Si mmekataa serikali ya majimbo lakini! Huu mfumo ungeleta maendeleo sana hasa mikoa yenye rasilimali kubwa kusaidia mikoa ya jirani yake ambayo iko less fortune.
Mkuu, kwa kweli kwa sasa Tanzania ilipawa kuendeshwa ki-majimbo tena yasizidi 7. Serikali ya Majimbo huleta maendeleo ya haraka kwenye Jimbo na Nchi kwa ujumla. Majimbo yote yapo vizuri kiuchumi. Kwa mfano:- 1. JIMBO LA KUSINI; kuna Korosho, Tumbaku, gas, madini, mafuta, makaa ya mawe, bandari, uvuvi n.k; 2. JIMBO LA PWANI: korosho, uvuvi, viwanda, kilimo, bandari, kiwanja cha ndege, gas, madini n.k; 3.JIMBO LA KASKAZINI MASHARIKI: bandari, mkonge, kahawa, madini, utalii, uvuvi, mifugo n. k; 4;
JIMBO LA KASKAZINI: Madini, mifugo, uvuvi, pamba, kahawa utalii n.k; 5; JIMBO LA KATI: Madini, Zabibu, Alizeti, mifugo, viwanda, utalii n.k;
6. JIMBO LA MAGHARIBI: Madini, uwindaji wa kitalii, uvuvi, mawese, nk; 7 JIMBO LA KUSINI NYANDA ZA JUU; madini, uvuvi, Kahawa, vanilla, pareto, mbao, chai, makaa ya mawe n.k..
Mazao mengine yote ambayo hayakutajwa kwenye majimbo yanapatikana kwenye majimbo karibia yote.
Kwa mantiki hiyo kila JIMBO LIPO VIZURI