Watu wengi wa Dar es Salaam wanaishi maisha magumu mno

Watu wengi wa Dar es Salaam wanaishi maisha magumu mno

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Saa kumi usiku utashangaa kuona daladala ile kubwa Eacher imejaza watu na vifurushi vyao vya ujasiriamali.

Mwingine kabeba utumbo wa ng'ombe, mwingine, kiroba cha ndizi, mwingine box la dagaa wabichi, mwingine ana kiroba cha embe, mwingine kiroba cha tembele, mwingine mchicha.

Jamani wananchi wanateseka.
 
Kama ulikuwemo kwenye hiyo Eicher ina maana na wewe bado hali ni tete. Nakushauri pambana. Hiyo ni hali ya kawaida kwa hapa duniani.

Hakuna sehemu watu hawapambani. Ni kaburini tu ndo utapata utulivu. Kama ni mkristo soma MHUBIRI 9:10
 
Ndio dunia hiyo, nenda new york uone wamachika wa huko wanavyofanya, wanavaa makoti marefu kama yale ya FBI lakini mifuko ya makoti hayo imejaa bidhaa za kuuza utafikiri stoo ndo manake wanatembea kwa kudunda si kwamba wanaringa bali uzito wa vitu umewaelemea.

Ukienda India panda treni ka utapata nafasi hata kusogeza mkono na usiku watu wanalala mabarabarani kwani kuwa mitaa Serkiali inazuia magari yasipite ili walala hoi walale, nenda Nepal, Ufilipino yaaani kote. Labla nchi za scandinavia kama Norway, Denmark na kule Canada ndo watu wanaishi poa!!
 
Mtoa mada yupo sahihi ila uwasilishaji wake una walakini kidogo. Asilimia kubwa ya watu wa Dar tunatafuta msosi kwanza mengine baadae.

La muhimu japo sio la kuzingatia wengi tunatamani kurudi nyumbani ila changamoto ya kwanza ni nauli yote kuipata Kwa pamoja.

Changamoto ya pili ni huko nyumbani hatujui tutawaambia nini kuhusu muda mrefu tuliopoteza DSM na mifukoni hatuna kitu.

Itaendelea.
 
Huko hawangoji pakuche sijui wanalala saa ngapi!! Mtu anarudi saa Saba usiku home, saa tisa tena mzigoni
Anyway ni upambanaji wa mateso!!
Ccm wananchi hawana raha[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom