GE2025 Watu Wasitengeneze Videos! Ukweli Ni Huu - Samia Alipogoma Kutoka ukumbini

GE2025 Watu Wasitengeneze Videos! Ukweli Ni Huu - Samia Alipogoma Kutoka ukumbini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mama Samia alikuwa anamalizia kwa mujibu wa katiba sasa ndio anaanza awamu yake hivyo tumuombee kwa.Mungu amalize miaka yake 10 hadi 2035
Inayomaliziwa ni awamu ya sita na sio ya Tano kwahiyo hiyo anayoanza ya kwake ni awamu gani??????

Mnachekesha kweli kweli
 
Yes ndio afuate utaratibu maana yeye mwenyewe anajichanganya utawala wa kurithi kuita awamu ya sita, wakati ni awamu ya tano, akichagulia ndio itakuwa awamu ya sita.
Yaani hata sijui kama somo la uraia huko mashuleni lipo wanafunzi watafundishwaje maana wanasiasa wenyewe wanachanganya mambo. Raisi wa awamu ya sita kuongoza kwa miaka 4 na sijui hii anayogombea itaitwa ya ngapi sasa
 
😄 🤣

Mtihani mkubwa
 
Mama Samia alikuwa anamalizia kwa mujibu wa katiba sasa ndio anaanza awamu yake hivyo tumuombee kwa.Mungu amalize miaka yake 10 hadi 2035
Safi sana watu wapo busy na Simba na yanga 2035 anafika huyu mama na ikifika 2040 tutakuwa sawa na Congo na Burundi.
 
Mama Samia alikuwa anamalizia kwa mujibu wa katiba sasa ndio anaanza awamu yake hivyo tumuombee kwa.Mungu amalize miaka yake 10 hadi 2035
Watu kama nyie ndio mnataka azikwe mapema.

Mpaka sasa moyonwake unawaka moto, amekimbilia Kizimkazi kupumua.

Nyie mmeshapewa baisklei mnabweka tu.

Imagine, kwa joto hili miaka ijayo mbele
 
Yes ndio afuate utaratibu maana yeye mwenyewe anajichanganya utawala wa kurithi kuita awamu ya sita, wakati ni awamu ya tano, akichagulia ndio itakuwa awamu ya sita.
awamu ni nini?

na definition hii ya awamu eleza unaitoa wapi, tukaiangalie
 
Mama Samia alikuwa anamalizia kwa mujibu wa katiba sasa ndio anaanza awamu yake hivyo tumuombee kwa.Mungu amalize miaka yake 10 hadi 2035

..ulilenga kumsaidia lakini umemharibia.

..kama anaanza miaka yake 10 inabidi ushindani ndani ya Ccm uruhusiwe.

..kwa maana nyingine Samia na wengine wanatakiwa waruhusiwe kuchukua fomu kama ilivyokuwa 2015 wakati wa Lowassa, Magufuli, Sumaye, Migiro, Makamba, Muhongo, Kigwangala, nk.

..Sasa kwa akili za kawaida unadhani Samia anataka au anaweza kushindana?
 
Utaratibu baada miaka mitano uwa wanamuacha amalize miaka 10.

Jpm miaka yake mitano ya mwanzo alishindanishwa na Lowasa, Membe na wengine.

Samia miaka minne alirithi kutoka kwa JPM, sasa kama alitaka kugombea ya kwake alitakiwa kufuata utaratibu kama JPM alivyoshindanishwa na hakina Lowassa, Membe.
Na hii ndio main issue ya Balozi HP. She is running for the first time lazima ashindanishwe….
 
Utaratibu baada miaka mitano uwa wanamuacha amalize miaka 10.

Jpm miaka yake mitano ya mwanzo alishindanishwa na Lowasa, Membe na wengine.

