Watu wenye pesa/mafanikio wako very humble

Watu wenye pesa/mafanikio wako very humble

Ukiona mtu mwenye pesa anafanya fujo yaani ulimbukeni wa matanuzi wengi huwa ni mafisadi, wazee wa ndagu, wazee wa madini, watumishi wa umma.
Huwezi kuta mfanyabiashara mpambanaji anafanya fujo kwake kila2 shilingi mia inayo thamani.
Waajiriwa Wanapesa kuliko wafanyabiashara lakini wafanyabiashara Wana maendeleo kuliko waajiriwa.
 
ukweli utabaki kuwa ukweli tu, japo uzi umejaa vichumvichumvi kiasi, ila uko straight kabisa watu wenye mafanikio ya kweli hawana longolongo wala kujionyesha onyesha kama hawa chawa wanaopiga picha mitandaoni na magari ya mabosi wao. Be humble dunia haihitaji mbweeeeembweeeeeeee.
 
Ukiona mtu mwenye pesa anafanya fujo yaani ulimbukeni wa matanuzi wengi huwa ni mafisadi, wazee wa ndagu, wazee wa madini, watumishi wa umma.
Huwezi kuta mfanyabiashara mpambanaji anafanya fujo kwake kila2 shilingi mia inayo thamani.
Waajiriwa Wanapesa kuliko wafanyabiashara lakini wafanyabiashara Wana maendeleo kuliko waajiriwa.
Well said, mkuu.
 
Habarini za wakati huu wakuu.

Nimegundua kwamba watu wengi (siyo wote) wenye pesa/mafanikio ya kweli wako very humble. Hadi naanzisha huu uzi, yapo matukio mengi yamethibitisha conclusion hii.

Jana jioni nilienda Morena Hotel Dodoma kujipumzisha. Nikiwa pale nikakutana na rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu. Akaomba ani-join kwenye meza yangu. Alikuwa anakunywa maji makubwa. Tukawa tunastorisha, akaniambia kwa sasa yeye ni Mhandisi binafsi, aliacha kazi Serikalini akaamua ajiajiri.

Tukiwa tunaendelea na story, nikapigiwa simu na business partner wangu, akaja kutu-join. Kwanza partner alipofika tu alikuwa kaning'iniza funguo za gari kwenye lux, alipofika mezani akazitoa kiunoni akazianika mezani, sambamba na iphone zake mbili. Nikamtambulisha story zikaendelea.

Story zikiendelea, partner akapigiwa simu na client ambaye tunamdai, badala ya kwenda kuzungumzia pembeni au kwa sauti ya chini akawa anapayuka kwa kutaja hadi kiasi cha pesa tunachomdai akidhani kwamba kama ni kiasi kingi kwetu basi ni kingi kwa kila mtu. Sikushangaa kwasababu nimeshamzoea, yeye ni mtu flani hivi (wakubwa mmenielewa).

Baada ya muda kidogo Mhandisi akaagiza Hennessy VSOP Cognac ya 700ml. Akatuambia na sisi tuagize. Mimi nimeacha pombe, nikaagiza grand malt na coke. Nikamuona partner ana wasiwasi, uso wake umesawajika, ni kama alikuwa anajiuliza kuhusu bill. Akaagiza Heineken, akaletewa 6! Bill ikaja, Mhandisi akalipa, alikataa kabisa kushea au sisi kulipa. Taratibuuu, partner akachukua funguo za gari na simu mezani akaweka mfukoni [emoji28].

Mhandisi akanywa Hennessy kidogo tu, ingine akabeba, akaomba tuhame pale, partner naye akabeba Heineken zake.

Ile tunafika parking, Mhandisi anasukuma Toyota Land Cruiser V8 VXR nadhani ni ya 2021 ile, partner ana Toyota Vanguard yake, akawa mpole sana. Msiulize mimi naendesha nini [emoji3]...

Mhandisi akaomba tumfate nyuma. Break ya kwanza Bambalaga. Aisee partner alilewa mpaka anauliza pale tuko wapi!

Tukaagana usiku wa saa saba, tukabadilishana contacts. Leo saa tatu asubuhi Mhandisi kanipigia, kuna mradi "X" amepata tender hapa Dodoma. Anataka tuwe Wanasheria wake, yaani tufanye 'retainership agreement', na anatulipa kwa mwaka mzima, leo hiihii amesha-deposit malipo yetu yote ya mwaka in millions. Partner amebaki mdomo wazi!

