Watu Wazima, Mnaowalaumu Vijana Kwa (UTOTO)

Kuanzia leo jukumu la kumlea Marry Diana tumekupa ww ShesRise_1
Mkuu naogopa mimi kulea mtu 🙏 Hakika ushauri ni bure kuufanyia kazi ushauri uliotoa sio juu yako tena
Ni mhusika mwenyewe
 
Hata watoto huwa wanatofautiana, hivyohivyo na watu wazima. Kuna watoto wana utoto mwingi na kuna wengine wana utoto wa kawaida. Kuna mtu anaweza kukosea kwa kutokujua wewe unayemtazama unamsamehe tu kwa sababu unajua ni utoto ila kuna wale wanaoamua kabisa kufanya utoto kwa sababu ni wanaamini ni watoto na wanataka uwachukulie hivyo. Watu wote wa aina mbili huwa kama sina ulazima wa kujihusiaha nao naamua kukaa nao mbali hasa huyo wa pili
 
Aisee hiyo kufanya kitu kwa mgongo wakusema ooh mimi mtoto watanielewa huo si utoto tena ni kijana anaejielewa vizuri mwenye tabia mbaya
 
Mimi nina perspective nyingine pia..

Gen z wengi wanaishi maisha ya mitandao..

Kipindi nakuwa hukukuwa na haja ya mzazi kukujuza namna ya kuact, yaani just by observing maisha yake na wakubwa zako, unaji kuta tu automatically sio mbishi mbishi.. Na hata ukisolewa ilikuwa unakuwa sharp kupick up ulipokosea maana hakujua na sehemu ya kulinganisha maisha kama zilivyo social media nyingi..

Ni kweli wazazi wengi hawajui namna ya kuwafundisha namna bora ya kuwaelekeza maana hata wao hawakuelekezwa Wali pick up kutoka kwa wazazi wao pia. Ila leo hata mzazi wa miaka 50 nae anataka alee mtoto kizungu.
 
Kwa mambo yalivyo sasa uwazi wa mambo ifike muda tuache kulaumu wazazi kwa kila kitu
Wazazi wana nafasi yao katika malezi tena kubwa wao ndiyo hujenga msingi wa maisha yako

Lakini kuna umri ukifika huwezi kuendelea kuishi kwa kanuni za zamani hasa kama zilikua sio kanuni chanya kwako

Exp: kuna waliolelewa vijijini unakuta mtoto anajua kupika kwa namna ile walioyokua wakitumia home kijijini
Kitunguu nyanya maji kibao chuzii bahari

Lakini leo kakua kakutana na upishi tofauti hawezi kuang'ang'ania vile vile vya nyumbani kwao

Kwa kua viungo vipo vingi na vinapatikana kwa urahisi
Anaamua kujifunza na kua hodari jikoni licha ya kua hakujifunza nyumbani au hakufunzwa

Ukiona unafikia hatua ya wewe mwenyewe kulaumu wazazi ujue wewe tayari unajitambua
Hilo tu la kundua wazazi wako walikosea ni ishara tosha wewe sasa unajitambua kazi kwako kuchukua hatua na kubadilika

Unasema mitandao sijui vijana kujilinganisha
Kwanini usijilinganishe kwa positive?
 
Mimi navyoona mitandaoni kuna asilimia ndogo sana ya mtoto kupata maadili...

Ni asilimia ndogo sana ya content za mitandaoni huwa zinakuwa positive, let alone zile ambazo zinakuwa trending..

So naona kama social media huwa na negative impact kuliko malezi bora physical ya wazazi... Lakini pia ili kitu kimake mtu inahitajika repetition ambayo hawezi kuipata kwa scrolling mitandaoni

Japo poa ukiwa discipned mitandao una hazina kubwa pia
 
Sawa mkuu asante kwa maoni
 
Vijana wenyewe mmevurugwa siku hizi hata ukiambiwa kitu cha busara unabisha mnaishi na social media.
 
Vijana wenyewe mmevurugwa siku hizi hata ukiambiwa kitu cha busara unabisha mnaishi na social media.
Hapana siyo wote wamevurugwa
baadhi wako hivyo kwa kukosa ushauri wenu

Mi naona kushauri tushaurini tu bila kujali kama ushauri utafatwa au lah!
 
Ulikua hujui kama wao kukosolewa ni mwiko hawataki kabisa
Sijui shida ni nini?
Shida ni taboo / Abomination kukosoa wazazi.

Cha ajabu huku makazini unaweza kukuta mzazi wako anapokea mfokeo au maelekezo kutoka kwa kijana.
 
Shida ni taboo / Abomination kukosoa wazazi.

Cha ajabu huku makazini unaweza kukuta mzazi wako anapokea mfokeo au maelekezo kutoka kwa kijana.
Mimi naona ni sawa mzazi kukosolewa
Kwa sababu pamoja na kua mzazi ni mtu mwenye umri mkubwa na huenda anajua vingi kukuzidi
Lakini hawezi kujua kila kitu
Sema tu inatakiwa namna nzuri ya kumkosoa bila kumvunjia heshima

Japo kuna dhana mzazi hakosei na kama hakosei basi hawezi kukosolewa(umeona hapo)
 
my dearest auntie, kwa viungo vyangu vyote, niinaunga mkono hoja hii kwa sababu for a fact ni rahisi sana kumwambia kijana X “una utoto mwingi sana”, lakini issue hapo siyo tu kumwambia dogolas una utoto mwingi ila kilicho na thamani zaidi ni kumwelezea barabara au kinagaubaga kwamba amekosea wapi, kwa nini nasema amekosea na afanye nini ili asirudie kosa hilo. Sasa huu utaratibu mazee wa mtu mzima anapomkosoa kijana bila kumwelekeza kwa ufasaha ili asirudie makosa, nadhani mara nyingi mtu mzima anakuwa amemhukumu huyu kijana X badala ya kumjenga. actually kila mtu aliwahi kuwa kijana na hakuna aliyezaliwa akiwa na hekima yote aliyonayo leo. Henceforth, kama sisi tulijifunza kupitia makosa na tukarekebishwa aidha kwa maneno makavu au bakora za kibabe, basi ni wajibu wetu pia kuwasaidia wanaokuja nyuma yetu kujifunza. Issue inakuja kama mtu mzima umeelekeza, umeshauri, umeonya , umeadhibu na kijana X bado anaendelea kufanya makosa tena kwa makusudi, hihihihhiih bagoshaaa hapo ndipo unaweza kusema tatizo si tena kutokujua bali ni kutokutaka kubadilika plus ujeuri wa kipumbavu.

narusha mic kwa Mc
 
Wazazi wenye hekima na Busara huwa wanatulia na kujishusha kwenye aspects ambazo hawana uelewa nazo na huwa wanakubali kupokea maelekezo hata kutoka kwa watoto wao.
Shida mtoto unajulikana ni kilaza pro max halafu ujifanye unampa maelekezo au unamkosoa mzazi wako, hapo lazima mtagombana.
 
Umepigaje hapa 👇
Issue inakuja kama mtu mzima umeelekeza, umeshauri, umeonya , umeadhibu na kijana X bado anaendelea kufanya makosa tena kwa makusudi, hihihihhiih bagoshaaa hapo ndipo unaweza kusema tatizo si tena kutokujua bali ni kutokutaka kubadilika plus ujeuri wa kipumbavu 📌
 
Ila kuna ukweli ujue mtoto kama unaishi kwa heshima na utulivu ni rahisi mzazi kuchukua ushauri wako
Japo wazazi wengine hawataki kabisa kukosolewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…