Shetwani lazima atajwe!
Kwa nini asitajwe sasa!
Ile "desire" ama "lust" to kill utaipataje bila ushawishi wa kaka ibilisi?
Tena akiweka ushawishi wake "maridhawa" hadi utasahau na kuziba mianya ya kufikiwa kirahisi kukamatwa kwako!
Inakuwa kama umevuliwa nguo na mwanamke uliyemhonga hadi kukufirisi, leo kwanza ndiyo umempata!
Unamkabili huku ukitetemeka na udenda ukikuchuruzika, akili zimezibwa na pazia kwa muda, hauoni mbali wala hausikii, tena bila kujali kuna maradhi na kifo, wewe unajisunda kavu kavu tu.
Akili zitakurudia baadaye ukishatenda, tena wakati huo umeshakwenda na maji kudadadeki!
Hapo shetwani anakuwa keshawajibika na kukuachia upambane na hali yako.