mtu aamini anacho amini lakini msiache kutumia akili kwa mambo ya kawaida.
 
Uhalisia ni kitu ambacho ni cha kweli na kilichopo kweli .
Ndio nimeuliza uhalisia ni upi katika hili suala la imani ya uwepo wa Mungu au ndio utaniambia tu hakuna uthibitisho wa kuwepo Mungu basi?
 
Angalia dunia.angalia mifumo ya dunia.kila kitu kimeundwa kwa ustadi mkubwa.Mungu aliona watu watahitaji maji akaweka mifumo ya mvua.akaona binadamu wake wanahitaji chakula na hewa safi akaleta mimea.kila kitu kimewekwa kwa ustadi mkubwa kwahiyo hauhitaji degree kuona uwepo wa Mungu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Ndio nimeuliza uhalisia ni upi katika hili suala la imani ya uwepo wa Mungu au ndio utaniambia tu hakuna uthibitisho wa kuwepo Mungu basi?
Uhalisia ni kuwa Mungu hayupo , ni kujifariji tu kutokana na akili ya binadamu kuwa na tamaa ya kuendelea kuishi.
 
Uhalisia ni kuwa Mungu hayupo , ni kujifariji tu kutokana na akili ya binadamu kuwa na tamaa ya kuendelea kuishi.
Unaishia kusema hilo neno uhalisia ila hauonyeshi ni upi huo uhalisia wenyewe katika hili, Mungu hayupo kwa sababu wewe umesema tu au kwa sababu umezaliwa na kukuta huo msimamo wa kupinga kuwepo kwa Mungu? Hebu elezea mkuu.
 
Kujadili uwepo wake au kuto kuwepo kwake inaonyesha tu Mungu hayupo .

Yani ni sawa na tuanze sasa ivi kumjadili mama samia yupo ana hayupo , tutaonekana wehu.

Mwenye madai ya uwepo wa Mungu ndio waliozalisha wapingaji wa huo uwepo kwa vigezo mbalimbali ,kwanzia kwenye maandiko yao na sifa za Mungu zinavyopingana na dhana mblimbal , hasa ya uweza wa yote.
 
Hilo la watoto kufa liko kwenye biblia 1yohana 5:19. Panaposema :-Tunajua tunatokana na Mungu, lakini ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu.
 
Hilo la watoto kufa liko kwenye biblia 1yohana 5:19. Panaposema :-Tunajua tunatokana na Mungu, lakini ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu.
Ulimwengu ulioumbwa na Mungu Mkamilifu unakaaje katika nguvu za huyo muovu?

Huoni kwamba Mungu huyo ni mdhaifu sana kwa kuruhusu ulimwengu alioumba mwenyewe kukaliwa na huyo muovu?
 
kila atheist anakuwa muumini pale tu anapokuwa katika mazingira yenye hati hati ya kutoa uhai wake .
 
Hapo ndio kwenye tatizo kwa wengi wenu, suala la uwepo wa Mungu ni suala la imani hivyo si ajabu kuwa na mjadala kwa wanaoamini na wasioamini. Na ndio maana katika kipindi chote hiki kumekuwa na wakana Mungu ambao wamekuja kuwa waamini uwepo wa Mungu na waamini Mungu ambao wamekuja kuwa wakana Mungu.

Lakini pia kumeshawahi kuwa na mjadala wa Marehemu Rais Magufuli, kulikuwa na mabishano kuwa yupo hai au hayupo hai ila mwishoni ikajulikana amefariki lakini pia juzi kati tu ukaja tena mjadala kuhusu Makamu wa rais Dr Mpango ila napo pia ikajulikana yupo hai hajafa, kwahiyo mijadala si ajabu.

Sasa kama hii imani ya uwepo wa Mungu si ya kweli basi kwa sasa tukubali kumekosekana hoja za msingi za kuifuta hiyo imani kwa kudhihirisha kutokuwepo kwa Mungu kama wanavyoamini watu.
 
H
Hakuna haja ya kuifuta hiyo imani kwa sababu kila mtu ana haki ya kuamini anachokiamini

Issue inakuja pale wenywe hizi imani kuhukumu wengine na hata kutoa tathimini ya kila jambo kwa kila mtu kupitia hizi imani , watu wa hizi imani hawatambui kama ni imani tu , na sio mahakama ya kuhukumu kila kitu kwa kila mtu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…