Samia miaka minne alirithi kutoka kwa JPM, sasa kama alitaka kugombea ya kwake alitakiwa kufuata utaratibu kama JPM alivyoshindanishwa na hakina Lowassa, Membe.
Umejibu sahihi sana
 
Anaanza awamu yake nani kamchagua? mbona unafikiria kwa kutumia sehemu za siri.
Tulipoingia mfumo wa vyama vingi 1992, suala lililowasumbua sana watawala ilikuwa nafasi ya Makamu wa Rais.
Huko nyuma Makamu wa Rais, alikuwa ni Rais wa Zanzibar automatically hata ikiwa Rais anatokea Tanganyika./Zanzibar. Japo anaweza kutokea to kuitwa Makamu wa Rais wa pili kutegemea na sehemu anayotoka Rais.
Mfano mwaka 1985 alipoondoka Mwl. Nyerere na kuingia Mzee Mwinyi, alimteua Mzee Warioba kuwa Waziri mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais na awamu yake ya pili walitokea Mzee Malecela na Mzee Msuya.
Hawa watatu mpaka kesho ndio watu pekee waliowahi kushika nafasi ya umakamu wa kwanza chini ya mfumo wa chama kimoja.
Tulipoingia mfumo wa vyama vingi 1992, iliibuka hoja tatanishi kuwa, ikitokea Rais aliyeshinda urais wa Jamhuri ya Muungano akatokea chama X na kule Zanzibar akashinda wa chama Z, itakuwaje.
Ndipo ikabidi watafute njia mbadala, kwa kuazima sehemu ndogo ya katiba ya Marekani sasa walichukua kiasi gani sijui,japo humu ndani wamo wabobezi wa sheria wanaweza kutusaidia.
Sasa kipengele hicho kinasema,ikiwa mgombea urais akitokea Bara basi Makamu lazima atokee Zanzibar.
Najua wakati huo, ilileta shida haswa huko Zanzibar kwa kudai ni kama hadhi ya Rais wa Zanzibar imeshuka.
Na hii ilianza 1995 wakati huo aliyeshinda alikuwa alikuwa Mzee Benjamin Mkapa na Makamu wake Dr Omar Juma..
Na ilisomeka Makamu wa Rais ni Rais, mtarajiwa wakati wowote ikitokea Rais aliyeko Madarakani hawezi kuendelea na majukumu kwa sababu zozote kulingana na vigezo vilivyowekwa na Katiba. Hivyo ndio sababu alipofariki JPM hatukuihitaji kumpigia kura Mama Samia kwani zile kura walizopata 2020 zilikuwa zao wote.
Japo kulingana na Humphrey Polelpole, najua walifanya uchaguzi kimazoea kuwa JPM atamaliza kipindi chake kama alivyonusurika Kikwete kwa kumpendekeza Dr. Bilali ili kumsaidia Dr. Shein 2010 kuendelea na awamu ya pili ya urais Zanzibar.
Sijui kama Mzee Kikwete alifikiria au aliwaza nini kama kilichomtokea Magufuli kingetokea kipindi chake.
Sasa kujazia hoja yako ni hivi huyu mama ni Rais toka 2015 kwani Ccm walimuona ana vigezo vyote vinavyohitajika vya kuwa Rais wa JMT, napata shida mioyoni mwao pamoja na kina Kikwete ambao inawezekana walikuwa sehemu ya huu mchezo hatari haswa ukiziingatia alivyochukulia poa alipompendkeza Dr. Bilali mgombea mwenza wake,ili tu kufanya siasa za Zanzibar zitulie bila kujiuliza huyu anayehofiwa Zanzibar angeweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa JMT na Zanzibar ikiwa chini yake Alipopendekezwa Mama Samia na JPM na wakachaguliwa hapo tayari alikuwa ni Rais anayesubiri kuapishwa ikitokea sababu zozote za Rais aliyeko Madarakani kushindwa kuendelea na majukumu yake kwa sababu zilizoainishwa kwenye Katiba.
Namalizia kwa kusema Polepole yuko sahihi, hii ni awamu ya tano na siyo ya sita. hivyo tulihitaji uchaguzi mpya na wagombea wapya kuianza awamu ya sita.

.
 
Uzito wa haya mambo mazito ni uzito mkubwa. Magu katumia neno "kwa kanuni zetu...", Lusinde katumia neno " kwa kanuni zetu....", Samia naye katumia neno "kwa kanuni zetu". Cha ajabu wote watatu wamefanya matendo tofauti. Hizo kanuni wanazosema zao zitakuwa na shida.
 
Kwenye chama chake tu mtu hajataka kufuata taratibu kwakuwa anaogopa ushindani, jiulize kuhusu ushindani wa nje dhidi ya vyama vya upinzani itakuwaje?​
 
Back
Top Bottom