Mhandisi ni mpole sana. Anachagua maneno ya kuzungumza. Hana mbwembwe yeye ni vitendo tu.

Hii siyo scenario ya kwanza, ziko nyingi sana.

Kwahiyo ukiona mtu anajisifia sana, anaonesha possessions zake hadharani ili kila mtu ajue, ujue hamna kitu hapo. Anafanya hivi ili kujilinda. Kuna kitu najifunza hata whatsap status za matajiri ni tofauti sana na za masikini. Matajiri wengine huwa hawapost kabisa au wanapost mara mojamoja, na wakipost hawawezi kupost fitina au majungu.

Hata humu JF, wadau ambao wako vizuri sana huwezi kuwaona ni wajuaji. Hata namna wanavyo-comment au ku-post, ni tofauti sana na masikini na waigizaji wa maisha.

Maisha ni safari ndefu, naendelea kujifunza..
Tunaomba kufahamu ulikuwa na gari yako au ulitegemea usafiri wa bajaji au bodaboda (be honest)
 
Tunaomba kufahamu ulikuwa na gari yako au ulitegemea usafiri wa bajaji au bodaboda (be honest)
[emoji28][emoji28]

It's very illogical kwamba magari yako 2 (la Mhandisi na la partner) and yet mimi nitumie bajaj/bodaboda [emoji2][emoji2]...

Usafiri wangu sitautaja hapa kwasababu wadau watahisi najimwamba-fy [emoji41][emoji41].
 
Funguo ziwekwe mfukoni. Mara nyingi suruali au pensi inakuwa na mifuko 4, miwili ya mbele na miwili ya nyuma. Mmoja wa nyumba unaweza kuweka wallet, mwingine wa nyuma weka handkerchief kama unayo. Mmoja wa mbele weka simu, na mwingine wa mbele weka funguo za gari na nyumba.

Point hazina mashiko coz kwanza kabisa simu ina screen protector, halafu mifuko ina usalama sana hata ukilewa, unless mtu aje akusachi.
Yaani niweke funguo yenye ncha mfukoni,, si kila sku ntakua nafanya kazi ya kushona mifuko kwa fundi. Kumbka funguo zenyewe sio za solex kama unavofikiria,,, funguo ni za aina hii👇👇.
IMG_20230314_105435.jpg

IMG_20230314_105407.jpg

Alafu ktu kngne ni mazoea,,, mm tangu nimejitambua,,, sjawahi weka funguo mfukoni,,, bi either kwenye lux au nikivaa penz nazishika mkononi,, sio show off lakn its just mazoea
 
Nimemiliki gari tatu na sijawahi ning'iniza funguo kiunoni wala kushika masimu nimetembea nayo mkononi.

Ninapomuonaga mtu anaeendesha gari akiwa amening'iniza mafunguo mengi kiunoni au anayachezea chezea na kuyatandaza mezani hua namshangaa sana!
 
Funguo zako za gari hua unaziweka mfukoni au??
 
Yaani niweke funguo yenye ncha mfukoni,, si kila sku ntakua nafanya kazi ya kushona mifuko kwa fundi. Kumbka funguo zenyewe sio za solex kama unavofikiria,,, funguo ni za aina hii[emoji116][emoji116].
View attachment 2550258
View attachment 2550264

Alafu ktu kngne ni mazoea,,, mm tangu nimejitambua,,, sjawahi weka funguo mfukoni,,, bi either kwenye lux au nikivaa penz nazishika mkononi,, sio show off lakn its just mazoea
Magari ya kisasa hayatumii funguo za namna hii mkuu [emoji28][emoji28]...
 
Nimemiliki gari tatu na sijawahi ning'iniza funguo kiunoni wala kushika masimu nimetembea nayo mkononi.

Ninapomuonaga mtu anaeendesha gari akiwa amening'iniza mafunguo mengi kiunoni au anayachezea chezea na kuyatandaza mezani hua namshangaa sana!
[emoji1666]
 
[emoji28][emoji28]

It's very illogical kwamba magari yako 2 (la Mhandisi na la partner) and yet mimi nitumie bajaj/bodaboda [emoji2][emoji2]...

Usafiri wangu sitautaja hapa kwasababu wadau watahisi najimwamba-fy [emoji41][emoji41].
Mpaka hapo ushajimwambafy ww ni mwenye nazo sabab unavojitahidi kwamba hujioneshi kama patna, vile ulivotuaminisha wenye nazo ni watu hamble japo umesahau wahaya mwenye nazo na kapuku huwezi watambua kirahis wote wanavimba
 
Back
Top Bottom