Watu wazima 25+: Ukiachana na kufiwa, ni TUKIO gani kubwa liliwahi kukutoa machozi hadharani 😭

Watu wazima 25+: Ukiachana na kufiwa, ni TUKIO gani kubwa liliwahi kukutoa machozi hadharani 😭

Wewe mie sipendi kuumwa 🤣

Kwani sindano nachomewa hadharani? Hata siogopagi
Pale doctor anapakapaka spirit tako mara apige pige sindano kuiweka vizuri...

Akichomeka tu kilio hiko...

Najua bado mtoto ila kwa umri huu kipi kinakuliza hadharani kwa sasa...
 
Pale doctor anapakapaka spirit ile mara apige pige sindano kuiweka vizuri...

Akichomeka tu kilio hiko...

Najua bado mtoto ila kwa umri huu kipi kinakuliza hadharani kwa sasa...
Sijawahi kuogopa sindano… mimi naogopa ile hali ya kuumwa tu.


Huu umri wa early 30 bado ni kuumwa, machozi yanaweza nilenga hosp.
 
Sijawahi kuogopa sindano… mimi naogopa ile hali ya kuumwa tu.


Huu umri wa early 30 bado ni kuumwa, machozi yanaweza nilenga hosp.
Sababu unapenda kudekezwa na kuonewa huruma ukiwa unaumwa ndiyo maana unalialia...
 
Mwaka 2014 nilipata breakdown ya gari mlima kitonga, ilikuwa ni mida ya jioni na kwa kuwa pale pana vibaka , nikashauriwa nitafute mwenyeji kwa ajili ya ulinzi . Nilimoata jamaa , kuitwa 'Tizo' akanisaidia usiku kucha na kutwa nzima kwa ulinzi na supports kadhaa , katika story alinisimulia mengi sana , jamaa alikuwa yatima na maisha magumu kupita kiasi na nikagundua 'Tizo ' ni kifupisho cha matatizo, na ndo lilikuwa jina lake halisi.
Baada ya breakdown kuisha niliachana naye na kumpatia stahiki yake , nikamatia nguo kadhaa na viatu kadhaa nikaondoka zangu , nilifanya hivi kwa miaka kadhaa mbele kila nilipokuwa nafasi na kupita eneo hilo maana hakuwa mbali na barabara ,baadaye tukapotezana ,
Nimekuja kumuona mwaka 2020 , baada ya kuanza kupita tena njia hiyo , kumuangalia vizuri hana mkono wa kulia , yani umekatika kwenye bega kabisa , namuuliza Tizo mkono umefanyaje tena akaniambia alianguka kwenye lori wakati anauza mahindi ya kuchoma ,akateleza na kukanyagwa na tairi , mkono, ulikuwa wa kupona ila hakukuwa na pesa ya matibabu hadi ulipoanza kuoza ndo ukakatwa.
Nilishindwa kujizuia kutoa chozi!
 
Back
Top Bottom