Watu wengi wa Kanda ya Ziwa sio wastaarabu wakati wa kula, wanatia kinyaa!

Watu wengi wa Kanda ya Ziwa sio wastaarabu wakati wa kula, wanatia kinyaa!

Kanda ya ziwa tuna taratibu zetu hata kwenye kula samaki kuna miongozo tuliyofundishwa tungali wadogo, hata ukataji wa kuku au uchunaji na ukataji wa nyama ya ng'ombe, mbuzi na kondoo sasa hayo unayoyasema labda ulikuwa kwa jamii yako yenye table manners za ajabu ajabu.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Ndo mpo hivyo, table manner kwenu mwiko!
 
Kama wameendelea kwenye uhuru na haki za binadam mbona wanawalazimisha wengine wafate tamaduni zao huoni ni kinyume na haki za binadam
Hakuna mtu aliyelazimishwa kukubali tamaduni.

Ghana wamepitisha sheria za kupinga ushoga wiki hii. Uganda wamepitisha.

Tatizo nyie mnataka misaada yao halafu hapo hapo mnajimwambafy kuwa hamtaki values zao za uhuru, kwa style ya "baniani mbaya, kiatu chake dawa".

Wakiwapiga chini kwenye misaada mnalialia kwamba mnalazimishwa kufuata values zao.

Ni weakness zenu wenyewe tu huko.
 
Hakuna mtu aliyelazimishwa kukubali tamaduni.

Ghana wamepitisha sheria za kupinga ushoga wiki hii. Uganda wamepitisha.

Tatizo nyie mnataka misaada yao halafu hapo hapo mnajimwambafy kuwa hamtaki values zao za uhuru, kwa style ya "baniani mbaya, kiatu chake dawa".

Wakiwapiga chini kwenye misaada mnalialia kwamba mnalazimishwa kufuata values zao.

Ni weakness zenu wenyewe tu huko.
Misaada inawasaidia watawala wananunulia mabus ,malori na Sio wananchi, wananchi wameachwa wapambane na hali zao
 
Watu wa vijijini na usafi ni mbalimbali...

Ukiwa kileji halafu ukaenda kwenye kilabu cha pombe ndio utaona namna watu wasivyojali kanuni za afya...

Pombe ikishawekwa mwenye kile kibaba, lile kombe linakuwa linazunguka kwa kila mtu kupiga funda...

Kuna mikoa pombe inawekwa kwenye ndoo, halafu wadau wanaizunguka na mirija ya kienyeji inayochuja machicha (imetengenezwa kwa mianzi myembamba)...
Observation ya muanzisha mada ina ukweli mwingi maana hata mimi nimeshayaona yote hayo huku Usukumani.

Ila, nadhani ni suala la sehemu nyingi nchini. Sidhani kama ni suala la kanda ya ziwa tu.

Na suala la usafi ni kwa nchi nzima. Fanya observation kila uendapo nchini utagundua kuwa suala la usafi ni changamoto kubwa kwa Watanzania.

Wewe unayejali usafi watakuona unajifanya una mambo ya Kizungu [whatever that is].

2016 nilikutana na mdada mmoja wa mjini. Akaniona natumia ‘hand sanitizer’ kusafishia mikono.

Kwa akili yake finyu akaona kuwa mimi nina mambo ya ‘Kizungu’ kwa kusafisha mikono na sanitizer.

Fast forward mpaka 2020 na mbele, matumizi ya sanitizer sasa ni jambo la kawaida kabisa katika sehemu nyingi tu nchini. Kwa mtazamo wake na akili yake finyu, si ajabu bado anaona matumizi ya sanitizer ni Uzungu.

Yaani mtu anahusisha usafi na Uzungu! Ni akili ya aina gani hiyo?

Kwa hiyo kwa ujumla, suala la usafi kwa Watanzania wengi ni kama vile ni jambo geni.

Kuna watu wanauthamini uchafu kuliko usafi.

Ni fikra duni sana.
 
Hiyo Cha mtoto, niliwahi kufika singida vijijini, ugali unapikwa kwenye chungu tena ni WA vidude Fulani vipo kama mtama mwembamba ,unga unasagiwa kwenye jiwe, unaliwa na mlenda usioungwa. Chungu kikitoka jikono hawapakui,

Wanawake ni marufuku kula sehemu Moja na wanaume, hivyo chungu kinapelekwa Moja kwa Moja kwa wanaume tena anakisogeza akiwabali. Wanaume watalia humo humo mpaka wakishiba makombo ndio wanawake wanakwenda kula.

Umesahau ile ya kunawa mikono kwenye chombo kimoja cha maji,daah disgusting.
 
Picha linaanza, nimeenda ukweni kanda ya ziwa kulipa mahari. Siku hiyo walichinja Ng'ombe na msosi ulikuwa wa kutosha. Muda wa kula nakumbuka sisi tuliwekwa sehemu moja na wenyeji wetu wawili ili tusiwe wapweke, daah walivyokuwa wanalamba vidole wale mabwana hadi nikaghairi kula. Wenyewe wanasema kuwa haitakiwi mkono ubaki na mabaki ya chakula, kwahiyo wanalamba mikono haswa ili kuisafisha huku wanaendelea kula, pia hawajui kula sehemu moja. Muda huu atamega tonge upande huu, ila tonge la pili litamegwa upande ule na tonge la tatu litamegwa katikati. Nikamtumia meseji waif afanye mchakato aniletee chakula cha peke yangu,kweli kikaletwa nikala. Japo maneo ya chichini yaliongeleka kuwa sipendi kula sahani moja na wenyeji.

Baada ya kuwa mwenyeji hii kanda kwa takribani miaka minne ndo nimegundua kuwa ile siku ya mahari haikuwa bahati mbaya, watu wengi huku kuanzia Simiyu, Shinyanga, Mwanza hadi mara wapo hivyo. Kukuta mtu anakula huku anajichokonoa meno kwa vidole mbele za watu ni kawaida, kula na kukibehulia chakula ni kawaida, kula huku analamba vidole vyote vitano ni kawaida sana, Kula chakula bila kuchagua upande ndo kabisa hawa jamaa ni mafundi, wanadonoa chakula kama kuku.Inatia hasira sana na inakera kushuhudia watu wa namna hii.

Angalau kidogo kwa waliosoma soma na wale wenye exposure ya kusafiri sehemu mbalimbali ndo wanaunafuu.

USHAURI:Wazazi wa kanda ya ziwa wafundisheni vijana wenu ustaarabu wakati wa kula.

Kuna mashemeji zangu walikuja kunitembelea ila nikawaambia waziwazi kuwa sipendi kumuona mtu anakula hovyo kama mbwa hapa nyumbani kwangu.Walienda kusimulia huko walipotoka kuwa nina roho mbaya ila mimi sijali.
Sisi watu wa kusini tulishaga staarabika Kitambo sana,hakuna mambo ya kushare kila mtu na sahani yake.
 
Si ungeenda moja kwa moja kwamba ni wasukuma? Ukisema kanda ya ziwa ujue unahusisha Wajita, Wakurya, Wahangaza, Wahaya, Wakerewe, Wazanaki, Wasukuma....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],Ngoja waje akina Ngosha wakutolee povu.
 
Sio sinia moja,kijiji kizima wanaleta mboga mboga na ugali halafu kuna mfalme wao.
Yalinikuta kijiji fulani,baada kulishwa milenda chukuchuku siku ya pili nikaona isiwe tabu
Agiza kuku 2 zichinjwe ntalipa.
Zikachinjwa chomwa.
Nikajua ntakula nusu aah wapi.
Kakabidhiwa king wao kuku wote.
Ananyofoa kinyama anawapa.
Wanapasiana.
Niliambulia kibawa
Tena wakasema amekuheshimu sana.
Kuku wangu mwenyewe mnampa mtu anigawie.
Nilinuna mpk basi

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Dah kuna boss mkubwa tuu ila anavyotafuna jamani mpk aibu...yani anaongea na machakula mdomoni mpk kero...ni msukuma og...wasukuma waliosoma seminar wakapata mafunzo ya kule hawapo hivyo..seminar inawashep watu
 
Pana Lile kabila ugali wa moto unaliwa kwenye sufuria kubwa pamoja na sufuria ya mboga Kama camp hivi.
Ukikata tonge ukaachia kisa unaungua mwenzako anapita na tonge lako wao mikono Yao imekomaa.
Usipokuwa makini utaambulia maji ya kunawa tu
Kuna ule ugali wa kwenye chungu wamoto muda wote watu wanakula wewe kila ukigusa wamoto unashtuka msosi umeshaisha
 
Back
Top Bottom