Watu Wazima, Mnaowalaumu Vijana Kwa (UTOTO)

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Kwenu watu Wazima, Mnaowalaumu vijana Kwa Utoto

Kuna (baadhi) ya watu wazima
wale ambao umri umeenda, wamekuwa na tabia ya kuzodoa vijana wadogo au watu ambao bado hawajafikia umri wao

Utasikia:👇

Yaani huyu utoto unamsumbua
Huyu ana utoto mwingi
Hajitambui
Na maneno mengine mengi sana

Lakini mara nyingi ni kulaumu tu bila kutoa suluhisho🙌

Kuna mtu fulani ni mtu mzima ambaye tulikuwa na jambo tunalifanya pamoja
Sasa kuna mambo yalitokea kutokana na namna ambavyo mimi nilivyoreact

Akaamua kuchukia na kususa

Baadaye mimi nikajishusha nikamtafuta, hasa baada ya kugundua kwamba nilikosea

Lakini nilipomtafuta, akaanza lawama
Ujue Shes una utoto sana
Pale ulifanya utoto

Sawa, inawezekana nilifanya utoto It’s okay

Lakini wewe ambaye ni mtu mzima, si ulitakiwa kuonesha ukomavu wako?

Si ulitakiwa kunishauri, kunielekeza na kunionesha nilipokosea badala ya kuishia kusema tu kwamba nina utoto?

Nilimuuliza swali moja:👇

Wewe kipindi ukiwa na umri kama wangu, ulikuwa na maarifa sawa na uliyonayo leo?
Ulikuwa na upeo wa mambo kwa kiasi ulicho nacho sasa?

Akasema hapana

Nikamuambia, kama wakati huo hukuwa na maarifa na upeo ulio nao leo, kwa nini sasa unawalaumu wengine ambao bado wako kwenye hatua ya kujifunza?(japo nahisi hakupenda haya maneno)

Na ujue kosa siyo kulaumu
Shida ni kulaumu bila hata kutoa suluhisho laumu ndiyo ukimaliza toa ushauri nini kifanyike

Nyie baadhi yenu watu wazima mliomo humu JF Forums ambao mna tabia ya kulalamikia vijana kwamba wana utoto nashauri msiishie kulalamika tu

Wapeni na elimu pia hao vijana
Waambieni wamekosea wapi
Waonesheni walitakiwa kufanya nini
Washaurini namna ya kujirekebisha

Kwa sababu kuwa mtu mzima siyo kuwa na miaka mingi tu
Kuna pia suala la ukomavu wa kufikiri na namna unavyomsaidia mtu ambaye bado anajifunza

Ni namna gani ya kujituliza sehemu ya kujituliza
Kuongea sehemu ya kuongea
Kunyamaza sehemu ya kunyamaza

Na kama tayari umemshauri ukamuelekeza, ukamueleza kosa lake na akashindwa kubadilika hapo sasa labda siyo tena utoto ni jeuri na kiburi na tayari hapo umefanya wajibu wako badala ya kulalama tu

Sasa wewe mtu mzima ambaye unajiona una maarifa makubwa
Baada ya kumaliza kulaumu na kulalama jiulize sasa

Huyo kijana unaedai ana utoto na ujinga umemsaidia kuelewa kosa lake au umeishia kumlaumu tu?

Swali la Mjadala

Je, ni sawa kwa watu wazima kuishia kuwalalamikia vijana kwamba wana utoto ujana bila kuwapa mwongozo ushauri au elimu ya kuwasaidia kukua na kuwa watu wenye maarifa zaidi? wenyewe wanaita Gnz

NB:Sisemi nawafundisha
Nauliza tu, kwa ajili ya mjadala 🙏

ShesRise_1 ✋️
 
✍️✍️
 
Watoto wanapaswa kuwa na utoto. Hilo linatarajiwa.

Unawezaje kushangaa kinyeo kunuka mafi?

Mimi nadhani kila mtu aishi vile iwezekanavyo.

Kulazimisha watoto wawe na utu uzima ni makosa.

Mtoto lazima awe mtoto, na mkubwa awe mkubwa.

Usilazimishe kuvaa chupi kichwani. Chupi ni kizibo cha mbunye.

TUMSIFU YESU KRISTO, MILELE AMINA.
 
Kwanza hongera kwa mada nzuri

Si sahihi kwa watu wazima kulaumu tu vijana badala ya kuwaonyesha wapi pa kuaanzia au kupitia

Maana lawama bila kuonyesha makosa yao,ina maana kesho watarudia tena kufanya jambo lile lile,na hapo utawaona vijana ni wajeuri au hawajielewi kwakuwa watazidi kufanya makosa yale yale

Kwahiyo kama watu wazima tuna jukumu la kuwaelimisha vijana na kuwapa muongozo wa nini cha kufanya na kipi si kufanya
 
Dah hii mifano yako imeniacha hoi 😅😅
Chupi ni kizibo cha mbunye 😮
 
Kwanza hongera kwa mada nzuri

Si sahihi kwa watu wazima kulaumu tu vijana badala ya kuwaonyesha wapi pa kuaanzia au kupitia

Maana lawama bila kuonyesha makosa yao,ina maana kesho watarudia tena kufanya jambo lile lile,na hapo utawaona vijana ni wajeuri au hawajielewi kwakuwa watazidi kufanya makosa yale yale

Kwahiyo kama watu wazima tuna jukumu la kuwaelimisha vijana na kuwapa muongozo wa nini cha kufanya na kipi si kufanya
Shukran 🙏

Wewe miongoni mwa watu wazima wenye maarifa makubwa 👏

Asante kwa maoni na karibu tena
 
Kuanzia leo jukumu la kumlea Marry Diana tumekupa ww ShesRise_1

Ndio uone kwa vitendo sasa kuwa kijana ukijifanya mjuaji mtu mzima anakaa pembeni kuona unavyofanya.

Ulitumia busara kumrudia, vijana wengne wasingerudi. Ila ulivyorudi si umeona amekuambia ushaur wake kwenye hilo jambo?.
Japo alikosea pia kukunanga kuwa utoto unakusumbua.

Kijana akikosea unamuambia, akikataa ushauri unamwambia hebu fanya unavyoona ni sahihi, ila ukikwama au kuhitaj mawazo mbadala niambie.

Na sio kulazimisha atumie njia/mawazo yako moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom