Mwaka 2014 nilipata breakdown ya gari mlima kitonga, ilikuwa ni mida ya jioni na kwa kuwa pale pana vibaka , nikashauriwa nitafute mwenyeji kwa ajili ya ulinzi . Nilimoata jamaa , kuitwa 'Tizo' akanisaidia usiku kucha na kutwa nzima kwa ulinzi na supports kadhaa , katika story alinisimulia mengi sana , jamaa alikuwa yatima na maisha magumu kupita kiasi na nikagundua 'Tizo ' ni kifupisho cha matatizo, na ndo lilikuwa jina lake halisi.
Baada ya breakdown kuisha niliachana naye na kumpatia stahiki yake , nikamatia nguo kadhaa na viatu kadhaa nikaondoka zangu , nilifanya hivi kwa miaka kadhaa mbele kila nilipokuwa nafasi na kupita eneo hilo maana hakuwa mbali na barabara ,baadaye tukapotezana ,
Nimekuja kumuona mwaka 2020 , baada ya kuanza kupita tena njia hiyo , kumuangalia vizuri hana mkono wa kulia , yani umekatika kwenye bega kabisa , namuuliza Tizo mkono umefanyaje tena akaniambia alianguka kwenye lori wakati anauza mahindi ya kuchoma ,akateleza na kukanyagwa na tairi , mkono, ulikuwa wa kupona ila hakukuwa na pesa ya matibabu hadi ulipoanza kuoza ndo ukakatwa.
Nilishindwa kujizuia kutoa chozi!