African businesses
Member
- Feb 13, 2024
- 80
- 204
- Thread starter
- #41
Nimesoma ulichokiandika, nimekipokea ila nasikitika kukuambia sitokifanyia kazi, hapa anayeitaji kujielimisha ni wewe wala sio mimiNi afadhali
Ungeutumia muda wako kujiendeleza kielimu kuliko kuandika vitu usivyo na uelewa navyo.
Jambo pekee la.maana na la kweli uliloliandika ni pale tu uliposema kuwa uhai wa mwanadamu yeyote ni wenye thamani.
Mengine yote uliyoandika, inaonekana huna kabisa uelewa nayo. Jielimishe kwanza, utakuwa unaandika vitu vya maana na kuepuka aibu na fedheha.
Marekani unaiingiza bila ya uelewa. Kama una uwezo wa kutumia internet, tafuta movement ya Wayahudi waliokuwa nje ya eneo lao la asili, iliyoitwa Zionisim, ambayo ililenga kuwahamasisha wayahudi waliokuwa Ulaya kurudi kwenye ardhi ya baba na babu zao, na hiyo ni baada ya Hitler kuwaua kwa maelfu Wayahudi waliokuwa wakiishi Ujerumani. Na Ujerumani, wakati huo ilikuwa ndiyo nchi yenye wayahudi wengi kuliko nchi yoyote.
Lakini pia ufahamu kuwa katika hiyo nchi ya Canaan ya kale, kulikuwepo na Wayahudi ambao tangu enzi za babu wa babu zao hawakuwahi kuondoka kwenye ardhi yao, nao waliishi pamoja na waarabu ambao leo wanaitwa Wapalestina.
Mtu mwenye dhamrra njema, ni lazima ahamasishe Waisrael na Wapalestina waishi kwa pamoja kama walivyoishi hapo kale. Chanzo cha matatizo yote ni Waarabu wanafiki wanaochochea na kuanzisha makundi ya kigaidi wakiwadanganya wapalestina kuwa watawasaidia kuwaangamiza Wayahudi, na wao watawale ardhi yote ya Israel, Gaza na West Bank. Na shetani mkubwa kwenye hili ni Iran. Falsafa ya Iran ni kwamba Wayahudi hawatakiwi kuwepo Duniani bali wanatakiwa kuangamizwa wapotee. Na ndiyo falsafa ya magaidi ya hamas na Hezbollah. Bila ya hawa hayawani, Wayahudi na Wapalestina wangeweza kuishi pamoja. Fikiria hata wewe, mtu akuambie kuwa wewe na wanao na ndugu zako, hamtakiwi kuwepo Duniani, mnatakiwa mteketezwe, hivi utakuwa na mahusiano ya namna gani na jitu kama hilo? Haya mahayawani yenye itikadi hizo ndiyo chanzo kikubwa cha maafa ya Wapalestina na Wayahudi, ya kila mara. Bila ya Wapalestina kuachana na hawa Waarabu wanafiki, wakaweza kusogeleana na Wayahudi kama ndugu, basi kamwe hizi jamii mbili hazitaonja amani.
Sin chuki na wapelestina wala sina chuki na hao waisrael wa mchongo ila soon nitakuja na facts zilizoshiba nikuonyeshe kwamba hao unaodhani kua ni wayahudi sio wale waliotajwa kwenye bibilia