Ila kimsingi napenda niwaambie jambo moja eji kizazi cha nyoka.
Haya yote ni matokeo ya kukaa mbali na neno la MUNGU aliye hai na anae ishi. Vijana wa sasa mnaabudu watu na kusikiliza maagano na maagizo ya wanadamu bila kujua haya huwapeleka moja kwa moja katika kufeli na kuishi maisha ya mateso, manyanyaso, mafarakano na kudhalilika kunakowaachia mkiwa wafu wanaotembea na kukosa hadhi ya utu.
Kimsingi, ndoa ni taasisi inayojengwa katika misingi ya ki MUNGU na si kidunia.....
Leo wengi wetu tunaingia tukiwa katika najisi ya uzinzi kwa maana tumeshatembea sana na watu tofauti kiasi kwamba miili yetu haina tena thamani kwa wale walioiona.... Hebu wazia wewe ni mke wa mtu ambae ulishawahi kuwa na mahusiano kadhaa nyuma lets say watu watatu kabla ya mumeo, wataka niambia kesho badala ya ndoa yako nyakati za magumu ya ndoa ukakutana na yule mzinzi mwenzako utakuwa salama na kujizuia kusaliti ndoa yako?!
Ni ngumu sana kujizuia kwa mtu ambae alishautazama huo mwili na kuchovya tupu yake kwako kulikoni mtu mpya ambae una uhakika hajui lolote juu ya mwili wako.
Hebu tujiruhusu kutambua kuwa tunamkosea MUNGU kwa kukiuka maagizo yake.
Kitendo cha kusema hutaolewa au kuoa na ile hali hauna sababu ya kimwili kukuzuia kufanya hivyo ni labda ukae maisha yako yote bila kufanya zinaa ila kama wajua utaendelea kufanya zinaa basi kaa ukijua hakuna la maana umeepuka ni heri ungeteseka katika ndoa mateso yako yangekuwa ya hekima kuliko furaha ya zinaa ambayo itakuja kukuacha na aibu utakayokwenda nayo kaburini.
Vijana mrejeeni MUNGU na kuyaelewa mafundisho yake nyakati hizi ngumu ambazo kuzishika amri za MUNGU huonekana ni jambo la ajabu na ni la kituko. Hebu msiogope kushika maandiko yake pale unapopitia nyakati ngumu basi mrejeeni MUNGU na mafunzo yake awatie nguvu na kuwaongoza.....
Hizo kero ni za muda tu na panapo MUNGU amani ya kweli hupatikana.
Mrejeeni MUNGU, acheni ufahari na ujuaji.
Sent using
Jamii Forums mobile app